Pigo la tatu kwa Lowassa, bado la Mwisho mwezi Mei

Naomba kujuzwa hawa wajumbe ni nani yupo kambi ya Mkuu wa kaya na ni nani yupo kwa Mkuu wa laizaboni(EL)

1. WASIRA
2.PINDI Chana
3.Tibaijuka
4. Jerry Slaa
5. Kimbisa
6. Nchimbi
7. Lukuvi


Zanzibar:
1. Nahodha
2. Hussein Mwinyi
3. Prof Makame Mbalawa
4. Dr Salm
5. Maua daftari
6. lL. Abuu
7. Samia

Mkuu kwani hii ndio CC ya CCM?....
 
Yeriko mimi nafikiri huu ni mchezo wa kutu-shake Watanzania ili wapate matokeo ya mtu anayependwa tu. Hapa hakuna tofauti kati ya Caldron na EL .....period. Hizi ni fikra Danby wanajamvi.......
 
Bwana Lowassa,

Nikupe pole nyingine baada ya ile ya maonyo yangu kwako nilipochukua wasaa kukueleza vichomi ulivyotegeshewa na ambavyo vimeanza kukuchinjia baharini tena kuleeeee Nungwiiiii na Chamwinooo! Jikumbushe hapa Pigo la Pili kwa Lowassa, bado la Tatu na la Mwisho! - Page 13

Naaam, Umemaliza kifungo chako cha miezi kumi na miwili, Bado unaamini hamkukutana barabarani? Hahahaaa kaamua kula sahani moja na wewe, iwe mchana ama usiku, jua lichomoze ama lizame, kamwe! Hautaiona pepo ya magogoni.

Ndio hilo ni pigo la tatu nililokueleza mwaka jana. Unafahamu kilichowapata wale watoto wa chuo Cha IFM uliowarubuni watangaze kwenye gazeti la nipashe kuwa "IFM wamuunga mkono Lowassa"? Wenye suti nyeusi washafanya yao. Hawana chuo tena.

Unajua kinachowapata wenyeviti wa CCM mikoani Mara na Geita waliosimama na kukunadi hadharani?

Bwana Lowassa wajua kwa sasa ni kharamu kujipambanua kuwa unamuunga mkono Lowasa, huchelewi kukutana na Caldron?

Hayo ni maagizo ya kikao cha mkuu wa Caldron na vijana kuhakikisha wanakuzima kila kona, muulize Madafa atakwambia japo yupo upande wa pili, pia Apson anaujua mchezo huu ila hawezi kukwambia kwakuwa anaheshimu makubaliano ya Ada Estate (Gentleman Agreement) kati yako na mwenyekiti kipindi kileee.

Bwana Lowassa, nakupa ukweli kuwa mkataba wenu ushakufa, kumbuka kikao cha dodoma mwezi juzi jamaa aligoma kuonana na wewe hata ulipojaribu kila njia angalau kupiga nae picha tu lakini alikukwepa, kumbuka alichojibiwa yule uliyemtuma akuombee miadi ya kukutana na mwenyekiti walau msalimia, kosa kubwa ulilolifanya nikuwa ulishajipanga na wapiga picha za magazeti ili kujijenga.

Vita vyako si vya Damu na Nyama, Bali ni vya pepo wabaya wa Magogoni wanaokula na kusaza mikononi mwa mwenyekiti wako!

Walijua PIGO la MWISHO lililo mbele yako??

Haya tutaftane.....!

Yeriko it will help to do or campaining for your party CDM,mambo ya CCM waachie wana CCM na wao ndo wenye maamuzi ya nani anafaa kuwa rais au la,wewe kapambane na wakina slaa,Mbowe na wengineo,
zaidi kabisa kwenye siasa za tanzania with ua age bado sana jaribu kujifunza ndipo uje hapa
ushauri wangu ni ukakojoe chap then ukalale
achana kabisa na Rais wetu Lowasa
 
Lowassa hapiti hata atembee uchi mchana kweupe.

Lowasa amechelewa kusawazisha goli hadi jamaa wamepaki bus. Hayo ya rohoni aliyonayo akitakiwa ayaseme wakati huo sasa Hivi ni too late. alitumia technic sana kujitangaza na akafaulu kuwashikia akili watanzania zaidi ya asilimia sitini alichokosea aliwahi. sasa Hivi jamaa wanapita kufuta alama za miguu. Wanakaba ni hatari kila akikanyaga wanafuta kwa kuthibitisha Hilo walihakikisha hawampI nafasi kwenye Mazishi ya Capt Komba hata ya kuongea na mjumbe wa nyumba kumi
 
Na Capt Komba ambaye aliapa kukuimbia sifa kemkem ndo hivo kashadedi, wote wanaokusapoti wanaundiwa zengwe hadi makanisani kina Flora Mbasha wamezimwa
 
Lowasa amechelewa kusawazisha goli hadi jamaa wamepaki bus. Hayo ya rohoni aliyonayo akitakiwa ayaseme wakati huo sasa Hivi ni too late. alitumia technic sana kujitangaza na akafaulu kuwashikia akili watanzania zaidi ya asilimia sitini alichokosea aliwahi. sasa Hivi jamaa wanapita kufuta alama za miguu. Wanakaba ni hatari kila akikanyaga wanafuta kwa kuthibitisha Hilo walihakikisha hawampI nafasi kwenye Mazishi ya Capt Komba hata ya kuongea na mjumbe wa nyumba kumi

Asante sana mkuu kumbe unalifahamu hili
 
Tunataka Kiongozi Muadilifu Mchapakazi, Siyo Kiongozi Fisadi Mchapakazi.
 
Historia imeonyesha na wakati umedhihirisha kuwa Rais aliye madarakani hawezi kumchagua kwa veto atakayechukua mikoba kwa hata si yeye aliyejichagua kuwa Rais. Hana mamlaka kikatiba au kichama. Bado mapendekezo ya wanachama ndio demokrasia halisi. Mfano Mkapa alipendekeza Sumaye ikaisha vibaya, Mwinyi na Mkapa etc. Hivyo hii kwa sasa ni tararira ila kanuni ziko wazi. Kikwete wananchi walimtaka vibaya sana na ndio kilichopelekea Sumaye kukosa. Kwa sasa kama hawa viongozi wetu watakumbuka historia kujirudia ndio kanuni, basi Lowassa anahitajika badly na wananchi pamoja na wanachama. Wanaomgwaya ni tu wabaya wake na wallah billah watakiona na mtema kuni. Waache waweweseke.
 
Mnafikiri lowasa ni kama dk slaa huyo ni sayar nyingine,watasema,watanuna,watatukana,kila hoja italetwa lakin mwisho amiri jeshi mkuu ni EDWARD LOWASA very soon stay tuned

uko sahihi mkuu cha msingi nikusubiri tuone kama maneno yako yatatimia kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom