Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,676
- 29,884
Ninaweka mtazamo wenye mjadala ndani yake. Ninawaomba wananzengo msiugeuze mjadala kuwa eneo la dhihaka bali tuliangalie hili jambo kwa macho mawili.
Baba wa Taifa pamoja na kuwa busy sana kuliko waliomfuatia aliweza kuandika hotuba zake na hata kuchapisha vitabu vingi kuliko marais wote Africa. Alikuwa pia anatoa makala keenye magazeti na majarida mbalimbali.
Marais waluofuatia baada ya Mwalimu walichoweza kuandika labda ni CV zao kwani walisaidiwa kila kitu na wasaidizi wao.
Kuna utamaduni umeanzishwa Tanzania na baadhi ya nchi za Africa ambapo taasisi za elimu ya juu zimekuwa zikiwatunuku shahada za Uzamivu viongozi wakuu wa nchi. Sababu ama merits zinazotumika kuwahalalishia ni mafanikio kwenye eneo la uchumi au maendeleo. Lakini ukifanya tathmini ndogo utagundua nchi zao hazipo hata kwenye uchumi wa kati kwa maana nyingine wapo katika umaskini wa kutupwa.
Kuna maswali kadhaa ya kujiuliza;

- Jopo la Wanazuoni wanaopitisha hizo shahada kwa viongozi wakuu, huwa wanajiona wapo sahihi kulazimisha taswira isiyo na ukweli iambatane na sifa za PhD?
- Je, hii inawezekana ni muendelezo wa rushwa ndani ya sekta ya elimu? Yaani wasomi wanajipendekeza wakumbukwe na mtawala kupitia recognitions za shahada ya uzamivu bila vigezo vitakiwavyo?
- Inawezekana sasa tuamini kwamba hali yetu mbaya kiuchumi na kisiasa ni usaliti wa wakufunzi wetu wanaowaandaa wasomi ambao hushindwa kuitumia elimu yao kwa maslahi ya nchi?
- Vipi kuhusu unafiki?