Picha za Pharaoh (Ramesses II) Enzi Ya Musa

mkuu siyo kilakitu lazima uingize dini. Kwanza wakati yote hapo juu yana tokea uislamu haukuwepo. Pili ni kwamba siyo wote humu waislamu sasa ukitumia uislamu kueleza kila jambo humu jf hauta eleweka. Kuna jukwaa la dini mkuu.


soma tena pale juuu inaelekea huna dini mana yale nilioweka sio ya uislam pekee yake auu ndiiio hizo chuki za uislam zimeshawafunika......?umarekani huo umewajaa cnn bbc ...lol




labda niwakumbushe historia ya jambo hili la huyo farao inapatikana tu kwenye vitabu vya dini sawa wakina baba na mama kwa huoja kwa haliafikiani na dini mnachemsha.
 
Mimi naona aya zile za kurani takatifu zilitumiwa vibaya ni kama machafuko matupu.
1) Kwanza aya hazina uhusiano wowote na kichwa kinachojadiliwa. Kama mwandishi alitaka kusema kitu aseme kama hajui jinsi ya kusema aulize swali au anyamaze.
2) Kutumia maneno ya maandiko matakatifu kwa njia hii bila maana ni kuchafusha heshima ya andiko hili.
3) kujaza ukurasa kwa herufi kubwa vile ni usumbufu mtupu na machafuko ya ukurasa huu.
 
soma tena pale juuu inaelekea huna dini mana yale nilioweka sio ya uislam pekee yake auu ndiiio hizo chuki za uislam zimeshawafunika......?umarekani huo umewajaa cnn bbc ...lol




labda niwakumbushe historia ya jambo hili la huyo farao inapatikana tu kwenye vitabu vya dini sawa wakina baba na mama kwa huoja kwa haliafikiani na dini mnachemsha.

Mbona una kimbilia kusema chuki zidi ya waislamu? kitu kidogo tu kikisemwa mtu kashaona Uislamu unachukiwa. Kwani nilisema nina tatizo na uislamu? Lol tusha zoea mtu ana kimbilia kusema udini.
 
Wazee turudi kwenye mada, nimeileta hii na kuitolea maelezo, maelezo ambayo kwa njia moja ama nyingine kuna mdau akayatolea maelezo ambayo yanakinzana kwa njia moja ama nyingine na yale niliyo yaeleza mimi kabla.

Sasa basi kama kuna mtu mwenye kuelewa zaidi kuhusiana na hawa wafalme wa kimisri, atumwagie Ilmu hapa ili tufaidike. Si vibaya mtu ku-quote baadhi ya aya au mistari toka kwenye vitabu vya dini...!Ilaa tuzingatie aya na mistari hiyo haita leta mtafaruku katika bandiko hili.

Swali:
Je Pharaoh huyu (Ramesses II) Ndiye yule wa enzi ya Musa!?
Pili Mfalme huyu ndiye aliyekumbwa na lile balaa la kuzama baharini?


Je tunaweza kujifunza chochote kutoka kwa hawa Mafirauni (Pharaoh).

Nawasilisha.
 
Hao mafarao walikuwa waafrika. Hiyo picha hapo ni ya mzungu. Hebu weka picha inayofanana na Sphinx yule waliyemkata pua makusudi ili asionekana ni Mwafrika!
 
Swali:
Je Pharaoh huyu (Ramesses II) Ndiye yule wa enzi ya Musa!?
Pili Mfalme huyu ndiye aliyekumbwa na lile balaa la kuzama baharini?

Je tunaweza kujifunza chochote kutoka kwa hawa Mafirauni (Pharaoh).
.

Kuhusu swali la kwanza linganisha [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Pharaoh_of_the_Exodus"]makala hii ya wikipedia[/ame]: kuna nadharia mbalimbali naona turidhike si sisi hapa tutakaopata jibu kamili la swali hili. Kuna uwezekano ya kwamba Ramses II alikuwa farao wa Musa lakini hakuna uhakika kuna sababu nzuri dhidi yake na kwa ajili ya majina mengine.

Kuhusu swali la pili uwezekano wa Ramses II kuwa farao aliyekufa baharini pamoja jeshi lililomfuata Musa ni mdogo mno. Ramses alipokufa alikuwa mgonjwa hakutembea tena au kwa matata makubwa kutokana na umri mkubwa wa miaka 90 na hali baya ya mifupa yake. Hakuwa mtu tena wa kuongoza jeshi lake katika safari hatari jangwani. Pia taarifa ya Biblia (Kutoka 14) haimtaji farao mwenyewe kati ya wanajeshi waliozama. Kuna Zaburi 135:15 pekee inayoweza kudokeza hivi lakini kama zaburi zote ni wimbo si taarifa ya kihistoria tena iliandikwa muda mrefu sana baada ya matokeo haidhaniwi kutunza habari za kihistoria.

Kuhusu swali la tatu: bila shaka unaweza kujifunza kitu fulani kutoka kila habari pia habari za wafalme wa Misri ya kale lakini unataka kujua nini? Yaani kila jibu hutegemea swali.
 
Last edited:
Hao mafarao walikuwa waafrika. Hiyo picha hapo ni ya mzungu. Hebu weka picha inayofanana na Sphinx yule waliyemkata pua makusudi ili asionekana ni Mwafrika!

Mzee wangu si Mafarao wote waliokuwa Waafrika. Watu wa Kazkazini karibu na Mediteranea walifanana na watu wengine wa Mashariki ya kati (si wazungu!) watu wa Misri Kusini walikuwa (hadi leo ni vile) Waafrika weusi kimaumbile.
Katika historia ndefu mchanganyiko ulitokea hivyo utaona kila aina ya watu kati ya mafarao; kwa muda fulani hata watu waliofanana zaidi na wazungu baada ya kuvamiwa kwa Misri na majirani kutoka kaskazini kuwa wafalme wa nasaba ya 22 (angalia wikipedia http://en.wikipedia.org/wiki/Twenty-second_dynasty_of_Egypt) walikuwa watu kutoka Libia.

Ramses II alikuwa na nywele nyekundu si dalili la kawaida kwa mtu wa Nubia au kusini ya Misri.

Tena Sphinx haikukatwa pua kwa makusudi ya kuficha kitu bali alkuwa Mwislamu Mmisri mkali aliyeitwa Mohammed Saim el-Dar aliyechukia sanamu kubwa yenye uso aliyoona ni dhidi ya sheria ya Kiislamu alijaribu kuharibu uso lakini aliuawa na watu waliokaa karibu ("In 1378 AD, upon finding the Egyptian peasants making offerings to the Sphinx in the hope of increasing their harvest, Sa'im al-Dahr was so outraged that he destroyed the nose, and was hanged for vandalism." - Great Sphinx of Giza - Wikipedia, the free encyclopedia).
 
Last edited:
Nimerudi kusoma mwili wa Farao, hata sijui ni kwanini nimemkumbuka leo;

Mada za Mapharaoh, history of black Egypt zimekuwa mada kuu kwa sasa ndani ya JF, una haki ya kujikumbusha thread za zamani zinazozungumzia hayo mambo
 
Back
Top Bottom