Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pilipili ina madhara yoyote mwilini?

Discussion in 'JF Doctor' started by Sajenti, Dec 29, 2009.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,677
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mtumiaji mzuri sana wa pilipili. Kila nipatapo chakula basi huwa nahakikisha pilipili haikosekani. Je eti matumizi ya pilipili nyingi yana madhara yoyote mwilini? Wataalamu wa afya na lishe nipeni ushauri.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 26,036
  Likes Received: 3,343
  Trophy Points: 280
  Jihadhari nayo...
  Ikifika maeneo yenye nyama laini muwasho wake huwa hauelezeki
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,610
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Haina madhara yoyote ila wakati wa kujisaidia inakuwa tatizo kiasi
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 26,036
  Likes Received: 3,343
  Trophy Points: 280
  tayari ni madhara hayo
   
 5. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,098
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nliskia (sina uhakika) yawezasababisha vidonda vya tumbo in a long run japo hata mi napenda kula pia.

  Labda wahindi watupe data maana nasikia wanatengeneza mpaka juice ya pilipili.
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,125
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Nahisi ingekuwa na madhara, wahindi na wachina wote wangeshakufa.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Dec 30, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Faida ya Afya ya Kula Pilipili

  Japokuwa Pili pili inaliwa na watu wa jamii mbali mbali duniani, faida na Afya ya kula pilipili wengi hawazijui au hazijulikani na watu wengi.

  Kwenye pilipili kuna kemikali iitwayo Capsaicin, ambayo ndio inayo sababisha muwasho na joto la pilipili.

  Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu:
  Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa mujibu wa timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti iliyochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, mwezi Julai 2006.

  Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.

  Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili

  Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi!

  Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer)

  Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.

  Kula pilipili usaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.


  [​IMG]
   
Loading...