PICHA: CHADEMA walivyoisambaratisha Ngome ya Magufuli CHATO

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kagera kimeisambaratisha ngome ya Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, baada ya kufanikiwa kuwahamisha viongozi na wanachama 80 wa CCM akiwamo kada maarufu, Dk. Benedictor Lukanima.

CHADEMA+CHATO.jpg
Vua gamba vaa gwanda ndani ya Chato.

Viongozi na wanachama hao wa CCM wakiongozwa na Dk. Lukanima, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na mtafiti katika Chuo Kikuu cha Norte kilichopo nchini Colombia, walitangaza rasmi kuvua gamba na kuvaa gwanda katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika juzi kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chato mjini, na kuongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kagera, Alfred Mganyizi Rwagatare.
CHADEMA+CHATO+4.jpg
Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare akimkabidhi kadi ya uanachama wa CHADEMA Dk. Lukanima
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jimbo na wilaya hiyo ya Chato, Wana CCM hao waliohamia CHADEMA walikiponda vikali chama tawala, kwa madai kwamba serikali yake imeshindwa kuwasaidia wananchi kuondokana na kero nyingi, ukiwemo umaskini wa kupindukia unaozidi kuota mizizi hapa nchini.
CHADEMA+CHATO+3.jpg
Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare akimkabidhi kadi ya uanachama wa CHADEMA Makonzela Phinias.
Baadhi ya viongozi wa CCM waliohamia CHADEMA ni pamoja na Makonzela Phinias ambaye alikuwa mjumbe wa UVCCM na mwakilishi wa mkutano mkuu wa Vijana Mkoa wa Geita, Masunga Maswanzali, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji cha Nyasenga, Kijiji na Kata ya Ilemela, Josephat Manyenye ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM pamoja na Dk. Benedictor Lukanima, ambaye mwaka 2010 alishika nafasi ya pili katika kura za maoni ndani ya chama hicho tawala.
CHADEMA+CHATO+5.jpg
Makusanyo ya kadi yakiendelea.
Akihutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare alimrushia kombora zito Waziri Magufuli kwa madai kwamba, kiongozi huyo ameshindwa kuondoa kero nyingi zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, ikiwamo ya uhaba wa huduma ya maji, afya, elimu na fursa za kiuchumi jimboni humo.
CHADEMA+CHATO+7.jpg
Kadi zilizorejeshwa.
Lwakatare alimuita Dk. Magufuli bingwa wa takwimu aliyeshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake, licha ya kuwa waziri kwa muda mrefu serikalini. "Magufuli ni bingwa mkubwa wa takwimu. Anaweza kuwaambieni hadi samaki walio na mimba Ziwa Victoria. Lakini ameshindwa kutoa takwimu za wanafunzi wanaokwenda shuleni bila viatu wala ‘yebo yebo'.


"Wakati umefika sasa wananchi wa Chato kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015, pigeni kura za hasira baina ya CCM na huyu Magufuli, kisha kuwachagua viongozi wa CHADEMA kwa maendeleo yenu," alisema Lwakatare.
CHADEMA+CHATO+9.jpg
Ulinzi uliimarishwa eneo la tukio nayo amani ikatawala.
Kuhusu bei ya pamba, Lwakatare ambaye amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), kabla hajahamia CHADEMA, alisema: "Serikali ya CCM pamoja na Magufuli imeshindwa kuwasaidia wakulima wa zao hili la pamba."
CHADEMA+CHATO+1.jpg
Dk. Lukanima na wenzie wakitoka kwenye mkutano.
Kwa upande wake, Dk. Lukanima aliituhumu CCM na serikali kwa kukosa mwelekeo wa kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
"CCM imekosa mwelekeo. Mimi na usomi wangu huu siwezi kuendelea kuwa ndani ya CCM ambayo naiona haina faida kabisa kwa Watanzania wenzangu. Hivi niwaulize ni yupi mwenye unafuu aliyeshika chuma cha moto na aliyeshika ubao?

"Jibu ni aliyeshika ubao...kwa hiyo njooni tujiunge na CHADEMA kwa ajili ya ukombozi wa nchi hii. Mfano, hapa Chato hakuna fursa za kiuchumi, mashirika yamekufa, huduma za kijamii mbovu, na anayeng'ang'ania CCM ni sawa na usaliti mkubwa wa maendeleo ya taifa hili," alisema Dk. Lukanima.

Aliwaomba wananchi wa Chato, mkoa na taifa kwa ujumla kukiunga mkono Chama hicho cha CHADEMA, ili kujikomboa na adha mbalimbali zinazolikabili taifa na wananchi wake, na kwamba kilichomsukuma kuhamia chama hicho cha upinzani ni kwenda kuongeza nguvu katika vuguvugu la mabadiliko.
 
Mkuu hiyo ya kadi ya njano naiona vibaya! ni kama ina nembo ya JW vile? Lol Vuguvugu la mabadiliko noma!!
 
Hali ikiendelea hivi huko chato, soon magufuli atasema "sitagombea tena ubunge, nataka nipumzike"
 
Hivi hizo kadi za CCM zinazorudishwa si wanazichoma moto? Hazina maana kabisa
 
"chadema ni chama cha kaskazini"-Nape, sasa sijui chato iko kaskazini ipi...
 
Good bye CCM.
MAGAMBA wamepoteza jimbo la chato Mh.Magufuli jipange 2015.
 
Mkulu ....KUNA KADI YA NJANO HAPO NA YA BLUE HAPO NA NYEUPE HAPO...Mkulu tuelezee ni za vyama Gani!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Unajua sisi Watanzania tuna kasumba mbalimbali, kwa mfano..Uwezo wa kukariri wa Magufuli unatufanya tumkubali na kusahau majukumu anayopaswa kufanya. Ila tuwe waungwana, The man (Magufuli) does the Job. Japokua alinitpka rohoni kwenye kashfa ya kuwauzia nduguze nyumba za serikali kwa bei ya debe la Mtama.
 
Vipi kuhusu Dk. Benedictor , ni daktari wa philosophy au binadamu? Na vipi kuhusu CV yake hapo CHATO anaweza kutufanyia mageuzi mkuu?
Na dulu za siasa zinasemaje hapo kuhusu mchakato wa chaguzi za serikali za mitaa na vijiji pamoja na viongozi ndani ya nyama vyote kwa ujumla?
 
Back
Top Bottom