Picha: Vurugu zilizotokea Kasulu Kigoma Kumpinga Dr. Slaa...

Lakini haujui pia yatawatokea hayo hayo wa CHAMA TAWALA? Unadhani hapo kutakuwa na USALAMA NCHINI? Demokrasia ni UHURU wa KUHUTUBIA na SIO UHURU wa FUJO...

Hapana! DEMOKRASIA NI UHURU WA KUTEUA SIKU FULANI FULANI NA KUZIITA 'PUBLIC DISOBEDIENCE DAYS!'
 
Hizi ni hujuma za wazi za Magamba kwa kushuirikiana na Zitto mwenyewe kunyamazia ujinga huu ambao pia unazid kumchafua zzk, ukitizama kwa makini utagugundua mabango yote ya kaki ni mwandiko na mawazo ya mtu mmoja, herufi kutoka bango moja mpk lingine zinafanana, wanayo haki kufanya hivo lakini wasivuke mipaka though wanatumika vibaya
 
Ningeamini hayo yanatoka moyoni endapo wote wangekua na mabango yana miandiko tofauti, mabango yote yameandikwa na mtu moja, muandiko unajionyesha kabisa, such a bad move... Aliyefanya hivo ana akili ndogo, kuhandle haya mambo inahitaji mtu anayefikiria ana plot kisa kinaonekana hapa kweli hapa, sasa huyu imechukua sekundi kumi kumgundua, what a p.....t
 
Kama namuona Zitto na CCM wanavyogonganisha glass kwa shangwe......Unafiki mpk mbaya sana.
 
wamebeba ujumbe mzito,,jadidi,,dhahiri,,,shazir wanahaki ya kusikilizwa hasa huyo hapo chini mwenye bango la kijani pekee anayeuliza mmiliki wa chama.....ni funzo kubwa kwa vijana wanokwenda kupoteza mda wao CHADEMA ni walaghai na kikundi cha ukabila chenye chuki kubwa sana dhidi ya watanzania wengine yafaa huyo mpangaji wangemtoa koromeo ashike adabu

Inakuhusu nini wewe gamba? kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote akipendacho.nawe unaruhusiwa kuendelea kuganga njaa huko magambani!
 
Hii ni habari ya uongo na hizi picha sio bonafide genuine, ni fake!, mkutano ulikwenda vizuri kabisa, na wapenzi wote wa Chadema walishiriki kikamilimu kwa utii na utulivu wa hali ya juu!. Wale wahuni wachache waliotaka kutuvurugia, sio Chadema, ni CCM wale!.

Pasco

Hahahahaha mzee wa Bonafide Genuine umenichekesga sana.

By the way, hilo bango linalosema Slaa amepewa kura hajaenda kushukuru linasikitisha mno. Slaa amekosa mshauri...
 
Hii ni habari ya uongo na hizi picha sio bonafide genuine, ni fake!, mkutano ulikwenda vizuri kabisa, na wapenzi wote wa Chadema walishiriki kikamilimu kwa utii na utulivu wa hali ya juu!. Wale wahuni wachache waliotaka kutuvurugia, sio Chadema, ni CCM wale!.

Pasco

ha haaaaaa haaaa
 
Hakuna mtu ambaye si mwanasiasa huko Kigoma.

Mrema aliweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kubebwa na kusukumwa kwenye gari.

Slaa ameweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kurushiwa mawe na kufukuzwa jukwaani kwa mabango.

Lipumba aliweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kupewa kibano na polisi.

Slaa ameweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kuwaamrisha polisi wawadhibiti wananchi na kuokolewa na kuhifadhiwa na polisi ili asidhuriwe.

Haya yote ni maendeleo...
 
Huyo babu kwanini hakupigwa mawe. Yeye anafurahia wanasiasa wenzake wakidhalilishwa
 

Makabila Mengine kama yapi hayo ?

Mbona CCM haijawahi kuteua Marais wasiokuwa SUNNI-MUSLIM au CATHOLICS-WAKRISTO ?

Sasa Unataka kuniambia kwasababu hiyo watu wa DINI NYINGINE Nchini wana CHUKI DHIDI ya CCM ???

AU

Yaani nchi yenye wananchi Milioni 40 CHAMA TAWALA kinakosa anayefaa kuwa KATIBU wa ITIKADI CCM toka KATIBU wa ITIKADI MZEE MOSES NNAUYE alipoondoka Madarakani hakuna anayefaa MPAKA wamsubiri MTOTO wake NAPE NNAUYE ??

Kwahiyo CCM inabagua???


FIKIRIA kwanza Wanachokiona ADIMU na UBAGUZI ndani ya CHADEMA pia WAPO wataoona hayo Maubaguzi Ndani ya CCM
poor thinking..........poor analysis you are so cheap
 
Nadhani Watanzania watakuwa wamewasikia na kuyasoma mabango. Kinachofaa kwa sasa, kama wao ni wanachama wa CDM wakihame hicho chama, wajiunge na vyama vingine au kama ikiwezekana, waanzishe chama chao ambacho kitazingatia matakwa wanayoyataka.

Mrema aliweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kubebwa na kusukumwa kwenye gari.

Slaa ameweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kurushiwa mawe na kufukuzwa jukwaani kwa mabango.

Lipumba aliweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kupewa kibano na polisi.

Slaa ameweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kuwaamrisha polisi wawadhibiti wananchi na kuokolewa na kuhifadhiwa na polisi ili asidhuriwe.

Haya yote ni maendeleo...
 
Nadhani Watanzania watakuwa wamewasikia na kuyasoma mabango. Kinachofaa kwa sasa, kama wao ni wanachama wa CDM wakihame hicho chama, wajiunge na vyama vingine au kama ikiwezekana, waanzishe chama chao ambacho kitazingatia matakwa wanayoyataka.
kabisa mkuu
 
Nafikiri tatizo la kina kabisa sio Zitto Kabwe, Zitto Kabwe amekuwa tu kama kondoo wa kafara, kwa bahati mbaya ni kwamba labda anafikiria kwamba harakati hizi zitamsaidia kwa namna fulani kufikia malengo yake na anaziunga mkono chini chini au labda hana jinsi ya kuzikemea kwa sababu zinaratibiwa na watu ambao wako juu yake au zimemzidi uwezo, suala la kwanza na pili naona ndiyo yanayoweza kuwa sahihi zaidi.

Ni jambo la hatari sana kuona kwamba CCM, viongozi wake na makada wake wamefikia hatua ya kukiita CHADEMA kwamba ni chama cha kikabila au chama cha kikanda, binafisi siwaelewi kwa sababu najiuliza itakapofikia wakati wa uchaguzi je CCM watakuwa na UHALALI GANI wa kwenda kwenye majimbo fulani ya uchaguzi ambayo wenyeji wake ni watu wa makabila fulani ambayo CCM kwenye propaganda zao za kijinga za sasa tayari wameshayatenga kwamba makabila haya ni milki ya CHADEMA au CCM itakuwa na UHALALI GANI wa kwenda kwenye kanda zile ambazo tayari makada wake kufuatana na propaganda zao za kijinga wameshasema kwamba kanda hizo ni za CHADEMA?

Binafsi huwa nachukizwa sana ninapoona watu ambao tunawakabidhi kutekeleza majukumu mazito ya nchi na yanayohusu maisha ya watu wengi wakifanya mzaha mzaha tu na kuongea ujinga ujinga tu.

Mheshimiwa John Samwel Malecela ni mwenyeji wa Dodoma, je alipovuliwa umakamu mwenyekiti wa CCM je CCM wangejisikiaje kama viongozi wao wanapofanya ziara Dodoma wanakutana na mabango ya wanachama wa CHADEMA ya kumtaka mwenyekiti wao ajiuzulu kwa sababu tu John Malecela amevuliwa uongozi?

Mheshimiwa Edward Lowasa ni mwenyeji wa Arusha, je CCM ingejisikiaje viongozi wao wanapofanya ziara Arusha au madhalani Monduli wanakutana na mabango ya wanachama wa CHADEMA ambao wanajifanya ni wanachama wa CCM ambao wangemtaka Mwenyekiti wao ajiuzulu kwa sababu tu amekubali kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Lowassa.

Naamini watu wasio na uwezo wa kufikiri na kuweza kutambua hatari iliyoko mbele yetu wanaweza kusema kwamba kitu hicho hakiwezi kutokea kwa CCM na kadhalika, lakini amini nawaambieni utulivu huu unatokana tu na NIDHAMU YA UOGA iliyoko kwenye jamii yetu, pindi nidhamu hii ya uoga itakapoisha katika jamii ya Watanzania mbegu zote hizi za UBAGUZI zilizopandwa na CCM zitajitokeza tu.

Sasa hivi kuna vuguvugu linaloendelea Bungeni kuhusu utendaji wa Waziri Mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda pamoja na Baraza lake la Mawaziri, na sauti nyingi zinazopazwa ni kwamba Waziri Mkuu aondolewe kwenye nafasi yake ikiwemo pia na mawaziri wengine ambao utekelezaji wao hauridhishi, je itakuwaje iwapo wakazi wa mkoa anaotokea Waziri Mkuu wataona kwamba serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi haikuwatendea haki kwa kumwondoa madarakani waziri mkuu Mizengo Pinda, je wenyeji wa mikoa hiyo wafanye vurugu na maandamano barabarani pale viongozi wa CCM na wa serikali watakapotaka kutembelea mikoa hiyo?

Je katika uongozi wa CCM wamekusanya makabila yote ya Tanzania ili kuweza kutuhakikishia kwamba CCM sio chama cha kikabila?

Siasa hizi za ubaguzi tukianza kuziongelea zitachukua miaka mingi bila kuzipatia ufumbuzi, kilichobakia tu ni CCM, viongozi wake pamoja na makada wake kuukubali kwa dhati kabisa ya moyo wao mfumo wa vyama vingi vya siasa, wakubali kabisa kwamba Binadamu siku zote wana mawazo tofauti na wana uwezo tofauti wa kufikiria mambo na kuweza kuyatatua. Wakubali kwamba haiwezekani WATANZANIA WOTE wakawa ni wanachama wa CCM, suala hilo ni UTAAHIRA. Viongozi wa CCM na makada wao warudi kwenye malengo na majukumu ya chama chao, wapigane kutekeleza malengo, majukumu na ahadi za chama chao, hicho ndio kitu pekee kitakachoweza kuwaokoa, KWA BAHATI MBAYA SANA NI KWAMBA HAWAWEZI KUYATEKELEZA HAYO ndio maana wamebakia majungu majungu na siasa za kijinga kijinga.
 
Lakini haujui pia yatawatokea hayo hayo wa CHAMA TAWALA? Unadhani hapo kutakuwa na USALAMA NCHINI? Demokrasia ni UHURU wa KUHUTUBIA na SIO UHURU wa FUJO...

Inaonyesha washauri wa dr. Slaa hawajitambui sababu huwezi kupanga program kwenye ngome ya mtu ambaye watu wanahisi ameonewa au ndo kujaribu Maji Kwa kutia mguu wenzenu wanajaribu kina Kwa kutumia kijiti huwezi kuwakamata watu wanaofikiri democrasia imebakwa. Sababu hiyo ndio demokrasia mtu kupingwa Kwa hoja Na sio mabavu. Peoplesssss ........
 
Back
Top Bottom