Pinda aondoka bila majibu mgogoro ranchi ya Missenyi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Monday, 14 March 2011 20:10
pindakilimokwanza.jpg

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda


WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema mapendekezo ya ufumbuzi wa mgogoro wa wawekezaji wa ranchi za Misenyi na wananchi, hayatatekelezwa bila kushirikisha wananchi wa maeneo hayo.

Pinda alitoa kauli hiyo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Bunazi Alhamisi iliyopita.

Alisema anasubiri kusoma taarifa ya makatibu wakuu waliokwenda wilayani humo hivi karibuni kuzungukia maeneo yenye migogoro na wawekezaji.
Baada ya kupitia taarifa hiyo, Pinda alisema watarejesha majibu kwa wananchi na kuwauliza kabla ya kuchukua hatua zozote zitakazokuwa zimependekezwa na timu hiyo.

“Lipo tatizo la historia na bado hatujafika mwisho, nasubiri taarifa ya 
makatibu wakuu tutaipitia na kuleta majibu, uamuzi hautafanyika kabla ya kuwauliza kwanza wananchi,” alisema Pinda.
 Awali, Mwakilishi wa wananchi hao, Abdallah Hassan, alimweleza Pinda kuwa mgogoro wa ardhi kati yao na wawekezaji, hauwezi kupata ufumbuzi iwapo viongozi wanaomiliki maeneo hayo wataendelea kulindana.

Hassan alisema wananchi hawawezi kupona kutokana na nguvu kubwa waliyonayo wawekezaji wanaoshirikiana na viongozi, ambao pia wamemilikishwa vitalu na kuendesha vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wananchi.
 Alisema viongozi mbalimbali wa kitaifa wamekuwa wakipotoshwa kuhusu ukweli wa mgogoro huo kwa madai kuwa, wananchi ni wavamizi huku historia ikionyesha vijiji wamekuwapo hata kabla ya ranchi ya Missenyi.


Aliendelea kuwa vijiji vilivyoathiriwa na mgogoro huo ni 
Kakunyu, Bubale na Bugango na kwamba, viongozi wanaofika huishia kupata maelezo ya Meneja wa ranchi, Ally Manjawa, bila kusilikiza wananchi.Mgogoro huo umeendelea kufukuta kwa miaka kadhaa sasa, wananchi wamekuwa wakilalamikia vitendo vya unyanyasaji, ukiwamo uporaji mifugo unaofanywa na viongozi wa wilaya na ubomoaji nyumba zao kama shinikizo la kuwahamisha.

Mwaka 2007, akiwa ziarani mkoani Kagera, Rais Jakaya Kikwete aliagiza wananchi wasisumbuliwe kwa sababu anakumbuka wakati wa vita ya Kagera mwaka 1978 alikuwa akipita kwenye mashamba hayo.Hata hivyo, kutokana na nguvu kubwa waliyonayo wawekezaji hao, imesababisha hata baadhi ya viongozi waliokuwa wakisimamia wananchi hao kuangushwa.
 
Ranchi ya misenyi ina vigogo wa serikali. Enzi ya Mkapa ilishachukuliwa na maharamia wa uchumi lakini mpiganaji lwakatare akairudisha.

Mheshimiwa Pinda ulikuja kiwanda cha Sukari Kagera wala hakutaka kuzungumza na wafanyakazi ili kujua kero zao. aliishia tu ofisini na kuzungushwa kiwandani na Meneja wa kihindi aliyenunua kiwanda toka Serikalini. Inasemekana Sukari inayozalishwa hapo kiwandani wanaiuza nje ya nchi pamoja na uhaba tulio nao, na pika wageni wameajiriwa kibao huku wakiwalipa wageni hao mamilioni kwa kazi ambazo wazawa wanaweza kuzifanya, hiki kilikuwa kiwanda cha Umma kilijengwa na jasho la wananchi!!!!
 
Back
Top Bottom