VIKWAZO
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 1,899
- 580
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameoneshwa kukerwa na jeuri inayooneshwa na uongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara (Nyamongo) unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold uliopoTarime katika kuwasaidia wananchi wanaozunguka mgodi huo.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Mara baada ya kuwasili hapa, Pinda alisema pamoja na kuzungumza na uongozi wa mgodi huo, atazungumza pia na wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo.
Alisema matatizo na migogoro baina ya uongozi wa mgodi huo na wananchi ni moja ya sababu zilizomfanya kuomba kukutana na uongozi wa Mgodi wa Nyamongo wakati wa ziara
yake mkoani hapa.
Hili suala la madini lina changamoto kubwa, ndio maana niliomba mwenyewe niende Nyamongo nizungumze na uongozi na wananchi, Serikali itoe tamko kuhusiana na suala hili maana haiwezekani mwekezaji anakuja na jeuri, mgodi upo katikati ya watu, yeye hataki kushirikiana nao na kila anapoelezwa anasingizia uwekezaji.
Hatuna maana kwamba wawekezaji wawawezeshe wananchi kuwa matajiri, lakini kuna ile misaada ya kijamii ambayo ni lazima wasaidie.
Unakuta mgodi una umeme mwingi unaowatosha na kubakia wa ziada au maji, lakini mwekezaji hataki hata kuwapa kidogo wananchi wa jirani huku ni kutafuta uadui wa bila sababu, alisema Pinda.
Alisema atakapofika katika Mgodi wa Nyamongo atafanya mazungumzo na uongozi wa mgodi na wananchi wa jirani ili kujifunza kiini cha migogoro inayotokea mara kwa mara kati ya wananchi na mgodi ili kupata ufumbuzi.
Alisema Serikali haitavumilia tena kupokea wawekezaji ambao baada ya kuwasili nchini na kuwekeza wanaanza kutoa kauli za kijeuri dhidi ya Serikali kwa kisingizio kwamba wao ni wawekezaji wanaotafuta faida.
Hatuwezi kukubali eti kwa vile wanawajibika kwa Wizara ya Nishati na Madini, basi watu wengine wasiwaguse au kuhoji juu ya suala lolote, ni lazima faida wanayoipata isaidie kupunguza matatizo ya kimsingi kwa wananchi wa jirani, alisema.