Pinda akamatwe na ashitakiwe ni mchochezi.

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
Amelipa nguvu jeshi la polisi kuua raia kila wanapokaidi wakati ni kinyume na haki za binadamu na utawala wa kisheria.
Kwa kauli ya Pinda askari akiomba rushwa ukakaidi upigwe tu! Pia hii inaleta tafsiri hii kwa wananchi kuwa yeyote atakayekufa ilimradi tu kuna uwepo wa jeshi la polisi basi jeshi la polisi linahusika kwa maana wameruhusiwa na Pinda kuua.
Pinda akumbuke kuwa polisi ndio wanaishi na wananchi,kauli hii ya pinda inaleta uhasama kati ya jeshi la polisi na wananchi kuwa kila atakayekufa ilimradi tu kuna jeshi la polisi,watuhumiwa namba moja ni polisi.Hapa askari wamewekewa mazingira magumu sana katika utendaji wa kazi zao,bila kujali nani kaua na kwa sababu gani mtuhumiwa namba moja ni polisi.
Ikumbukwe tu kuwa unapofanya uchunguzi wa matuko kama haya,wanaohojiwa sana ni wananchi,sasa kama wananchi watatumia ushahidi kwa kufanya reference na kauli ya Pinda ya polisi kuruhusiwa kuua, polisi watachomokaje katika hili?
Na kama wananchi kwa pamoja wakakubaliana kutoa ushahidi wa matukio haya kuwa polisi wanahusika na polisi wanafanya kazi kwa maagizo ya wakuu wao,serikali ya ccm na washiriki wake haiwezi kukwepa tuhuma hizi na serikali itakuwa ndio watuhumiwa wakuu.
Nahitimisha kwa kusema hivi,wananchi hawatakuwa na hawana imani na jeshi la polisi.kwa kuwa jeshi hili linatumika kisiasa na kauli(wapigeni tu..tumechoka) ya waziri mkuu imethibitisha kuwa jeshi la polisi linatumika kisiasa.
Yangu maoni.
 
Jaribuni kukumbuka maneno ya Meya wa Jiji
la Dar aliwahi kunena maneno haya hapa.


Didas Masaburi
"Mnafikiri kwa kutumia...........Yenu ninyi
wabunge wa Dar"
 
Jaribuni kukumbuka maneno ya Meya wa Jiji
la Dar aliwahi kunena maneno haya hapa.


Didas Masaburi
"Mnafikiri kwa kutumia...........Yenu ninyi
wabunge wa Dar"

haya ni maneno yako ya kujifariji,kwani hata mgonjwa wa ukimwi huambiwa atapona wakati wengi huwa hawaponi.R.I.P WEWE NA CCM YAKO,YATATIMIA TU HAYA KINACHOSUBIRIWA NI MUDA TU.
 
Ndugu yangu nani atamkamata WMkuu! Mimi ninachojua ni kuwa historia itamuhukumu yeye hata awe wapi. Kwanza itaanzia kwa ndugu zake watakapoanza kumsusa! Na hii si mbali ni hivi karibu. Wakati mwingine tuangalie sana side effects za dose ya huu ugo..............I am sorry to say so but it might be a reality
 
Pinda hakunza leo na kauli za utata, mnakumbuka kauli yake kutaka kila mtuhumiwa wa mauaji ya maalbino wauawe bila kufikishwa mahakamani
 
Pinda hakunza leo na kauli za utata, mnakumbuka kauli yake kutaka kila mtuhumiwa wa mauaji ya maalbino wauawe bila kufikishwa mahakamani

hakuna waziri mkuu aliyewahi kushika wadhifa huu aliye dhaifu na kilaza kama huyu.Hamna kabisa.
 
Hakika hatuna kiongozi na msimamizi mkuu. Huyu bwana si ndiye aliyewahi kulia hadharani?? Tena akasema atayekutwa au kutuhumiwa kuua maalbino naye auawe hapo hapo?
Nasikia huyu bwana ni mwanasheria kitaaluma. Kama kweli ni mwanasheria nguli basi ni doa kubwa kwa taaluma.
 
Back
Top Bottom