PICHA: Vurugu Zanzibar: Mabaki Ya Kanisa Lililochomwa Moto kama ingekuwa Msikiti ingekuwaje?

Status
Not open for further replies.
Watwana na watumwa wakiungana huwa ni balaa tupu..........

1.jpg

Hivi hiyo BENDERA hapo nyuma ya maandamano ni ya NCHI GANI???Wapeni nchi yao waishie huko!
Kwani wakijitenga Zanzibar sisi TANZANIA BARA(Tanganyika) tunapoteza nini??? Kwanza mimi naona ikishatokea Muungano kuvunjika basi sisi nasi TUTARUDISHIWA TANGANYIKA YETU ambayo ilifutwa kwenye ramani ya Dunia tangu 1964.

Let them Go. They will be the loosers not Tanganyika bana.
 
Wengine tunasubiri Serikali ya Mapinduzi itoe tamko rasmi. Suala la kuchoma makanisa linaashiria chuki ya Waislam na Ukristo huko Zanzibar. Huenda hata huku "Tanganyika" linafukuta! Wananchi hatutakuwa na mwingine wa kumlaumu ila Rais tuliyemkabidhi kulinda amani ya nchi yetu.
Tunaomba Waislam wasomi wa Islamic theology watuambie kama mauaji na kuharibu mali, ikiwa ni pamoja na nyumba za ibada za madhehebu yasiyo ya Kiislam, ni mafundisho ya Uislam.
Serikali isilazimishe Muungano at the expense of blood sheding. Let Zanzibar be a Sovereign State so that we Live in peace and not in pieces.Hii itawafanya akina Mzee Mwinyi na Viongozi wengine, na Wanzaibari waishio Tanganyika warudi kuishi Zanzibar au waombe uraia wa Tanganyika. Kuendelea kuwa na Muungano na Zanzibar ni sawa na kuishi na koboka ndani ya nyumba.
 
hawajui kama wenyewe watakuwa ni watwana na wale waarabu(akina jussa and co) watakuwa mabwana wao...

Ukweli ndio huo lakini ni vipofu hawauoni kwasababu ya kuzibwa na pesa toka uarabuni. I wish Mkapa was still Rais wa Jamhuri huu usengee wa hawa jama usingekuwepo kwani angewathibiti big time!!
 
Kweli kuchoma nyumba ya Mungu siyo jambo la kawaida, mfano mwepesi tu ni hapa Arusha kuna kibaka mmoja aliiba jenerator ya kanisa na akaliuza anakojuwa yeye. tamko la kanisa lilikuwa ni alirudishe na hakuna adhabu yoyote ambayo angepewa lakini asiporudisha tunaingia kwenye maombi na litakalomtokea atajua mwenyewe. Huyo jamaa alikamatwa sehemu nyingine anaiba wakamuua na kabla hajafa akasema yeye ndo aliiba kanisani na wapi aliliuza. Kama Watu wa Zanzibar waona kuchoma makanisa ni jambo jepesi wasubiri waone. Hakuna kisasi jambo la kusubiri tu Mungu wa kweli awaadhibu.
 
rais wetu ni dhaifu sana na kibaya zaidi ni mwislamu na anaweza kuwa anapata wakati mgumu kudili na hawa jamaa... halafu kwa nini kila kukiwa na rais mwislamu kunakuwa na haya mambo ya kipuuzi puuzi mengi tu???
 
Kwa haya mambo ya kuchoma makanisa yanayondelea kutokea Zanzibar, amani ya nchi yetu sasa iko njia panda!!! Tuendelee kumshukuru Mungu kwa hekima aliyowajalia wakrito otherwise Tanzania isingekalika!.
 
Hali hii inatisha,inasikitisha tena inahuzunisha sana,Nadhani kama ingekuwa ndo msikiti umechomwa hali ingekuwa mbaya sana, pangekuwa hapatoshi Tanzania na wengi wakristo wangekuwa wakimbizi kwa sababu hakuna wa kuwatetea ila MUNGU wao tu!
 
we angalia kwanza hao viongozi wenyewe waarabu hao wanaitaka io zanzibar dawa yao tuwaache waarabu wakishaichukua hao weusi waanze kutumikishwa, mtoto akililia wembe mpe japo kidogo tu
 
