Picha sio umati: Nape atamba kumuumbua Dk. Slaa kesho Singida

Haya Nape tunakusubiri nasikia unataka kumpima oil Dr wa ukweli Dr wa shule. Ila kabla hujaanza wasiliana na riz1 yeye alipima wiki mbili zilizopita sasa akiulizwa anapiga mayowe.

Nape siku tisini umezusha sasa unataka kuja na single ya Dr slaa utaiweza????? Kesho ndio leo. pop corn please
 
Ajenda ya siku tisini imekwisha ngoja tuweke ingine.
Watu wanapenda fleva tofauti;au sio jamani?
 
Huyo dogo hana lolote CCM ya leo ya kuweka mitoto ya english media kwenye secretariet ni bomb litalokuja lipuka punde, hivi baba yako akiwa kiongozi na wewe ni kiongozi? Au ndo yale ya ukikaa karibu na waridi... Halafu Chiligati achunguzwe nahisi anakula miraa(joke)
 
Kwasasa kama ni timu basi CHADEMA ni Barcelona - CCM ni AFC (ya ARUSHA)....yaani mashambulizi ya CDm yana wachanganya sana CCM mpka hawajui wamjibu yupi wache yupi...pole sana CCM naona vitambi vitapungua mwaka huu.....
 
Namhurumia sana huyu kijana, kama alivyosema memba mwingine kuwa huyu kijana anajaribu kudandia gari kwa mbele. Nafikiri ingekuwa vyema amalize kazi iliyondani ya sekretarieti yake na kuwaondoa wachafu kwenye chama chake kabla hajaanza kujipiga kifuani. CCM hakieleweki kinaenda wapi, ingekuwa vyema kutumia muda mwingi kujenga chama kabla ya yeye naye kulipuliwa.
 
Sasa Ndugu Nape anacheza muziki wa CDM, yeye anaongelea ufisadi wa mapacha watatu tu? mbona watuhumiwa niwengi? Je anamuweka wapi Mkuu wao?

Hiyo picha inaonyesha Nape alikuwa anahutubia watu wasiozidi 50! je sasa aoni kwamba hotuba zao hazina tena mvuto?
Tumewachoka!
 
Watu wenyewe wachacheeeeeeeee hivi kweli hao ndio wapenzi wa chama huko singida?

hahahaha,afu akaandika facebook eti mkutano ulikua na mafanikio sana,...how?
hao hapo kama hakuwapa hela ya chumvi hawapati tena maskini
 
duh? amazing 90% ya wachangiaji wanaikandya ccm, lkn mbona kwenye kupiga kura hamjitokezi?

Tunajitokeza halafu KIRAVU na shemejiye MAKAME wanaziiba....usijali 2005 walijipa 80.6%........2010 walijipa 61%.......2015
 
Nape haelewi hata rythim ya muziki anaoucheza, Mukama karudishia gamba na superglue, sasa akingangania kutoa gamba lake atajichuna ngozi. ameshaambiwa hakuna alipewa siku tisini. Sijui ana lipi jipya.:phone:
 
Hebu kwanza nielimisheni maana pengine mimi nilipitwa na taarifa fulani fulani. Nawasikia jamaa wakihutubia kuwa ccm imejivua magamba na sasa ni clean. Tena waliotoka kwa kukata tamaa sasa warudi "maana yale hayatajirudia tena" nakadhalika, nakadhalika. Sasa ambalo mimi sielewi ni kwamba sijasikia badiliko lolote lililofanyika ccm tangu mkutano wa Dodoma ambapo mabadiliko yaliyofanyika pale ilikuwa ni kumuondoa Makamba mkubwa na kumsimika Makamba mdogo, kumsimika Nnauye mdogo kwenye nafasi yake ya sasa na ile hali ya kutakiwa kujitathmini na kuchukua hatua. Hata hivyo sijasikia kama kuna waliojitathmini na kuchukua hatua hadi sasa lakini jamaa wanahubiri kuwa mabadiliko yamefanyika ndani ya ccm sijui ni yapi hayo??? Labda pengine nilipitiwa na usingizi kidogo, hebu mnijuze
 
Tunajitokeza halafu KIRAVU na shemejiye MAKAME wanaziiba....usijali 2005 walijipa 80.6%........2010 walijipa 61%.......2015


Hapo mkuu hesabu ni rahisi: 80.6 - 61 unapata 19.6. Sasa kwa 2015 chukua 61 toa 19.6 = 41.4 na hiyo pamoja na kuchakachua, kiinteligensia na usalama wa taifa.
 
Chama cha magamba kwa kweli kina kufa,labda waanze kujivua na ngozi kbs,ikishindikana wabadilishwe damu labda itasaidia kuondoa damu chafu ya ufisadi,uropokaji na roho ya unafki kwa wananchi.
 
Let me think... kuna uwezekano huyu dogo kupata msaada toka vyombo vya usalama waka-foji document kulingana na matakwa yao ili watumie kuhuburi kuwa ni ufisadi wa Dr. Slaa! mmm... tusubiri tuone.
 
HAwa ni WAJINGA sana maana hapo ni kijiji anchotoka mshikaji wangu.......

Ni barabarani kabisa na hapo inapita RELI na barabara kwenda Mwanza-Dar es salaam. Ni kijiji alichotoka TUNDU LISSU.

Sasa walitegemea waende hapo na wavunje rekodi ya shujaa wao?

Ni sawa na uende MSOGA na utegemee utapata umati wa watu wakati wee ni mtu wa Iringa.
 
Hana jipya, anatapatapa tu lakini tunaofahamu hatushangazi.CCM walikuwa wanatafuta pa kummalizia na sasa wamepapata.Hako kacheo ni njia ya kumpleka kwenye kaburi lake kisiasa.Aendelee tu na propaganda,Nape mwisho wake upo karibu sana kisiasa.RIP NAPE.
 
Sisiem wametegwa kwenye mtego na Chedema na bila kujitambua wametumbukia kwenye 18. Sasa chama tawala kimetangaza rasmi kurudi kwenye kampeni, na ukizingatia kwamba wao hawaungwi mkono wa watu bila kuwapa chochote basi tutarajie Epa nyingine kuzalishwa ili kuendesha hizi kampeni.
Ccm ndio walioshikilia serikali tunataka tupate jibu ni kwa nini mfumoko wa bei umeshamiri na gharama za maisha kupanda kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa toka uhuru.
Nape atueleze ni gamba gani wamelivua ccm na kama ni kweli ajibu je EL, EC na RA wamekwisha kujiondoa kwenye nyadhifa zao ndani ya chama?
Atueleze pia mkuu wao yaani Jk nae anasubiri nini kujivua gamba? Maana kama wametumia tuhuma, yeye jk ni miongoni mwa wanaotuhumiwa(rej: Epa) hao watakaojivua gamba ni lini watafikishwa mahakamani? Vinginevyo namshauri dogo Nape aache kupiga bla bla maana sisi raia tunasumbuliwa na njaa ya kusababishiwa na viongozi mafisadi w chama chake.
AISE NAPE BABAANGU NYAMAZA KIMYA TUTAKUTOA ROHO ATI! TUNA NJAA ILIYOCHANGANYOKANA NA HASIRA KALI!!
.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom