Picha za Mkapa na Vincent wakiwa kwenye msiba wa baba-Vincent yaani Kiboko Nyerere

Sitashangaa kusikia kesho BWM anasema wameni-edit hiyo picha kwa sababu hapa mahala mi sikuwepo siku hiyo
 
ni kawaida kwa wa magamba kukanusha waliyoyaamini na kuyasemea,mbona hata nyara za taifa zilikanusha kauli zake!
 
Sidhani kama unajua hata kinachojadiliwa.
Mkuu usipoteze muda wako huyo yupo kundi la wafu, hebu angalia hapo chini sio maiti zote kwamba zipo kaburini!!

kipanya_27_-_03_-_2012_20120327_1083838111.jpg
 
Acheni kutetea uongo. Yani rais mstaafu ataendaje kumzika Kiboko halafu aje amkane mwanae hadharani? Hizi ndio mbinu chafu alizotumia enzi za utawala wake wa mabavu lkn anashindwa kujua kuwa sasa Tanzanians are aware. Na huu ndio tunaita umbumbumbu wa kisiasa.
 
kwa uzibitisho huu kweli nimeamin mzee mkapa ni mnafik sana na c wakuaminika tena mbele yatamii, haiwezekan m2 ameuzuria msiba wa baba yako nakuonyesha uzun na unyenyekevu mbele ya familia ya marehemu, leo hii kwa sababu ya campain uikane ile familia kua huijui na wala vicent c ndugu wa mwl nyerere, imeniuzunisha sana kuona kiongoz wa juu kama yeye kutoa kauli za uongo mbele ya wa tz, ingekua ni nchi za wa2 wanaojua kuwajbika basi uyu mzee angewajibika mbele ya jamii kwakujivua kuwa rais mstaafu nakua raia wakawaida tu
 
That is why I love JF. Mkapa ameumbuka because of his selective amnesia!

Hivi watanzania tutaendelea kumtunza kwa kodi zetu huyo MUONGO mpaka lini. Huu naon ni ufisadi kodi zetu kugharamikia mtu kusema uongo!

Asivyokuwa na aibu sidhani kama atamuomba radhi Vicent Nyerere kwa DEFAMATION!
 
kazi kweli kweli tunasemaga sie vikongwe

Nilikuwa nasubiri comments zako kwa shauku kubwa ... kulikoni hao waandishi wa kambi ya EL?

FP hebu funguka kidogo maana huu mwelekeo sijui hata destination ni wapi, halafu BWM akijua kwamba Balile yuko kambi yenu, huoni kama inaweza kuleta kitimtim?
 
jibu hoja, kwani wamiliki wa Jamhuri ni wawili na wote waandishi, hakuna agenda ya 2015 kama unavyoficha huyo BOSI.Ukweli lazima yasemwe.twasubiri Mengi zaidi.hongera Wanajamhuri mnakuja vizuri.angaza kila kitu.
 
Nadhani hili litakuwa funzo tosha kwa Ben.. Aachane na siasa za kukitetea chama kilichogubikwa na kila aina ya kashfa.. Chama ambacho kimesababisha Tanzania kuzidi kuwa ombaomba duniani.. Wananchi wameamka na wako tayari kudai haki zao at all cost..
 
View attachment 50319

Kama hutaweza kuona vizuri picha hizi ni kwamba zimepigwa mara mbili. Moja ni Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Josephat Kiboko Nyerere, huku pembeni yake akiwepo Anne Mkapa, Maria Nyerere na Chief Japhet Wanzagi.

Nyuma ya Mkapa ni Vincent Nyerere huyu mbunge wa CHADEMA lakini wakati huo yaani December 19, 2007 hajawa mbunge. Utaona picha ya Vincent imezungushiwa duara ili kumuonyesha vizuri.

Hapo ni nyumbani kwa marehemu yaani kwao na Vincent Nyerere.


Picha ya chini ni kwenye misa ya mazishi katika Kanisa Katoliki, parokia ya Butiama. Mnamuona Benjamin Mkapa amekaa kiti cha mbele kanisani akiwa ameshika kitabu akifuatilia misa. Hapa vilevile nyuma ya Mkapa ni Vincent Nyerere.

Kazi kwenu wana JF, the place we dare talk, the place we dare expose the unexposed!

Source:
JAMHURI,
ISSN-1821-8156, No. 17
March 27, 2012
Acha siasa za kijinga ,Mkapa alisema Vicent Nyerere siyo mtoto wa Mwl.Nyerere.Ishu iliyopo hapo ni kumkosoa MKAPA? kuwa ndugu siyo TATIZO,je ni kweli V.Nyerere ni mtoto wa JK Nyerere?.......Acheni uchochezi usio na maana.Arumeru wanataka maendeleo lakini si undugu na NYERERE
 
Kimsingi tuna tatizo kubwa sana la uchambuzi wa kauli mbalimbali na pasipo kuzifikiria kwa kina na kutoa uchambuzi sahihi tunaliweka suala hili kwa UMMA either kwa kujua kwa NIA ya kuupotosha ili wakubaliane nasi au kwa kutokujua; sasa hili la BWM na Vincent mie kwa mtazamo wangu sioni kama kuna haja ya kum'beza BWM kwa kuwa hakulisema kama jinsi suala hili linavyojadiliwa; BWM alizungumzia uwepo wa Vincent kwenye Familia ya Mwl na hakukataa kuwa Vincent si mwana ukoo wa Nyerere; Familia & Ukoo Tafakari"
 
Back
Top Bottom