Hii inasikitisha mno , inaumiza sana!
Nashindwa kuvumilia kububujikwa na machozi. Hizi picha zimezidisha simanzi maana zinaonyesha mengi sana:
1.Ajali za barabarani zitatumaliza jamani.
2. Umaskini uliokithiri nchini mwetu - yaani tumeshindwa hata kuwasitiri hawa marehemu japo hata kuwafunika vizuri! Hapo wamesitiriwa na vitambaa vya mabango yao wenyewe tu. Halafu wamewekwa chini - thamani ya binadamu hapo hakuna kabisa.Kama mzazi nimeumia sana!
MUNGU WA REHEMA NA NEEMA ZISIZO NA MWISHO, UWAJAALIE PUMZIKO LA MILELE.
DUNIANI TUNAPITA TU......
Mliotangulia, pumzikeni kwa amani, ole wetu siye tuliobakia!