Picha iliyozua utata duniani na kupelekea kifo cha mpiga picha

Hii stori unataka tuchangie au unatukumbusha tu?
maana nahisi kila mtu anaijua...
na ishapostiwa humu mara nyingi mno...


Majitu mabinafsi utayaona tu asa kwa kuwa wewe umeshawai kuisoma basi ndio isiletwe tena humu???

Jf kila dakika wanaingia watu wapya..
Wengine ni wavivu kutafuta habari .

Mfano mimi nipo jf tokea 2015 hii habari sijawahi kuisoma na kuielewa kama nilivyoisoma leo..
Japokuwa hii habari haipatikani jf peke yake..

Tuwe na upendo huyo jamaa hapo juu
kaweka bando kwa pesa yake
,kanunua simu kwa pesa yake
Katumia muda wake kutuletea habari nzuri na yenye funzo..

Wewe unataka kumpangia cha kupost we nani kwani???????????
 
Inahuzunisha! Dunia inaharibiwa na watu wabaya. Lakini inaharibiwa zaidi na watu wema wanao tazama yatendwayo na hao wabaya bila ya kuchukua hatua stahiki.
 
Yaani kwa mara ya kwanza nilipoiona hii habari nilihizunika sana na jamaa alipojiuwa nikasema ni karma imempata
Kweli alikuwa kazini lakini kumuacha aliwe na tai ilikuwa ni maamuzi magumu sana na ya unyama.

Mimi kuona mnyama kazaliwa na akiliwa na mnyama mwingine huwa inaniuma sembuse binadamu tena asiye na uwezo wa kujisaidia



Sent from my SM using Tapatalk
 
screenshot-books.google.co.tz-2018.12.31-23-18-46.png


Tunaomba source mkuu, sababu historia inaeleza tofauti, Kevin alimfukuza huyo ndege na mtoto alipona ingawa alikuja kufariki miaka minne baadae .! ( He chased the bird away )

Source : Google Books
 
Mpaka nimejihisi kulengwa na machozi ... inasikitisha sana . Duniani sio mahala salama kwetu kama ambavyo wengi huwa tunadhani .." ni kwa sababu hatuna tu mahala pengine pakwenda kuishi ndio maana tunapaona kuwa panafaa" dunia imejaa unyama sana .. ona tamaa za madaraka ya watu jinsi inavyo weza kupoteza uhai wa maelfu/malaki/ mamilions ya watu " huku watu wengine wakiendelea kuishi na makovu yasiyo futika ambayo yame sababishwa kwa kuumizwa kihisia. " baada ya kuwapoteza watu wao"

- waliokuwa wanawapenda .. mbaya zaidi wamewapoteza watu hao kwaajili ya maslahi tu ya kikundi cha watu fulani ambao wameamua " kuitoa sadaka amani ya taifa lao kwaajili ya kupigania maslahi yao binafsi ya kisiasa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii story sijawahi kuizoeya kila nikikutana nayo inaniumiza sana....

Fikiria mtu unaumwa njaa mpaka unakufa,yaanni njaa inamuuwa mtu!!mateso gani haya?dah Mungu awasaidie wote wanaohangaika kutafuta mlo wao,sisi tuna shida ila kuna watu wanazo shida ukiambiwa hata kama ulikuwa mgonjwa unapata nguvu.

Sent from my Redmi Note 5 using Jamii Forums mobile app
 
hii story inafahamika ila ukijaribu kufatilia kwa ndani zaidi unaona ni muendekezo wa wazungu kutuona sisi weusi ni wapumbavu..kwa ushahidi wa kimazingira tu hii story maneno mengi ni ya kutunga...!!
 
Inahuzunisha! Dunia inaharibiwa na watu wabaya. Lakini inaharibiwa zaidi na watu wema wanao tazama yatendwayo na hao wabaya bila ya kuchukua hatua stahiki.
Toa credit kwa Napoleon Hill kwa wewe kutafsiri nukuu yake.
 
Back
Top Bottom