Pinda azidi kushangaa

Dar_Millionaire

JF-Expert Member
Aug 6, 2008
227
82
Baada ya kupagawishwa na kilimo cha Korea Kusini, Mheshimiwa Pinda leo anatusimulia maajabu aliyoyaona India.

--- Nanukuu ---

“I was in India recently and I was surprised that ministers are using very ordinary vehicles. Here it is different, although we are very poor, we are competing in buying the most expensive vehicles. Ministers, Members of Parliament, Permanent Secretaries, regional commissioners, municipal directors, and administrative officers are driving luxurious vehicles,” Premier Pinda lamented during his meeting with livestock stakeholders in Dodoma.

--- Mwisho wa kunukuu ---

Source: http://www.dailynews.co.tz/home/?n=4118
 
Ndio maana wenye kuelimika wanasema hiki cheo cha waziri mkuu ni sawa na bure...hakina maana yoyote.
 
Sasa anashangaa nini wakati yeye ni PM? Kwani hao wanaonunua hayo mashangingi si wako chini yake? Si ni serikali yake inayo andaa bajeti ama bajaeti huwa inaandaliwa na serikali nyingine na wao wanaletewa tu?

Mambo mengine ni aibu hata kuyaongelea, bora angekaa kimya. Wananchi hawajaanza leo kulalamikia matumizi ya magari ya bei mbaya. Watu walishatoa mifano ya Kenya, Uganda na Rwanda. Ila kwa kuwa serikali yetu ina itikadi ya ufisadi wala hawaelewi kilio cha wananchi.

Poor Pinda na sielewi anashangaa nini?!?!
 
Baada ya kupagawishwa na kilimo cha Korea Kusini, Mheshimiwa Pinda leo anatusimulia maajabu aliyoyaona India.

--- Nanukuu ---

“I was in India recently and I was surprised that ministers are using very ordinary vehicles. Here it is different, although we are very poor, we are competing in buying the most expensive vehicles. Ministers, Members of Parliament, Permanent Secretaries, regional commissioners, municipal directors, and administrative officers are driving luxurious vehicles,” Premier Pinda lamented during his meeting with livestock stakeholders in Dodoma.

--- Mwisho wa kunukuu ---

Source: http://www.dailynews.co.tz/home/?n=4118

Mkuu this is sad. Kama hata waziri mkuu hajui ambayo ordinary Tanzanians tunajua it is very sad indeed. Nimeshuhudia mawaziri wa nchi za magharibi ulaya wakitumia baiskeli, wakitembea wa miguu na kutumia magari ambayo huku kwetu tunayaita ordinary.
Nimesikia Japan viongozi hawatakiwi kutumia magari ya kifahari. Nimesikia China kuwa kama kiongozi ukitumia gari ambayo haiko kwenye orodha ya magari yanayotakiwa kutumiwa na viongozi, basi ni kigezo tocha cha kuondolewa madarakani, hawatumii magari ya kiwango cha chini lakini pia hawatumii magari ya kifahari. This is the knowledge i had 10 years ago, leo PM ambaye ni bosi wa usalama wa taifa anasema hajui hayo, nimkweli au ni kutuzuga. Mbona hapa JF kuna siku wadau walipiga picha msafara wake na kueleza sana hii kitu? bado tu alikuwa hajui?
 
haya kushangaa shangaa kumetosha, sasa suala ni kwama ataifanyia kazi vipi hiyo mishangao yote? ili akienda safari ijayo asishangae tena
 
Ndio maana wenye kuelimika wanasema hiki cheo cha waziri mkuu ni sawa na bure...hakina maana yoyote.

Ninakubaliana na wewe, lakini cheo hicho kinaweza kuwa na maana iwapo aliyepewa ana msimamo unaoeleweka.

Tatizo la Pinda ni kwamba anatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Anahakikisha anamtumikia JK hivyo inabidi akubaliane nae, na pia anamtumikia EL kama mlinzi wa maslahi ya mafisadi. Kwa mwendo huo lazima Pinda atakuwa anachemka saa zote.

PM anatakiwa kuwa na msimamo na asiwe bendera fuata upepo, sasa kama kiranja mkuu wa mawaziri anaanza anaanza kushangaa sisi wengine tufanye nini?
 
Usanii mtupu.

Hapo ndipo Scarface anakwambia "Don't talk, shoot".

Wewe PM una government on your shoulder all this time then unashangaa shangaa tu bado?
 
Baada ya kupagawishwa na kilimo cha Korea Kusini, Mheshimiwa Pinda leo anatusimulia maajabu aliyoyaona India.

--- Nanukuu ---

“I was in India recently and I was surprised that ministers are using very ordinary vehicles. Here it is different, although we are very poor, we are competing in buying the most expensive vehicles. Ministers, Members of Parliament, Permanent Secretaries, regional commissioners, municipal directors, and administrative officers are driving luxurious vehicles,” Premier Pinda lamented during his meeting with livestock stakeholders in Dodoma.

--- Mwisho wa kunukuu ---

Source: http://www.dailynews.co.tz/home/?n=4118
You'll even be surprised much more when you find that ministers, University Presidents, City Mayors in the third World Largest Economy are riding bicycles!
These appoint our learders not to lead us but to Learn!!
 
inaonekana kuwa hapa Tanzania uongozi unaonekana kwa kutumia respurces za serikali na sio kuperform.
 
CCM imechukua keki ya nchi nzima na wanafikiri itakuwepo daima na wataendelea kuila tuu mguu juu na kwamba haiishi.
Wameshazoea kuvuja mali mpaka hawajui kua mashangingi ni luxury. Pinda anashangaa nini, yaani mpaka leo hakujua gharama ya kununua na kuendesha hizo shangingi, ama kwa kua ni mali ya umma hakua hata na mpango wa kudadisi mpaka akaone India. Sisi raia tukisema kuhusu hizo shangingi wantupuuza na wanasema tunawaonea wivu tu na tuna roho mbaya, na wapinzani wakisema pia wanapuuzwa eti hawana jipya. Eti ninyi CHADEMA ni wakabila na msitegemee kushinda uchaguzi, lakini CCM eti ipo kwa ajili ya watu.
Mshangao wa Pinda yaonyesha wazi weakness yake, hawezi kabisa, yupo pale kama picha tu. Tatizo la TZ hata hujui power anayo nani badala yake raisi ama kila kiongozi wa serikali ya nambari wani CCM anashangaa shangaa tu eti kwa nini hatuendelei - jibu ni wazi TZ haiendelei tokana na UFISADI wa CCM na kutegemea wafadhili. Wafadhili wameilamaza CCM hata hawana hata aibu wala hawajui watendalo tena. Muulize Pinda, atakwambia TZ inaheshimika sana duniani.
 
Kama anaona Serikali ilikosea kununua hayo magari, ayachukue ayapige mnada. Ingawa tena hapo kutakuwa na ufisadi mwingine. Bongo kila mtu ni opportunist, anasubiria leo mkubwa kasema nini anatumia nafasi hiyo kujitengenezea pesa ipasavyo. Hiyo kauli ya Pinda ni kama ya kuwapumbaza watanzania na kuwaona wajinga.
 
Very sad, I knew our "leaders" were to say the least uninformed, but the extent of Pindas ignorance is quite surprising.
 
sasa anashangaa nini wakati yeye ni pm? Kwani hao wanaonunua hayo mashangingi si wako chini yake? Si ni serikali yake inayo andaa bajeti ama bajaeti huwa inaandaliwa na serikali nyingine na wao wanaletewa tu?

Mambo mengine ni aibu hata kuyaongelea, bora angekaa kimya. Wananchi hawajaanza leo kulalamikia matumizi ya magari ya bei mbaya. Watu walishatoa mifano ya kenya, uganda na rwanda. Ila kwa kuwa serikali yetu ina itikadi ya ufisadi wala hawaelewi kilio cha wananchi.

Poor pinda na sielewi anashangaa nini?!?!

......tatizo sio pinda ni pm bali mfumo wa serikali ndio unamfanya awe ktk kundi la walalamikaji.waziri mkuu wa tz sio mtendaji mkuu ktk baraza la mawaziri bali yupo kupokea maelekezo ya rais.
 
huyo ndo waziri mkuu Pinda aka mtoto wa mkulima..yeye kila kitu anashangaa tu
 
Hapana shaka Pinda ni kati ya viongozi wazalendo tulionao kwa nyakati hizi... Namshauri ajiuzulu kwa sasa ili heshima yake iendelee kuwepo kwa vizazi vijavyo.. maisha ni process na nilazima yakamilike!...
 
Hapo kwenye highlight, huo msamiati haupo kwenye kamusi za hawa waheshimiwa
 
mchanga wa macho huu!! Unless kama Pinda anaishi 'under a rock', hili ni swala lililo wazi sana kwa mtu mwenye exposure yeyote.
Ngojea tuone implication zake...but wait...awamu yake imeisha na campeni zimeanza!
 
Huyo pinda naye msanii tu, kwani yeye mgeni israel hii, au ni mbinu ya kujijenga kisiasa. cha kufanya yeye awe wa kwanza kutumia bajaj ili wengine wafuatie kwani kuongoza ni kuonyesha njia sio zile habari za fuateni ninayosema sio nitendayo! Haki ya Mungu pinda mugongo siku hizi anakera kwa vikauli vyake!!!
 
Back
Top Bottom