Lileteni faili la Lowassa tulichambue haraka

ngumarwa

Member
May 15, 2015
12
13
Na Daniel Mbega

MASHAIRI ya sasa ya siasa hayana mizani wala vina, tena hayana urari! Hata ngonjera na tenzi vyote huwa na beti, mizani na vina.
Tanzania imegubikwa na tufani ya Ukawa, hususan Edward Lowassa. Wimbi kubwa la wanaohemka ni la vijana, wengi wao wakiwa waliozaliwa katika miaka ya 1980, ambao kwa hakika ndio viongozi wa sasa wanaotakiwa kuleta mabadiliko. Vijana siyo taifa la kesho tena, ni la leo.

Naam. Wale wazee na vijana hirimu yangu wanaogelea katika wimbi la mageuzi hayo ambapo wapiga kasia ni vijana. Wengi wanafurahia upepo unakoelekea na wanaomba usije ukabadilisha mwelekeo – pepo za Kusi na Kaskazi huwa hazitabiriki wakati mwingine na zinaweza kuleta madhara.

Wanasiasa wakongwe wanaona huu ndio wakati muafaka wa kupata neema nyingine. Ndiyo. Wapo waliokuwa wabunge kwa miaka mingi, wapo waliokuwa wanaongoza vyama vya siasa kwa miaka mingi. Wengi kati ya hawa wamechokwa na wananchi waliokuwa wanawaongoza. Wametemwa na vyama vyao na sasa wameona kimbilio pekee ni kudandia mashua inayopelekeshwa na upepo wa mabadiliko – ya vijana!

Japokuwa tayari mashua imempata nahodha, ambaye ni Lowassa, lakini kwa kiasi kikubwa vijana ndio wanaoisukuma, tena kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba kama litatokea wimbi kubwa linaweza kukipaisha chombo na wote wakazama. Ni mtazamo wangu tu miye ambaye niko ng'ambo naangalia.
Lowassa ametoka katika Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya chama hicho kumbwaga akiwa ndiyo kwanza anataka kuianza safari yake ya matumaini. Amekaa akatafakari wee akaona hapana, safari ya matumaini inaweza kuendelea, hata kwa kutumia ngalawa.

Akapokelewa kwa huba na mahaba huko Chadema na hata Ukawa kiasi kwamba ndani ya siku mbili tu, tayari akawa amekabidhiwa mikoba ya kuwania urais. Mikoba ambayo kabla ya kuelekea huko wapinzani hao walikuwa wameafikiana kwamba aibebe yule Paroko mstaafu, Dakta Wilbrod Peter Slaa.
Na mara tu Lowassa alipotua Ukawa, Dk. Slaa akaingia mitini, kukaa kidogo, Profesa Ibrahim Lipumba naye akatimua. Wale waliokuwa nguzo ya upinzani wameondoka kabla chombo hakijang'oa nanga.

Yanaendelea kusemwa mengi kutokana na kuondoka kwa wanasiasa hao wawili ndani ya Ukawa. Wanatuhumiwa kwamba wamelambishwa sukari guru, ndiyo maana wameondoka ili wakidhoofishe chombo hicho na kukwamisha safari ya matumaini ya Lowassa pamoja na ndoto za Chadema za kukaa pale Magogoni kwa mara ya kwanza!

Kuvuja kwa pakacha, nafuu kwa mchukuzi, maana mzigo utakuwa mwepesi. Ukawa inabidi wafurahie kuondoka kwao. Unadhani wakichukua nchi si watakuwa na nafasi mbili za Paroko na Profesa ambazo lazima wangepewa hao kama wangekuwepo?

Leo hii wanaozisubiri nafasi hizo ni wengi mno – Ukawa kuna orodha ndefu, halafu Lowassa kama taasisi ameondoka CCM pamoja na ‘watu wake' ambao alikuwa nao kitambo na wengi walikwishaahidiwa nyadhifa nyeti kama wakifanikisha safari ya matumaini. Uongozi mzuri bwana, asikwambie mtu, na hasa unapopigiwa mizinga 21!

Lakini tayari Profesa Lipumba amekwishasema kwamba ameondoka Ukawa na CUF – alikoachia nyadhifa zake zote – kwa sababu dhamira yake inamsuta. Yawezekana anayajua mengi yaliyo nyuma ya pazia kuhusu mchakato wa kuingia kwa Lowassa.

