Pinda abanwa, kuvunja uongozi Misungwi

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,948
na Sitta Tumma, Magu



WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, juzi alibanwa kwa maswali magumu na kutoa majibu ya sababu zinazoifanya serikali yake kushindwa kuboresha huduma muhimu za kijamii, ikiwemo sekta ya afya, maji na barabara, jambo ambalo linadidimiza ukuaji wa maendeleo ya Watanzania.


Pinda amekumbana na hali hiyo juzi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba mjini Magu, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo. Baadhi ya wananchi walimweleza waziwazi Pinda juu ya kukithiri kwa ubovu wa huduma za kibinadamu na hasa tatizo kubwa la ukosefu wa dawa hospitalini, licha ya kulipia fedha, hivyo wanaona kama serikali imewatelekeza wananchi wake.


"Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa nini serikali mmeshindwa kuiwekea lami barabara hii ya kwenda hospitali ya wilaya ya Magu? Huduma zenyewe za afya ni mbovu, tunakosa hata dawa ya panaldo kwa nini lakini? "Nina hasira sana mheshimiwa usinione hivi. Sasa tunaomba utuambie leo hapa," alisema mkazi mmoja wa wilaya hiyo ya Magu, kisha kushangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamefurika mkutanoni hapo.


Hali hiyo ilimkumba pia Waziri Mkuu Pinda alipokuwa wilayani Ukerewe Jumatano wiki iliyopita baada ya wananchi kumtaka awaeleze sababu ya serikali kugawa umeme kwa upendeleo katika baadhi ya maeneo wilayani humo.


Akijibu maswali ya wananchi wilayani Magu, Pinda alisema serikali haiwezi kuhangaika na uwekaji barabara lami huku wananchi wengi wakikosa huduma ya maji safi ya kunywa. "Punguza jazba mama unisikilize na mimi. Mikakati ya serikali imeelekezwa kutatua kwanza adha kubwa ya maji hapa Magu. Ni afadhali fedha za kuweka lami kipande cha barabara ya kwenda hospitali ya wilaya tukazitumia kununulia dawa."


Kuhusu uhaba wa dawa za binadamu hospitalini, Pinda alisema tatizo hilo ni la kitaifa, na kwamba serikali imeweka mipango mikakati yake katika suala zima la kutatua adha hiyo ya maji, kwani ni asilimia 17 tu ya wakazi wa wilaya ya Magu ndiyo wanapata huduma ya maji safi na salama ya kunywa.
"Wewe mama sikiliza, hospitali utakwenda tu hata kama barabara ni mbovu. Lakini acha kwanza tuboreshe huduma hii ya maji, au mnasemaje wana Magu?" alisema Pinda huku baadhi ya wananchi wakisikika wakisema: "Kauli hiyo ni funika kikombe mwanaharamu apite."

Kuvunja uongozi Misungwi


Katika hatua nyingine, Pinda alilazimika kutangaza kuivunja Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ndani ya siku chache zijazo, kutokana na kile kinachodaiwa kukithiri kwa vitendo vya kifisadi vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo.


Mbali na nia hiyo pia aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), mkoani Mwanza ihakikishe inaanza mara moja kuandaa mashtaka, na kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi katika halmashauri hiyo yenye madiwani 36 wote kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM).


Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo baada ya kubanwa kwa maswali mazito kutoka kwa wananchi kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika mjini Misungwi. Wananchi wa wilaya hiyo wakionekana kuwa na hasira walimtaka Pinda awaeleze hatima ya halmashauri hiyo na tuhuma nzito za ufisadi zinazomkabili mwenyekiti wa halmashauri hiyo pamoja na baadhi ya vigogo wanaotuhumiwa kutafuna mabilioni ya fedha za miradi ya maendeleo.


Wananchi hao ambao walidiriki kumzomea mwenyekiti wa halmashauri hiyo alipoitwa kuwasalimia, walimtaka Waziri Mkuu kuchukua hatua za haraka kunusuru mali za umma zinazodaiwa kutafunwa na watumishi hao.
Tuhuma hizo, ziliwahi kumfanya Waziri Mkuu Pinda kumuagiza aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Exavieri Tilweselekwa, ashushwe cheo na ashtakiwe mahakamani kwa tuhuma hizo nzito.


Akizungumzia tuhuma hizo, Pinda aliyeonekana kukasirishwa na tuhuma hizo, alisema halmashauri hiyo imeelemewa na mchwa mkali unaotafuna fedha za maendeleo, kwani mwaka 2009/2010 ilipata hati yenye mashaka, na mwaka wa fedha 2010/2011 halmashauri hiyo chini ya mwenyekiti wake, Polcarp, ilipata hati chafu, jambo linalothibitisha kuwepo kwa ulaji mkubwa wa fedha unaofanywa na baadhi ya vigogo wa halmashauri hiyo.


Alisema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, pamoja na ripoti ya Tume ya ukaguzi maalumu zimeonyesha wazi kuwepo kwa upotevu mkubwa wa fedha za maendeleo wilayani humo na kwamba madai ya mwenyekiti huyo wa halmashauri kuwa Mbunge wa Misungwi na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga, kuingilia ukaguzi huo, hayana ukweli wowote, kwani vyombo hivyo ni vikubwa na vina heshima yake kubwa ndani na nje ya nchi.


"Ripoti ya CAG na ile ya tume maalumu zinatueleza ukweli wa tatizo hapa Misungwi liko wapi. Mwenyekiti wenu huyu amekuwa akifanya biashara na halmashauri yake kupitia kampuni yake ya ujenzi. Kimaadili, kiuongozi na kisiasa ni jambo lisilokubalika hata kidogo.


"Kiongozi mzuri na makini huwezi kufanya hivyo, maana lazima italeta mgongano tu wa kimaslahi. Ni dhahiri hapa Misungwi hakuna kinachofanyika katika kusimamia maendeleo ya wananchi. Nataka TAKUKURU ifanye kazi yake tena kwa haraka sana. Na wahusika wote wa ufisadi huu wapelekwe mahakamani.


"Swali la kujiuliza hapa. Kwa nini mwenyekiti ufanye biashara na halmashauri? Kama una kampuni yako kwa nini usingetafuta mtu ukamuweka akawa ndiye mwenye kampuni badala ya wewe mwenyewe? Je, ukijipatia tenda ya ujenzi utajisimamiaje na nani atakuwajibisha?" alihoji kwa hasira Pinda, wakati akijibu swali la Victor Thomas aliyesema mwenyekiti huyo hahitajiki tena kuiongoza halmashauri hiyo.


Alisema kulingana na uwepo wa tuhuma hizo dhidi ya mwenyekiti huyo, yeye (Pinda), alimshauri zaidi ya mara mbili juzi kwenye kikao cha ndani na madiwani wote wa halmashauri hiyo ajiuzulu nafasi hiyo, lakini alikataa ushauri wa Waziri Mkuu ambaye ndiye mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa nchini (TAMISEMI).


"Juzi (majuzi), Polcarp alinifuata kuja kuongea na mimi. Lakini nilimshauri ajiuzulu nafasi yake akakataa. Aliniambia Misungwi hakuna tatizo (wananchi wakazomea). Akaniambia kwamba anayesababisha yeye achukiwe na wananchi ni mbunge (Kitwanga)," alisema Pinda mbele ya wananchi.
"Mwnyekiti huyu amekataa ushauri wangu wa kumtaka ajiuzulu. Mimi ndiye bosi wake na ndiye mwenye kauli ya mwisho. Ngoja nirejee Dar es Salaam na ndani ya muda kidogo kisheria nitaivunja halmashauri hii ya Misungwi.


"Maamuzi haya ni mazito maana hapa Misungwi hamtakuwa na madiwani hadi mwaka 2015, na hatua kali za kisheria lazima zichukuliwe kwa wahusika wote," alisema Waziri Mkuu, huku wananchi wengi wakishangilia na kumtaka aivunje halmashauri hiyo papo hapo, kwa madai wamechoshwa na ufisadi.

My take: Hali ya namna hii haiko Misungwi tu bali ndio reflection ya karibu halmashauri zote zinazoongozwa na ccm.

 
[h=3][/h]



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, huenda akalazimika kuivunja Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza baada ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bernard Polycalp, anayetuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za maendeleo kugoma kujiuzulu kwa hiari.

Akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi kwenye uwanja wa Mwanakenenge mjini Misungwi baada ya kufanya ziara ya kukagua shughuli za maendeleo, Pinda alisema atalazimika kufanya maamuzi magumu ikibidi kuivunja halmashauri hiyo kama njia ya kumuondoa Mwenyekiti huyo ambaye amekataa katakata kujiuzulu licha ya chama chake (CCM) kumtaka afanye hivyo kwa hiari.

Pinda alisema mbali na CCM mkoa wa Mwanza kumshauri ajiuzulu, hata yeye (Pinda) amejaribu kumshauri mara mbili lakini bado aligoma kuachia ngazi.


“Juzi Mwenyekiti wenu wa Halmashauri (Polycarp), alikuja pale Ikulu ndogo (jijini Mwanza), tukazungumza naye kuhusu tuhuma zinazomkabili, nikamshauri alijiuzulu lakini akakataa akidai eti anayesababisha achukiwe na wananchi ni Mbunge," alisema.

Aidha, alisema wakiwa katika kikao cha ndani kilichohusisha madiwani wote wa halmashauri hiyo, alimshauri kwa mara nyingine ajiuzulu lakini aligoma.

"Mwenyekiti wenu amekataa ushauri wangu wa kumtaka ajiuzulu. Hajui kuwa mimi ndiye bosi na mwenye kauli ya mwisho. Nadhani hakuna njia nyingine isipokuwa kuivunja halmashauri. Hatma ya jambo hili itajulikana siku chache zijazo baada ya kurejea Dar es Salaam,” alisema Pinda.

Hatua ya Waziri Mkuu kuweka hadharani sakata hilo ilikuja baada ya kumuita Polycalp, aliyekuwapo kwenye mkutano huo wa hadhara awasalimie wananchi baada ya kuwa amesahaulika wakati wa utambulisho uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo.

“Kabla sijazungumza lolote, kuna mtu muhimu sana hapa amesahaulika kutambulishwa. Namuomba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi aje jukwaani japo awasalimie wananchi," alisema Pinda baada ya kukaribishwa kuwahutubia wananchi.

Hata hivyo, wakati Polycalp akisimama kuelekea jukwaani, wananchi walianza kumzomea huku wakipaza sauti kumtaka Waziri Mkuu amuondoe madarakani kwa madai kuwa ni fisadi ametafuna fedha zao za maendeleo.

Licha ya kujitahidi kuwatuliza na kuwasalimia kwa kuchanganya lugha ya Kiswahili na kisha Kisukuma, Polycalp aliendelea kukabiliwa na shinikizo la kelele za wananchi ambao waliendelea kumzomea na kumuita fisadi na mchwa anayetafuna fedha za maendeleo.

“Hatukutaki, ondoka, fisadi wewe umekula fedha zetu,” walisikika wananchi wakipaza sauti, hali iliyomfanya Pinda amtake Polycalp ateremke jukwaani na kurudi kuketi.

Baada ya zomea zomea hiyo ya wananchi ndipo Waziri Mkuu alipoamua kuweka hadharani hali halisi kuhusu sakata hilo la ubadhirifu unaomkabili Polycalp na jinsi alivyokaidi ushauri wa kumtaka ajiuzulu ili kulinda heshima yake na chama chake.

Tofauti na utaratibu alioutumia wa kuwahutubia wananchi moja kwa moja wakati alipokuwa kwenye ziara katika wilaya nyingine, ilimlazimu Pinda atoe fursa kwa wananchi kuzungumza au kuuliza maswali kabla ya kuwahutubia.

Idadi kubwa ya wananchi walinyoosha mikono kutaka kuzungumza lakini Pinda alitoa nafasi kwa watu sita ambao wengi hoja zao zililenga kutaka kujua hatma ya halmashauri yao baada ya kubainika kuwepo kwa ubadhirifu uliosababisha aliyekuwa Mkurungenzi Mtendaji Xavery Tiluselekwa, ashushwe cheo na kufunguliwa mashitaka.

Akitoa ufafanuzi juu ya hoja hizo za wananchi, Pinda huku akionekana mwenye ghadhabu, alisema mwaka 2009/2010 halmashauri hiyo ilipata hati yenye shaka na mwaka wa fedha 2010/2011 chini ya uenyekiti wa Polycalp, ilipata hati chafu, hali iliyoonyesha kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma.

Alisema mbali ya ripoti hiyo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ripoti ya Tume ya ukaguzi maalum, pia ilionyesha kuwepo kwa upotevu mkubwa wa fedha za maendeleo wilayani humo.

"Ripoti ya CAG na ile ya Tume maalum zinatueleza ukweli wa tatizo lilipo hapa Misungwi. Mwenyekiti wenu huyu amekuwa akifanya biashara na halmashauri yake kupitia kampuni yake ya ujenzi. Kimaadili, kiuongozi na kisiasa, ni jambo lisilokubalika hata kidogo,” alisema.

Pinda aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mwanza kuharakisha uchunguzi wake ili watakaobainika kuhusika katika ubadhirifu wa fedha za wananchi wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

CHANZO: NIPASHE

6324088563257897474-8919564871786386371

 

Haya... WIZI MWINGINE na BADO TUNAKITETEA CHAMA CHETU cha NYUNDO na JEMBE...

Hao wezi wote watahamishwa Makao kwenda kuiba kimya kimya kwingineko... Ndani ya CCM hakuna KUFUKUZWA KWA WIZI NA UBADHIRIFU
 
Back
Top Bottom