Picha: Gamba jipya W. Malecela yuko wapi? Bilal akutana na Watanzania waishio New York

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Katika hafla hiyo hata viongozi wa Jumuiya hiyo hawakuwa nyuma katika kutekeleza majukumu yao kama kawaida japo ilikuwa ni jumapili, hapa ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Miriam Abu (kushoto) na Mweka hazina msaidizi, Mzee Temba, wakiwa na nyaraka zao ambapo pia walikuwa wakiendelea na zoezi la kusajiri Watanzania wapya waliokuwa wakitaka kujiunga na Jumuiya hiyo.

Jumuiya hiyo ilianza kuwa active zaidi baada ya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa kuiongoza uliofanyika mwezi April mwaka huu na kuwapata viongozi wapya kama Mwenyekiti, Haji Hamis na Makamu wake huyo, Katibu Vicent Mughwai na Katibu msaidizi, Shaban Mseba na Mweka Hazina, Phillip Lwiza na msaidizi wake, Mzee temba na sasa Jumuiya hiyo imejipangia majukumu na malengo mengi ikiambatana na mikakati kabambe ya kuwawezesha kusonga mbele katika kujikwamua kiuchumi na kuweza kusaidiana kimaisha.




Sehemu ya watanzania waishio New York na vitongoji vyake, wakianza kukusanyika kwa ajili ya kujiandaa kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa ajili ya kukutana na kuzungumza nao jana Juni 11, 2011.


Idd mtoto wa Kawe jijini Dar es Salaam (kulia) akijumuika na wadau wenzake katika hafla hiyo ya wabongo


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal Balozi Obeni Sefue na Waziri Juma Duni Haji, wakisimama na kuimba wimbo wa maalum baada ya kuwasili kwenye eneo la hafla hiyo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia Watanzania waishio New York na Vitongoji vyake wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo nao na kuwatambua ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.


Pichani Juu na Chini;
Baadhi ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed gharib Bilal alipokuwa akiwahutubia.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake, Haji Hamis akizungumza na kutoa utambulisho wa viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo, ambao hadi sasa wamefiki 110.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa jumuiya hiyo baada ya kuwahutubia.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa jumuiya.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimia na baadhi ya watanzania hao ikiwa ni sehemu ya kuwaaga baada ya hotuba yake.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Zakhia Bilal akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya kinamama wanachama wa Jumuiya hiyo.


Baadhi ya wabongo wakijisevia msosi wakati wa hafla hiyo.


Mchezaji wa zamani wa timu ya Balimi Fc ya Kagera Henri Rwekagingira (wa pili kushoto) akipozi na dada zake kwa picha wakati wa hafla hiyo.


Sufianimafoto pia alikuwa ni miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo hapa akipozi na mchezaji wa zamani wa timu ya Balimi Fc ya Kagera Henri (wa pili kushoto) na dada zake.(Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR).

 
hapo hawezi kuja maana mzee kakosa uongozi na hao kina bilal ndo wachawi wake, natania tu mjomba.
 
hawa warudi kwao bwana wanafanya nini huko? mbona hatuoni mchango wao katika taifa letu hapa wananenepeana tu na kutaka kuonekana kwenye picha hapa.
 
Ama wanafikiri kuishi marekani ni sifa siyo huku bongo tunawabit mbaya huko kazi yao kula tu na kufanya vibarua warudi bwana
 
hawa warudi kwao bwana wanafanya nini huko? mbona hatuoni mchango wao katika taifa letu hapa wananenepeana tu na kutaka kuonekana kwenye picha hapa.


yutong nimecheka sana
kuna jamaa alitoa comment hapa siku chache zilizopita alisema eti wengine wanajiuza kwenye internet,du aisee
si warudi tuu home!
 
William @ New York, USA, hawezi kuhudhuria party za kinafki kama hizo, kwanza watu waliohudhuria hawazidi 30, sasa unataka kuniambia New York kuna Watanzania 30?
Hivyo ni vijumuiya feki vya kugangia njaa na kutafutia ulaji tu, watu waache kupiga box waende kumsikiliza Bilal? this is nonsense.
 
Ama wanafikiri kuishi marekani ni sifa siyo huku bongo tunawabit mbaya huko kazi yao kula tu na kufanya vibarua warudi bwana

wee huoni mr gamba jipya william kila akileta thread lazima aweke new york city
 
hawa warudi kwao bwana wanafanya nini huko? mbona hatuoni mchango wao katika taifa letu hapa wananenepeana tu na kutaka kuonekana kwenye picha hapa.

Afadhali waendelee kukaa huko huko maana bongo hamna dili kabisa.Wakomae tu kitaeleweka.
 
Mazoe kitu kibaya sana, sasa watu wachache namna hiyo Bilal
imetumia mike kuongea nao?

Alafu hii inaleta maswali zaidi, amepata muda wa kuongea, kula,
na kumake fan na watu thelathin, nadhani ilimchukua dhaidi ya saa
moja, lakini hawezi kwenda nyamongo kutoa pole kwa
watanganyika waliokufa kutokana na ubabe unaofanywa na idara
iliyo chini ya mzanzibar mwenzake?

Anyway, ameshindwa hata kuitisha mkutano mmoja tu wa kushukuru
wapiga kura wake huko lindi, wakati hawa na huo ushalobalo wao
hawakuchelewa hata kwenda kwenye kituo cha kupiga kura october 2010.

Poa Bwana Bilali, Zam Yenu hii
 
Miaka 8 hivi imepita nakumbuka nilifika hapo nyumba ya serikali ya Tanzania ndani ya ardhi ya Marekani anapoishi balozi wa Tanzania umoja wa mataifa. Alifika Rais Mkapa kuwasalimia Watanzania na watu tulikuwa wengi sana kiasi cha kukosa viti na nafasi ya kukaa. Niliporudi usiku wa manane nikaongozwa na mwenyeji Lwangisa kupata entrance ya express way rout 95, nilifanikiwa kuendesha gari salama umbali wa ml 320, Mungu ashukuriwe.
Leo waliohudhuria ni kama familia fulani tu ambayo hata haina mvuto wa kumkaribisha Makamu wa Rais hapo Westchester kando ya jiji la NY. Kufilisika huku wa idadi ya watu inanipa jeuri ya kuumbuka serikali yetu kwa wananchi wake. Ingawa itikadi za kuwapokea viongozi wa nchi si za kisiasa bali kitaifa, lakini hii imenishtua nikikumbuka siku tulipokutana na mkapa uwanja huo huo huko Westchester. Nitakapokuja tena NY nitajitahidi kuwahimiza watanzania wajitokeze zaidi.

William Malecela magamba dogo haonikani hapa, labda limo ilikwamba au kupata punch pale Rout 1 au rout 95. Alitakiwa aende kumlaki mkuu wake wa magamba ili aongeze idadi kidogo. Angebuku ukuu wa wilaya kabla hatujafuta nafasi hizo zinazoangamiza bajeti ya sirikali.
 
Mkuu Gamba Jipya ni jina la member humu ngani, next time kuwa makini na heading zako...lols

Respect
 
Back
Top Bottom