Dah mi najiuliza sijui dini nyingine zilitoka wapi!dini ambayo inalaziisha watu wote tuifate hyo otherwise ndo tuchomewe makanisa?hivi kwan kwenda peponi si ni hiari ya mtu ndomana tumepewa utashi, iweje sasa dini yako inalazimisha watu wote waifuate! kila leo ukisikia mihadhara wakristo wanatukanwa ila ukisikia mkutano wa injil wala uislam hautajwi,inakuwaje sasa waislam wanakosa usingizi sababu ya ukiristo?kama zanzibar hoja nimuungano makanisa yanaingiaje hapo?nimegundua kuishi na muislam tena yule anayejiita mwenye siasa kali ni kazi ngumu kuliko kitu chochote dunian!Anyway Mungu wasamehe ila bora tuvunje Muungano kuliko kunyimana uhuru wa kuabudu hvo!na tukivunja Muungano wazanzibar wote walioko bara warudi kwao kila mtu aishi na aman, we are fed up indeed!
 
Tatizo ni nini? Muungano au Ukristo kuwa Zanzibar. Mimi sielewi elewi. Mihadhara inazungumzia Muungano na kero zake ambazo kila mtanzania anakubaliana nazo. Sasa iweje makanisa yachomwe?Tunaanza kuamini sasa issue siyo kero za Muungano. Issue yawezekana ikawa ni udini.
 
upole wa wakristo unaotokana kristo anasema hata mkitendewa mabaya msirudishe mabaya. Wakristo msilipize endeleeni na amani yenu.
 
Askofu pengo yuko wapi?

mbona hatoi tamko juu ya hili?


Hili pia linatia wasiwasi na niamini kabisa kuwa wenyewe ndio walihoma moto makanisa na kuwasingizia uamsho! siasa ni mchezo mchafu sana! kueni macho binadamu na hila za binadamu , ukiwauliza wenye zanzibar wanakwambia ni njama zilizofanya ionekane uamsho ndio umefanya hivo mbona viongozi wa dini kama Pengo yupo kimya?
 
Tafadhali usihusishe uislamu na jambo hili,hakuna muislamu anaeendezwa na fujo! mbona tuliskia Arusha huko kuna fujo? wale waislamu? zinapotokea fujo arusha WANADAI HAKI, wazanzibar wakidai haki bsi uislamu fujo na matusi mengiii kuweni wastaarabu , hapa litafutwe suluhisho!

Acha upuuzi wewe unakurupuka tu...tumia akili kufikiri....Toa hoja ....Hawa ni waislamu na fujo zao zina malengo ya kidini yanafichwa nyuma ya pazia la Kisiasa na si vinginevyo. the end justify the means
 
Ni rahisi kuongea, wazanzibari sio watanganyika, ni watu wasioogopa kufa , angalia yalotokea bara arabu !

Si mkifia kwenye mapigano ndo mnapata thawabu?? Ama kweli.....shule zimejengwa tuzitumie jamani Lol...
 
Mheshimiwa Rais wangu Kikwete hili janga ni lako. Katikati ya mwanzo wa kujadili mustakabali wa katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ulisikika ukiwafunga breki watz hawataruhusiwa kujadili suala la muungano. Na hata serikali ya Zanzibar ikasikika pia ikishadidia hilo. Watu watajadili na kutoa mapendekezo yepi kama kero za muungano zimekuwa zikiimbwa miaka tangu Uhuru na hazijashughulikiwa. Hayo ndio majibu ya mchezo wenu wa kisiasa kwenye masuala ya msingi.
Hili raisi wangu ulibebe kwa hekima, kwani nguvu hazitatupeleka kuzuri. Waliokuwa wanapeleka ujumbe kwa maandamono ya amani wamefnyiwa hayo kwa ubabe wa polisi na kwa vyovyote kwa maelekezo ya wanasiasa wasiwataalamu wa saikolojia ya wanadamu. Mimi nadhani mngewaacha , wameandamana, wakasema au tuseme wakapasuka hasira zoa na wakarudi majumbani mwao, sasa kukamatana kumekujaje tena?
Na kwa wale waandaji wa maandamano, tunapinga kwa nguvu zote kiligeuza hili la Muungano kuwa la kidini au la kikabila. Kanisa na Muungano vinahusianaje? Kuwataka wabara warudi kwao kuna uhusiano gani na suala la Muungano, kwani wako wazanzibar Sweden, Uingereza, Marekani na huko hakuna Muungano na Tanzania.
HILI RAISI WANGU LINATAKA HEKIMA, TENA YA HALI YA JUU KULISHUGHULIKIA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom