Picha: Kwanini Simba/ Chui hawashambulii watalii wakiwa kwenye gari?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Nimejiuliza Sanaa, nishendaga mbugani mara 2, zote hizo nilikua kwenye closed safari vehicle,
Sasa hawa wanaokua kwenye magari ya wazi Nini kinawalindaa.

gettyimages-82999960.jpg
cheetah-climbs-in-suv-safari-02.jpg
Screenshot_20240319_212937_Google.jpg
animals-dont-attack-safari-vehicle.jpg
Screenshot_20240319_213517_Google.jpg
 
Daaadeki, kuna Mwamba hapo Sijui kama damu ilikua inapita vizuri kwanye veins zake...

Anyway Simba/Chui hufanya attack kulingana na Size, sbb ni kua wanyama hulenga sehemu moja hasa shingo kwa ajili ya Single bite mpk prey afe, Akiona size haimudu basi anaacha, ndio maana Sio rahisi kuona chui akimuwinda Nyati, Simba akimuwinda Tembo/faru/kiboko, hajui aanzie wapi..

Vivyo hivyo kwa mtalii huzani ya kua Wewe/mtalii ni Sehemu ya lile gari Kubwa.
Ndio maana unaambiwa hata akutishie vipi usithubutu kutoka kwenye gari au kusimama akajua kua upo Separate..
Lakini pia hata ukiwa umetulia, usichezeshe macho, akikuangalia na wewe mkazie, usizungushe shingo.

Risk ni kubwa zaidi kwa Leopard ku attack ukiwa kwenye gari tofauti na Simba, nahisi wao wapo more skilled...
Mwisho, Simba/chui humchukulia Binadamu kama Adui zaidi ya Chakula, unavyokua umetulia unamuondolea hofu ya kuhisi hatari.

NOTE: Hii haihusiani KABISA na Tembo.
hapa👇 watu wamebilingishwa wote wapo nyuma, wanataka wamwagwe...
Screenshot_20240319_220306_Gallery.jpg
 
Mazoea waliyozoeshwa na watunzaji wa mbuga yanapelekea wanyama kuwa marafiki kwa aina fulani ya watu ambapo hao askari wanyamapori wanavaa mavazi maalumu ambayo wanyama wanaona hakuna hatari yeyote kuwa karibu nao... Watalii wanakuwa salama seems wanaelekezwa na mna ya kubehave pale mnyama anapowasogelea hata kuwanusa....
 
Lions may perceive safari vehicles as a single large entity, rather than as individual humans inside. They may also consider people to be bony, and find it dangerous and not worth the risk to mess with people.

Google is free.
Sio kweli, simba wakiona mtu yupo juu ya gari wanajua ni mtu,

Hata hao duma unawaona kabisa wanaoanda juu ya gari na kwenda kucheza na hao watalii, wanatambua kuna mtu na kuna gari

Simba hapendi kushambulia watu bali tu pale inapobidi, mfano Simba jike akiwa kajifungua ukimkaribia hata ukiwa juu ya gari anakushambulia.
 
Nami nashangaa ina maana wanaogopa binadam
Hawaogopi binadamu bali chombo walichopo.

Wanyama wanajua chakula chao, hivyo huwa hawawezi attack kitu ambacho huwa hawakili labda kama kimehatarisha maisha yao.

Kuna siku nilikuwa Serengeti tume set camp chini ya mti kumbe kuna chui juu. Aliruka akakimbia.

Huwa nashangaa sana wanaosema koboko (black mamba) huwa anakimbiza watu. Huo ni uzushi labda kama ni nyoka wakutumwa.
 
Hawaogopi binadamu bali chombo walichopo.

Wanyama wanajua chakula chao, hivyo huwa hawawezi attack kitu ambacho huwa hawakili labda kama kimehatarisha maisha yao.

Kuna siku nilikuwa Serengeti tume set camp chini ya mti kumbe kuna chui juu. Aliruka akakimbia.

Huwa nashangaa sana wanaosema koboko (black mamba) huwa anakimbiza watu. Huo ni uzushi labda kama ni nyoka wakutumwa.
Okay
 
Back
Top Bottom