Dk. Slaa kwa upande wake ndiye amemwaga sumu Septemba Mosi, 2015 wakati alipoeleza bayana kwamba mchakato uliyumbishwa na viongozi wenzake ndani ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, kiasi kwamba hata barua yake ya kujiuzulu ilichanwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari.

Yapo mengi aliyoyasema pia kuhusu ujio wa waziri mkuu mstaafu mwingine Frederick Sumaye ndani ya Chadema, lakini kuna mengine amesema ni silaha zake za maangamizi, ambazo ninaamini atakuwa nazo kwenye faili. Tayari Sumaye ndiye ameteuliwa kuwa Meneja wa Kampeni wa Lowassa, kuhakikisha ushindi unapatikana.

Alipotua Ukawa, mara moja Lowassa akatamba kwamba yeye tayari ni rais, anasubiri kuapishwa kwa sababu siku ya Oktoba 25, 2015 atanyakua ushindi asubuhi tu! Nadhani itabidi tutoke saa tisa alfajiri kama tulivyokuwa tunafanya tulipokuwa tunajiandikisha kwenye BVR ili tufanikishe safari ya matumaini!
Hakuishia hapo, akasema anazijua fitna zote za CCM na atahakikisha anakomaa mpaka kinaeleweka. Wewe vihunzi vyote alivyoruka mpaka sasa anajaza nyomi kila anakopita na kumhakikishia safari ya matumaini unadhani usingizi unaweza kuja?

Lakini Lowassa lazima azijue fitna za CCM kwa sababu yeye alikuwa miongoni mwa ‘wajumbe wa kamati ya usajili' na pia kocha mchezaji. Anajua vyema harakati zake za safari ya matumaini zilizoanzia mwaka 1995. Tena anajua vyema namna walivyouanzisha ‘Mtandao' ndani ya CCM mwaka 2005 ili kufanikisha ushindi wa Jakaya Kikwete.

Lowassa ni dhahiri anajua mchezo uliofanyika mwaka 2005 wa kumkata mapemaaa Mzee Cigwiyemisi John Samuel Malecela mpaka akashindwa kuingia kwenye tano bora. Sijui kwanini yeye safari hii amelia na kuomboleza baada ya kukatwa mapema. Hakika kidonda kiko kwako, kwa mwenzako hakiumi!

Naam. Lowassa pia atakuwa anakumbuka kilichotokea mpaka mwanadiplomasia ninayemheshimu sana, Dk. Salim Ahmed Salim, akafanyiwa fitna kwa picha yake kutengenezwa na kuzushiwa kwamba ati aliwahi kuwa mwanachama wa Hizbu, kile chama kilichokuwa na Waarabu wengi ambacho kilikuwa kinapinga harakati za ukombozi Visiwani zilizokuwa zinafanywa na vyama vya African Association na Shirazi Association ambavyo baadaye vikaungana na kuunda Afro-Shiraz Party.

Zile zilikuwa ni fitna mbaya sana na wahusika walioucheza mchezo huo nadhani nafsi zao zinawasuta. Wengi dhambi ile inawatafuna kwa sasa.
Duru za siasa zinaeleza kwamba ati kuna ‘Mafaili ya Lowassa na Sumaye' yanayoandaliwa na baadhi ya watu – ndani na nje ya CCM wanaopinga hatua yake ya kugombea urais kwa sababu siyo msafi kama anavyojinasibu – ambayo pengine yanasubiri wakati muafaka tu yatolewe hadharani wakati mapambano ya hoja za majukwaani yatakapoanza. Sijui kama kama kauli ya Dk. Slaa ni mwanzo wa kuyafumua faili hayo ama la.

Mimi nalisubiri sana mafaili hayo ili kujua kuna nini ndani. Sijui kama yatakuwa yanazungumzia kuhusu kuanzishwa kwa ‘mtandao' ambao ndio umekivuruga chama ingawa Lowassa mwenyewe anayedaiwa kuwa mhusika naye analia kwamba chama kimeharibika?

Natamani nione mafaili hayo ili kujua hasa chanzo cha ‘chuki' ya Lowassa kwa Malecela. Sijui kama ilianza wakati ule alipokuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais akishughulikia Haki na Mambo ya Bunge miaka ile ya 1990 wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, au ilianza kipindi kile cha mwaka 1997 wakati vijana wa CCM walipotaka kumwangusha Malecela kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara na kumpa Frederick Sumaye kabla Mwalimu Julius Nyerere hajaenda Dodoma kuzima jaribio hilo!

Bila shaka mafaili hayo yatakuwa na kashfa za uuzaji wa viwanja vya Kariakoo jijini Dar es Salaam akimtumia mfanyabiashara Baghdad wakati yeye akiwa Waziri wa Ardhi wakati wa Mwinyi, au pengine wanataka kuanika ukweli wa zilikopelekwa fedha za msaada zinazodaiwa kutumika kwenye ujenzi wa nyumba ya Lowassa ambayo kaupangisha Ubalozi wa Afrika Kusini kule Masaki.

Pengine faili la Lowassa litakuwa linaeleza bayana namna alivyohusika kwenye mchakato wa mkataba wa Richmond, tofauti na utetezi wake alioutoa wakati akienda Ukawa.

Naamini nyaraka za Baraza la Mawaziri hasa Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoketi Februari 2, 2006 (takriban mwezi mmoja na nusu tangu Lowassa ateuliwe kuwa Waziri Mkuu), zitakuwemo na zitaeleza ni kwanini baada ya kikao cha Februari 2, 2006, saa 10 jioni ya siku hiyo hiyo, Ibrahim Msabaha (aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo), aliufuta mchakato ulioanzia kwenye Serikali ya Mkapa na kubarikiwa na Baraza la Mawaziri na hatimaye kampuni ya Richmond ikapewa zabuni ya kufua umeme wa dharura.

Au pengine linaeleza uamuzi wake, akiwa Waziri wa Maji na Mifugo, wa kuruhusu mifugo itawanyike nchi nzima bila maandalizi yoyote wala elimu kwa wakulima na wafugaji, hatua ambayo imesababisha mauaji makubwa kutokana na migogoro baina ya jamii hizo mbili.

Kama sivyo, basi huenda faili hilo litakuwa limejaa kashfa za rushwa, kwamba alikuwa anatumia jumuiya mbalimbali za CCM ili kumuunga mkono kwenye safari yake ya matumaini ya kwenda pale Magogoni.

Nalisubiri kwa hamu faili hili kama kweli litatoka. Pengine basi litakuwa na orodha ya watu – wakiwemo wanahabari – ambao wanadaiwa wanalipwa ili kufanya kazi maalum ya kumpamba na kumtakasa kwa nia ya kumsindikiza hadi Magogoni.

Au pengine faili hilo, mbali ya kuwa na orodha ya utajiri wa Lowassa na familia yake, na jinsi ulivyopatikana, pia linaweza kuwa na orodha ya marafiki zake ambao wanamsaidia ama kumchangia fedha – zikiwemo zile ambazo amekuwa akizitoa kwenye harambee mbalimbali au namna marafiki zake hao walivyozipata fedha hizo ingawa sina imani kama hilo haliwezi kuiathiri Benki ya CRDB!

Kwa upande wa Sumaye, nasubiri kuona lina nini ndani ili kulinganisha na ‘madongo' aliyoyaporomosha kwa serikali ya sasa.
Inawezekana faili hilo litaeleza ushiriki wake katika kudidimiza kilimo kwa maana amekuwepo kwenye Wizara ya Kilimo na Ushirika tangu mwaka 1985 hadi 1995 – kwanza akiwa naibu waziri na baadaye waziri kamili.

Pengine litaeleza namna mashamba ya umma (NAFCO, DAFCO na NARCO) yalivyobinafsishwa na hata kuuzwa baada ya wakubwa kuyatafuna watakavyo.

Yumkini faili la Sumaye litaeleza yaliyotokea akiwa waziri mkuu kwa miaka 10, mwezi mmoja na siku tatu. Huenda tukajua mikataba yote mibovu ya nishati na madini ilivyosainiwa ama wakubwa walivyojitwalia mashirika ya umma.

Naamini yapo mengi, na Watanzania wanatamani kuyaona ama kuyasiki sasa ili waweze kuyajadili, maana mambo yaliyofanyika wakati huo ndiyo yameongeza ugumu wa maisha kwao.

Kama kweli yapo, mafaili hayo ni muhimu kuyaona na ninawashauri wenye nayo wayalete haraka tuyachambue na kuyajadili.

Mimi nayasubiri!
 
Lowassa hatuna haja ya kusoma faili lake. Hivi sasa machungu ya mgao wa umeme tunayoyapata tayari ni file tosha la kumuhukumu huyu mwizi.
 
Failihata likiletwa kwa sasa halitasaidia kweli lakini usimuhukumu kwa tatizo la umeme linalojitokeza sasa bali ihukumu CCM kwa ujumla wake yote haya ni matokeo ya uongozi wa CCM. Lowassa katoka kwenye uwaziri mwaka 2008 how comes useme tatizo la umeme sasa unamuhusu yeye? Na hata kama alihusika wakati huo CCM ilikuwa wapi kushindwa kuzibiti uharifu huo? Unayatofautisha vipi mabaya ya Lowassa na CCM? Be analytical and logical
 
Lowassa hafai sema wenzetu wapiga madili wa CDM ndo ivyo tena hawasikii la mwadhin wala mpiga swala.
 
Jamani tuwe wa kweli hivi ukawa na cc ni wepi wapiga dili?

Najaribu kuwaza kwa sauti,kama Mwenyezi Mungu angeshuka leo akasema WANACCM wote anayejiona yu hana dhambi basi ampopoe Mawe Lowassa nina uhakika wengi watakufa au watakimbia kwa kihoro.

Ni ajabu sana tuliyonayo binadamu tunapenda kuhukumu bila kuwa na mipaka.Tumeshasikia maovu yake yote ingekuwa vyema kwa sasa wakanyamaza.

Wangekuwa na akili kweli wangekaa chini wakajitathmini kwa nini iwe hivi pamoja na tuhuma zote hizi bado watanzania wameng'ang'ania pale pale.

Ni wakati wa kuacha sasa,tumwachie aliyemuumba amuhukumu kwa maovu yake.
 
Na nyie leteni mafaili ya ESCROW kupitia stanbic, mafaili ya pembe za ndovu na ya wauza unga tuone kama mgombea wenu hayumo
 
EPA, RICHMOND, ESCROW, IPTL, SONGAS, ATMAS, AGRECO, NET GROUP SOLUTION, DHAHABU, ALMASI, URANIUM, VITALU VYA UWINDAJI, VIPUSA, SEMBE, ARDHI, VIWANDA, ATC, TRL, NBC, BANDARI, MEREMETA, DEEP GREEN, KAGODA ... R.I.P KOMBE, R.I.P SOKOINE, RIP JK NYERERE ... Malofa tumeamua kuwa CCM lazima Ing'olewe... Hata mkimuita Lowassa majina yote mabaya ya Duniani sisi tumeamua kuwa atakuwa Rais wa awamu ya 5 ya JMT ...
 
Failihata likiletwa kwa sasa halitasaidia kweli lakini usimuhukumu kwa tatizo la umeme linalojitokeza sasa bali ihukumu CCM kwa ujumla wake yote haya ni matokeo ya uongozi wa CCM. Lowassa katoka kwenye uwaziri mwaka 2008 how comes useme tatizo la umeme sasa unamuhusu yeye? Na hata kama alihusika wakati huo CCM ilikuwa wapi kushindwa kuzibiti uharifu huo? Unayatofautisha vipi mabaya ya Lowassa na CCM? Be analytical and logical

well said mkuu,wengi hapa jamvin ni watu wa mihemko tu,
 
Na Daniel Mbega

Lakini tayari Profesa Lipumba amekwishasema kwamba ameondoka Ukawa na CUF – alikoachia nyadhifa zake zote – kwa sababu dhamira yake inamsuta. Yawezekana anayajua mengi yaliyo nyuma ya pazia kuhusu mchakato wa kuingia kwa Lowassa.

Dk. Slaa kwa upande wake ndiye amemwaga sumu Septemba Mosi, 2015 wakati alipoeleza bayana kwamba mchakato uliyumbishwa na viongozi wenzake ndani ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, kiasi kwamba hata barua yake ya kujiuzulu ilichanwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari.

Duru za siasa zinaeleza kwamba ati kuna ‘Mafaili ya Lowassa na Sumaye' yanayoandaliwa na baadhi ya watu – ndani na nje ya CCM wanaopinga hatua yake ya kugombea urais kwa sababu siyo msafi kama anavyojinasibu – ambayo pengine yanasubiri wakati muafaka tu yatolewe hadharani wakati mapambano ya hoja za majukwaani yatakapoanza. Sijui kama kama kauli ya Dk. Slaa ni mwanzo wa kuyafumua faili hayo ama la.

Mimi nalisubiri sana mafaili hayo ili kujua kuna nini ndani. Sijui kama yatakuwa yanazungumzia kuhusu kuanzishwa kwa ‘mtandao' ambao ndio umekivuruga chama ingawa Lowassa mwenyewe anayedaiwa kuwa mhusika naye analia kwamba chama kimeharibika?

Natamani nione mafaili hayo ili kujua hasa chanzo cha ‘chuki' ya Lowassa kwa Malecela. Sijui kama ilianza wakati ule alipokuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais akishughulikia Haki na Mambo ya Bunge miaka ile ya 1990 wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, au ilianza kipindi kile cha mwaka 1997 wakati vijana wa CCM walipotaka kumwangusha Malecela kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara na kumpa Frederick Sumaye kabla Mwalimu Julius Nyerere hajaenda Dodoma kuzima jaribio hilo!

Bila shaka mafaili hayo yatakuwa na kashfa za uuzaji wa viwanja vya Kariakoo jijini Dar es Salaam akimtumia mfanyabiashara Baghdad wakati yeye akiwa Waziri wa Ardhi wakati wa Mwinyi, au pengine wanataka kuanika ukweli wa zilikopelekwa fedha za msaada zinazodaiwa kutumika kwenye ujenzi wa nyumba ya Lowassa ambayo kaupangisha Ubalozi wa Afrika Kusini kule Masaki.

Pengine faili la Lowassa litakuwa linaeleza bayana namna alivyohusika kwenye mchakato wa mkataba wa Richmond, tofauti na utetezi wake alioutoa wakati akienda Ukawa.

Naamini nyaraka za Baraza la Mawaziri hasa Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoketi Februari 2, 2006 (takriban mwezi mmoja na nusu tangu Lowassa ateuliwe kuwa Waziri Mkuu), zitakuwemo na zitaeleza ni kwanini baada ya kikao cha Februari 2, 2006, saa 10 jioni ya siku hiyo hiyo, Ibrahim Msabaha (aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo), aliufuta mchakato ulioanzia kwenye Serikali ya Mkapa na kubarikiwa na Baraza la Mawaziri na hatimaye kampuni ya Richmond ikapewa zabuni ya kufua umeme wa dharura.

Au pengine linaeleza uamuzi wake, akiwa Waziri wa Maji na Mifugo, wa kuruhusu mifugo itawanyike nchi nzima bila maandalizi yoyote wala elimu kwa wakulima na wafugaji, hatua ambayo imesababisha mauaji makubwa kutokana na migogoro baina ya jamii hizo mbili.

Kama sivyo, basi huenda faili hilo litakuwa limejaa kashfa za rushwa, kwamba alikuwa anatumia jumuiya mbalimbali za CCM ili kumuunga mkono kwenye safari yake ya matumaini ya kwenda pale Magogoni.

Nalisubiri kwa hamu faili hili kama kweli litatoka. Pengine basi litakuwa na orodha ya watu – wakiwemo wanahabari – ambao wanadaiwa wanalipwa ili kufanya kazi maalum ya kumpamba na kumtakasa kwa nia ya kumsindikiza hadi Magogoni.

Au pengine faili hilo, mbali ya kuwa na orodha ya utajiri wa Lowassa na familia yake, na jinsi ulivyopatikana, pia linaweza kuwa na orodha ya marafiki zake ambao wanamsaidia ama kumchangia fedha – zikiwemo zile ambazo amekuwa akizitoa kwenye harambee mbalimbali au namna marafiki zake hao walivyozipata fedha hizo ingawa sina imani kama hilo haliwezi kuiathiri Benki ya CRDB!

Mimi nayasubiri!

Amen. Uchafu wa LOWASSA inabidi uwekwe wazi.
 
Lowassa hatuna haja ya kusoma faili lake. Hivi sasa machungu ya mgao wa umeme tunayoyapata tayari ni file tosha la kumuhukumu huyu mwizi.

una mawazo mgando(hata ulivyo safishwa ubongo bado tu?)(brain wash) Waziri mwenye dhamana anawambia wananchi mgao wa umeme mwisho tarehe 14-9-2015 leo ni tarehe nagapi file ndiyo umeme au uongozi wa Tanesco na wizara ya nishati
 
Ma-file yapo mengi sana tunayoitaji kuyaona,hata wale walio mkunja TWIGA wakamuingiza kwenye ndege,meno ya TEMBO,escrow,meli mbovu,mabehewa mabovu nk.na bila kumchagua EL kwenda ikulu,na akifka kazi yakwanza nikuvunja makomeo na kumwaga pombe yote.Ikulu ni maalipatakatifu hatuwezi kupeleka pombe Ikulu. Lowassa mwendo mdundo ikulu ileeeeeeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom