Plane crash at Kabuku!

Mdadisi

Member
Aug 1, 2007
55
2
Nimetumiwa text msg kuwa kuna ndege imeanguka punde na kugonga gari eneo la segera na barabara imefungwa. Wadau mnaombwa kufuatilia news hii

======
UPDATE:

It's confirmed, ndege imeanguka eneo hilo (maeneo ya Kabuku) na imeliangukia gari ambalo inahisiwa ni la watalii, mwandishi wetu anafuatilia kwa karibu tutawafahamisha zaidi
 
Zipo taarifa kuwa ndege inayosadikiwa kumilikiwa na Jeshi imenguka barabarani katika barabara Kuu Chalinze-Segera eneo la Kabuku na mtu mmoja amepoteza maisha hadi sasa. Inasidkiwa iligongana na gari la watalii. Barabara hiyo haipitiki kwa sasa. Na kama ada uokoaji wetu ni duni sana vyombo husika havijafika eno la tukio.
 
Wadau nasikiliza CloudsFM hapa; kuna ndege imedondoka katikati ya barabara na kugonga lori lilokuwa imebeba watalii huko Kabuku Tanga.

Mpaka sasa inasemekana watu wote waliokuwa kwenye ndege wamekufa kwani imeharibika vibaya na ilikuwa ikimilikiwa Jeshi ; kambi ya Ngerengere!

Wenye habari watujuze zaidi
 
Tafadhali waleta habari wawe specific.wengine wanasema Segera wengine Kabuku nashindwa kuelewa ni sehemu gani haswa hiyo ajali imetokea.Kuna umbali mkubwa kutoka Kabuku na Segera almost 21 km,tena kuna vijiji vingi btw eg Michungwani,Chang'ombe,kwedizinga na nk.
 
Wale madalali weu wanaouza ndege chakavu wakidhani ni vyuma chakavu wanasikia haya?
 
ni kabuku wadau,kuna mdogo wangu yupo kwenye basi anaenda arusha ndio kanipa habari.
 
Majanga haya yataishi lini, kila siku ni ajali MUNGU TUNUSURU NA HAYA
 
Tafadhali waleta habari wawe specific.wengine wanasema Segera wengine Kabuku nashindwa kuelewa ni sehemu gani haswa hiyo ajali imetokea.Kuna umbali mkubwa kutoka Kabuku na Segera almost 21 km,tena kuna vijiji vingi btw eg Michungwani,Chang'ombe,kwedizinga na nk.
Wengine wanasema MBWEWE!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom