Pinda azidi kushangaa

Huyo pinda wala hana jipya, yeye awe wa kwanza kutumia bajaj na wengine ndo wafuatie.
 
Hainishtui, hata Muungwana alikiri mwaka huu mwanzoni kwamba hajui kwanini Tanzania ni masikini.

Hayo pia yaliwahi kutamkwa na waziri mkuu mstaafu Sumaye baada ya kukaa miaka 10 kama waziri mkuu, akaenda kusoma marekani na alipograduate akakiri alikuwa hajui kwa nini Tanzania ni masikini mpaka alipoenda kusoma.

Vijana nchi hii wamelala mno, siku wakatae kuishi mbagala na kuparamia na kuchoma moto nyumba zote Masaki, Oysterbay na mbezi beach labda ndio vingozi wetu watajua maana ya nchi kuwa masikini na kubana matumizi.

Mashangingi ya serikali yanajazana Bar na mahotelini weekends, yanafanya nini??
 
Huyu PM anaendelea kupoteza muelekeo. Yaani mpaka aende india ndiyo aone kuwa viongozi wanatumia magari ya bei raisi hatua ndiyo zichukuliwe? Hapo tumepata hasara kubwa sana.

So wakati anasema watasimamisha ununuzi wa mashangingi alikuwa anarefer wapi? Waache usanii waongee facts!! We are tired.

Analaumu mawaziri kununua mashangingi sini wao kwenye baraza analoliongoza ndiyo wote kwa kushirikiana wanapitisha maamuzi ya kuyanunua? SASA ANASHANGAA NINI?

Hapa ili aleweke lazima aseme kuwa mashangingi yananunuliwa kwa kiasi fulani hivyo kwa kuamua kununua magari madogo tunasave kiasi fulani kitakachopelekwa kwenye secta fulani. SIYO SIASA TU.

ACHENI KWENDA KUTEMBEA HUKO NENDENI KUJIFUNZA KWA VITENDO SI MANENO.
 
aendelee kushangaa fleet ya state of the art BMW na top of the range vehicles zinazonunuliwa kwa mkuu wa kaya kila toleo au model mpya inapoingia sokoni. haipandi kabisa kwamba jitu limeliwa na mifunza sawasawa utotoni na kusahau limetoka wapi. miafrika mingine inakera kweli kweli!
 
Baada ya kupagawishwa na kilimo cha Korea Kusini, Mheshimiwa Pinda leo anatusimulia maajabu aliyoyaona India.

--- Nanukuu ---

“I was in India recently and I was surprised that ministers are using very ordinary vehicles. Here it is different, although we are very poor, we are competing in buying the most expensive vehicles. Ministers, Members of Parliament, Permanent Secretaries, regional commissioners, municipal directors, and administrative officers are driving luxurious vehicles,” Premier Pinda lamented during his meeting with livestock stakeholders in Dodoma.

--- Mwisho wa kunukuu ---

Source: http://www.dailynews.co.tz/home/?n=4118[/QUOTE]

10.JPG

steved-albums-mh_pinda-picture166-msafara-pinda-morogoro-mjngw1.jpg


...hata wao 'wanatushangaa!'...​
 
Namuunga mkono Keil kwa 100% Kwani nini kinamzuia kusema "Naagiza kwamba kuanzia sasa viongozi wote wa serikali, ukitoa Rais na Makamu wake, watumie magari yasiyozidi cc 2000. Wenye magari yanayozidi ukubwa huo wawe wameyarudisha Wizara ya Ujenzi ifikapo 31 Dec 2009" ili yauzwe". Kwa kuongoza kwa mfano angeendelea kusema "hata mimi nitaumia gari aina ya Suzuki ya cc 1800". Hivi ndivyo alivyofanya Uhuru Kenyatta, Waziri wa Fedha na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya.

Pse Pinda be serious. You have immense powers. Wield them. La sivyo nyamaza. Waache wananchi walalamike.
 
haya kushangaa shangaa kumetosha, sasa suala ni kwama ataifanyia kazi vipi hiyo mishangao yote? ili akienda safari ijayo asishangae tena

Mkuu hii sio mara ya kwanza Pinda kuongelea suala la magari ya kifahari kwa viongozi. Alishasema badala ya kununua mashangingi serikali itanunua matrekta. Mie namshangaa kuwa bado anaendelea kushangaa badala ya kutoa maagizo.

Viongozi wetu wana matatizo ya akili, utafikiri hawajaenda shule au wameenda kushangaa majengo na hawakuelimika, aibu tupu.
 
Baada ya kupagawishwa na kilimo cha Korea Kusini, Mheshimiwa Pinda leo anatusimulia maajabu aliyoyaona India.

--- Nanukuu ---

“I was in India recently and I was surprised that ministers are using very ordinary vehicles. Here it is different, although we are very poor, we are competing in buying the most expensive vehicles. Ministers, Members of Parliament, Permanent Secretaries, regional commissioners, municipal directors, and administrative officers are driving luxurious vehicles,” Premier Pinda lamented during his meeting with livestock stakeholders in Dodoma.

--- Mwisho wa kunukuu ---

Source: http://www.dailynews.co.tz/home/?n=4118

Hivi huyu Pinda anayeshangaa haya, ANATUMIA GARI GANI? Hivi alishawahi kujishangaa yeye mwenyewe kwa aina ya gari anatotumia? NINACHOKIONA NI KUWA ANATAFUTA KUONEKANA ANA HURUMA NA PESA YA SERIKALI. Haiingii akilini kuona anashangaa wakati yeye ana gari aina hiyo hiyo anayoishangaa. Mi nadhani ni unafiki tu kushangaa. YETHUUU NA MARIA KWENYE HUU UCHAGUZI TUONA MENGI ATIIII.........
 
Bhaghosha,

Haya mambo ni kama vile hawa viongozi watwangiwa maji kwa kinu last time PM Pinda alitamka hilo swala kwa Mjengoni kule Dodoma jamani tuangalie budget za wizara zetu katita ununuzi wa magari ya kifahari sijui sasa izi Government office zakaguriwa na nani ktk budget zao za ununuzi wa magari??? Hilo alilo lisema PM kuhusu kulingishiana magari ni kweli na limeishafika mpaka majumbani kwa hao viongozi unakuta mtu kaagiza Benz kari tizama thamani yake uone? Sasa napenda kuwa kumbushia hioli swala limetokea Kenya tu hapo nchi jirani Waziri Uhuru Kenyatta aliwambia viongozi wenzake warudishe magari yote ya kifahari DT Dobi Toyota na wale wa Toyota hawakubisha na waliya chukuwa yale magari na wafanyakazi 10 ndani ya ikulu ya kenya walifukuzwa kazi kwani kwanza waligoma kuyarudisha. Huo ndio mfano wa uongozi wa Katiba na sheria.

Sasa hapa kwetu wakati wa budget huwa kuna mchezo mchafu huchezwa kabisa, kwani siamini kuwa pesa zilizo baki kwa budget iliyopita kwa kila wizara husika kama hurudishwa kwanza na kupangiwa upya ktk mwaka mwingine wa budget??

Jamani tunapigo kubwa sana hapa nchi Huduma mbovu na kutokuwepo na vitendea kazi vya kisasa ktk mahospitali yetu na husababisha vifo vya kiana mama wajawazito na watoto wachanga na ugonjwa wa maralia unao waua watoto kati ya mwaka mmoja hadi miaka 5,

Ivi kweli jamani kuna haja kubwa sana ya kumchagua mgombea atakaye tupigania kwa hayo japo ni machache ndugu zangu tujisikitieni sie kwa vizazi vijavyo.

Ntasistahajabika sana tumeshindwa boresha haya ya hospitali miundombinu maji hata madini tu kama dhahabu na alumasi twataka kimbilia Uleniam.

TUSIDANGANYIKEEEEEEEEE watanzania wenzangu hojini kila mkionacho si sahihi
 
hivi huyu naye tulitoka naye wapi?mbona anaongea ongea vitu senseless,anang`ang`ana magari ya kifahari mbona yeye hatumuoni anapanda landrover 109?mi natamani kutapika juu ya huyu PM jamani...
 
Usanii mtupu.

Hapo ndipo Scarface anakwambia "Don't talk, shoot".

Wewe PM una government on your shoulder all this time then unashangaa shangaa tu bado?
...well he seems to be 'getting high on his own supply'....watamkatia hizo ziara sasa hivi.
 
Ninakubaliana na wewe, lakini cheo hicho kinaweza kuwa na maana iwapo aliyepewa ana msimamo unaoeleweka.

Tatizo la Pinda ni kwamba anatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Anahakikisha anamtumikia JK hivyo inabidi akubaliane nae, na pia anamtumikia EL kama mlinzi wa maslahi ya mafisadi. Kwa mwendo huo lazima Pinda atakuwa anachemka saa zote.

PM anatakiwa kuwa na msimamo na asiwe bendera fuata upepo, sasa kama kiranja mkuu wa mawaziri anaanza anaanza kushangaa sisi wengine tufanye nini?

Mkuu Keil,
Asante kwa maelezo mazuri sana. Ila mie naungana na member uliyemjibu kuwa PM Tanzania ni kupoteza tu pesa. Hana nguvu zozote za kikatiba. Hawezi kumdisia Rais wake ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chake. Yaani kama ukitaka kusema kashikwa na EL basi sema kabanwa pande tatu. Yes, kabinywa in 3Dimensions. Kikwete kambana mara mbili na EL mara moja.
Nakumbuka nilivyojiunga JF, hili ndiyo lilikuwa swali langu la kwanza. Hadi kesho napinga kitendo cha Rais kuchagua PM na baadaye kumchagulia mawaziri na makatibu. Ukweli unabaki kuwa PM na mawaziri wake wote wako ngoma droo na wanaweza kumdisia. Tofauti ni moja kuwa PM akiondoka wanavunja baraza la mawaziri na waziri hawavunji. Na kuvunja na kuunda kwani ni kazi? Si ni kazi rahisi sana ya RAIS?

Nilitegemea Mkapa angelirekebisha hili kwani yeye lilimsumbua sana. Akiwa Waziri wa elimu ya juu na sayansi na Tech. katibu mkuu alikuwa Dr. Billal. Billal na Kigoma Malima walikuwa na tabia ya kuwaruka maboss wao na kwenda moja kwa moja kwa Mzee Ruksa kwa sababu alikuwa Muislam/Mzanzibar mwenzao. Hili tatizo nilishawahi liona hata nchi za wengine kwamba PM alichaguwa mawaziri wote kasoro wale wanne muhimu. Hawa alichagua kwa kukubaliana na Rais. Sasa yule wa mambo ya nchi za nje kwa kujua yuko pale kwa nguvu ya Rais, alikuwa anabisha na tena ubishi wa kitoto. Ugomvi wao ukawa wazi hadi kwenye TV.
Ndoto zangu ni kuwa siku moja ni chama tawala (huku Rais akiwa nje ya hicho chama hata kama ni chama chake) wanachagua PM bungeni na siyo State House. PM akichaguliwa anapewa uwezo wa kuunda baraza lake la Mawaziri. Hapo sasa tutakuwa "walau" na serikali ya kweli ya PM na siyo hii PAZIA iliyopo iitwayo PM. Tunaongeza tu wala vya BURE. Heri kila kitu kingebaki wazi kabisa kuwa Chama, Serikali na State house viko chini ya mtu mmoja na tusiwe tunaGAWA LAWAMA.
 
Back
Top Bottom