pole mama yetu, uzazi ni mapenzi ya Mungu

Ms Judith

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
2,563
918
Aliyejifungua mapacha watano atoboa siri



na Ali Lityawi, Kahama




SHIJA Maige, mkazi wa Kata ya Bulungwa, wilayani Kahama ambaye hivi karibu alijifungua mapacha watano, amesema alikimbia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mjini Mwanza kwa kuwa tangu watoto wake waanze kufa hajawahi kuona maiti zao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Shija alisema yeye alikuwa amelazwa wodi namba nne huku watoto wake wakiwa wodi namba mbili na kwamba alikuwa akienda wakati wa kuwanyonyesha tu, lakini kila alipokuwa akienda alikuta kuna upungufu wa watoto wake bila wauguzi kumuonyesha maiti zao.

Mwanamke huyo ambaye alishawahi kuzaa watoto mapacha wawili katika mimba zake sita alisema pia alilazimika kukimbia kwa kuwa wanawake wenzake waliokuwa wamelazwa naye walikuwa wakimwambia kuendelea kuwepo katika maeneo hayo hata yeye angepelekwa machinjioni walikokuwa wakipelekwa watoto wake.

Alidai kuwa hata mumewe aliyekuwa amefika siku moja kumuangalia alikuwa ameshauawa, hali ambayo ilimfanya atoroke na kumuacha mtoto wake mmoja aliyebaki.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Meja mstaafu Bahati Matala, Ofisa Tawala wa Wilaya ya Kahama, Paulo Cheyo, alisema kutokana na madai ya mama huyo aliuagiza uongozi wa hospitali ya wilaya kuhakikisha suala hilo linafanyiwa kazi na mama huyo anarudishwa hospitali ya Bugango chini ya uangalizi wa muuguzi kutoka hospitali hiyo.

Cheyo alisema mbali ya hilo, ofisi yake inahitaji kupata ufafanuzi wa kina kuhusu mama huyo tangu alipokuja katika Hospitali ya Wilaya hadi kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando na pia mama huyo aende katika hospitali ya Bugando kujiridhisha juu ya kufariki kwa wanawe.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Heleni Membe alisema kuwa maneno anayoongea mama huyo yanatokana na kuchanganyikiwa baada ya kupata kifafa cha uzazi na kufariki kwa watoto wake hao wanne.
 
Which is which??

SHIJA Maige, mkazi wa Kata ya Bulungwa, wilayani Kahama ambaye hivi karibu alijifungua mapacha watano, amesema alikimbia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mjini Mwanza kwa kuwa tangu watoto wake waanze kufa hajawahi kuona maiti zao.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Heleni Membe alisema kuwa maneno anayoongea mama huyo yanatokana na kuchanganyikiwa baada ya kupata kifafa cha uzazi na kufariki kwa watoto wake hao wanne.
 
that is the role of a woman in the society. she bears all the agony on her shoulders. pain in childbirth, kifafa cha uzazi na sasa anawalilia watoto wake who are no more! huenda pia imani za kishirikina zinautafuna moyo laini wa mama huyu bila huruma, majirani zake wodini waliopaswa kuwa mstari wa mbele kumfariji, wamegeuka kumtisha.... its all that confused her. ooh Lord have mercy on the poor woman
 
mzazi ana haki ya kuona maiti ya wanawe kama hajaonyeshwa basi madaktari na uongozi mzima wa hospitali lazima uwajibishwe waleleze zilipo maiti za hao watoto.Tutajuaje kama wamewauza hao watoto? tutajuaje kama wamewauwa ili kuwafanyia medical experiments? kisheria wana hatia na hata majibu yao yanaonyesha wazi kuna kitu hapo.wanasheria waliopo mwanza na kahama hebu msaidieni huyu mama apate haki zake.Kama angekuwa na kichaa cha mimba kajuaje idadi ya watoto aliowazaa na anajuaje wanatakiwa kunyonya? haingii akilini.
 
ee Mungu wangu sikia kilio changu uyasikie maombi yangu
toka mwisho wa nchi nitakulilia, nikizimia moyo
ee Bwana wangu na Mungu wangu
ee Bwana usiniache X2
ii Bwana, dunia hii ni taabuni,
ee Bwana usiniache

source: ST. James, Tumaini choir, kaloleni, arusha katika album yao ya Shangilieni #2, wimbo usinipite Mwokozi

ee Mungu sikia kilio cha mzazi huyu, uyasikie maombi yake maana amekulilia toka mwisho wa nchi akizimia moyo. amen
 
Back
Top Bottom