Points 10 za ujenzi: Chumvi katika jengo

greater than

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
797
1,226
MAKALA YA 4
Karibuni katika Makala yetu ya Ujenzi,Ambapo dhana na lugha ngumu ya Kitaalam inageuzwa kuwa nyepesi na kueleweka.
Leo japo kwa ufupi tutajadili kuhusu suala la "Chumvi kwenye Jengo"

1.CHUMVI KATIKA JENGO : Hii ni moja ya athari na matokeo ya Dampness/unyevu katika sehemu za Jengo.
Katika kila Majengo 15 uyaonayo ukiwa mizunguko kuna ma4 ambayo yanakumbwa na kadhia hii ya Chumvi Chumvi kwenye Kuta,Slab au Msingi wa jengo.
Aina za element za chumvi ni Sodiam,Potashiam,Kalshiam,Magneshiam,Kloraid,Salfeti,Kaboneti na Naitreti.

2.CHANZO : vyanzo vikuu vya Chumvi katika jengo.
I) Ujenzi katika eneo lenye Udongo wa maji chumvi au maji chumvi.
Ii) Shughuli za kibinadamu mf. Ufugaji,
III) Bahari
IV) Matilio

3.USAMBAAJI : Chumvi Kwenye jengo usambaa kwa njia kuu tatu.

i) Unyevu unaopanda:hapa unyevu upanda kutoka kwenye Ardhi kwenda kwenye Jengo kupitia Msingi au Sakafu.
Ambapo maji hayo huwa na Chumvi ndani yake
-Hii hutokea pale unapojenga kwenye eneo ambalo udongo wake una chumvichumvi
-Namna ya kuyajua maeneo yenye chumvi:
a.maeneo yenye mikoko namatoresheo ya maji ya bahari. mf.Kunduchi Kilongawima na Ununio,Somangira na Geza.​
b.Maeneo yenye Udongo mweusi ambapo kipindi kirefu cha mwaka utaona umelowa​
Mfano;Mikocheni A,Bonde la Mpunga (Msasani),Bwawani(Mwananyamala).​
c.Maeneo ambayo kuna Visima vifupi ,vyenye maji chumvi​
-Kuangalia mimea, Kuna mimea kuota kwenye udongo wa chumvi mf.upupu,

4.USAMBAAJI
ii.Unyevu Unaopenya: Hapa Hupenya kwenye Ukuta moja kwa moja.
-mvua ikinyesha na matone yake, yanarusha udongo wa chumvi ukutani​
-Chumvi inayopeperushwa kutoka baharini kwenda kwenye majengo​
-watu,Viumbe hai kukojolea ukutani.​
- maji kutoka mazizi ya wanyama kugusa ukuta.​
Nyumba za ukanda wa pwani huathiriwa sana na chumvi ya baharini.

5.USAMBAAJI
(iii)Matilio zenye Chumvi : kwenye njia hii ya tatu, Hapa watu hujenga kwa kutumia
-matofali yenye chumvi.​
Utajuaje​
Unapoenda kununua,haya. matofal katikati ya nyuso yana weupe.​
- Mchanga wenye Chumvi Utakuta mchanga una rangi. kama ya kahawia(Dar)​
- Maji ya chumvi Maji yanakuwa na radha ya magadi​

6.VICHOCHEZI : Ongezeko la Chumvi kwenye jengo lako,huchochewa na
i) Kiwango cha maji :
chumvi ili ipenye kuwa katika sehemu za jengo na kupenya huitaji uwepo wa unyevu/maji

ii) Joto :
uwepo wa joto, huvukiza maji yaliyo kwenye kuta na kubakisha chumvi.
-ndiyo mana mikoa pwani huathiriwa sana na chumvi kwasabu ya joto la pwani

iii) Upenyeshaji wa matilio :
matilio huwa na vitundu vidogo sana, ndipo maji hupenya na chumvi zake
Mf.Matofali ya BamBam ,vitundu huwa vingi kuliko tofali za Umeme.

7.Athari : chumvi ina athari nyingi sana kwenye jengo,hii ndiyo hufanya majengo ya ukanda wa Pwani na joto ,yasidumu kuliko majengo ya Mikoa yenye ubaridi.
-Chumvi humeng'enyua matofali
-Huaribu rangi
-Huaribu matilio za metali I.e Kopa, Aluminium
-Huarakisha kutu katika nondo
-Huaribu kwanza kuondoa ung'avu wake kisha uweka kutu.
-Huaribu mbao.
-Huaribu zege
-Upunguza maradufu uhai wa jengo.
 
8.KINGA : (Kabla ya Ujenzi )
ni ngumu kulikinga kwa 100% jengo kuathriwa na chumvi ila unaweza punguza nafasi ya chumvi kwenye jengo kwa njia zifuatazo.
I) Ondoa udongo wa chumvi na / au weka kifusi cha udongo mwingine
Mf. Kabla ya Mayfair plaza kujengwa walifanya hivi.
Tahadhari
Usijenge kwenye machepuo ya bahari au kwenye mikoko.hapo hata kifusi magari 1000 ,chumvi itapanda tu.​

II) Ondoa mikondo ya maji yote inayoelekea kiwanjani kwako.

(Kipindi Cha Ujenzi)

I) Usitumie matilio zenye chumvi.Epuka mchanga,Matofali au maji chumvi.

II) Tumia matilio imara:Tumia
-Matofali magumu ya umeme au ya kuchoma.​
-Simenti maalum yenye kuendana na eneo la chumvi (kama mradi mkubwa)​
-Mabati imara yenye kinga dhidi ya kutu.​
III) Utumizi wa vidhibiti Unyevu (waterproofing materials).
-Uwekaji wa DPC wakati wa ujenzi wa Msingi
-kemikali za vidhibiti Unyevu, kuchanganywa na screed

(Baada ya Ujenzi)
i)
Kutofanya mifugo karibia na jengo lako.
ii) Bustani Isikaribiane na ukuta, kwani mbolea ya bustani nayo ina chumvi
-kuwe na umbali wa mita 0.5 kutoka bustani hadi ukutani.
Iii) kutokukojoa ukutani
Iv) Kuhakikisha maji hayatuwami katika eneo lako.

9. KINGA NA MAREKEBISHO KWA SEHEMU ILIYO ATHIRIKA
Namna ya kurekebisha Sehemu ya jengo ambayo imeshakwisha athirika.
I) Uwekaji wa Plasta au Mota nyepesi kwenye ukanda wa chini wa UK kuta, ili kuruhusu eneo hilo tu kushambuliwa

II) Kuondoa sehemu ya base ya ukuta na kuweka tofali mpya.

III) Kukata Sehemu ya Base ya Ukuta na kuweka DPC
IV)Electro-Osmosis, kutumia umeme

Tahadhari
Ukuta ulioathriwa na Chumvichumvi usije ukarabati kwa plasta imara kwa juu na skimming na kuweka rangi ya mafuta,,hapo utazuia mvukizo, na chumvi itaharibu ukuta kwa ndani au kuhamia upande mwingine

10.Kabla ya ujenzi, tafuta mtaalam akupe ushauri kwanza, awe Mwanajiolojia, Mhandisi Ujenzi au Msanifu.
Fundi ujenzi hatoweza kukupa hizi taarifa.

Nakaribisha maoni, maswali.
-Tuma swali likiambatana na picha za sehemu yako yenye shida
-Picha ziwe angalau nne
Kama unataka privacy, mni PM
 
Mwezi wa 4 naingia likizo
Kwa mwenye kuhitaji kutembelewa katika eneo lake, kukagua na kutoa ushauri juu ya tatizo lolote, kuwa huru kunijuza.

Gharama : Huduma hii ni bure
Usafiri : ndiyo pekee utagharamia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom