PhD za nchi yetu hizi

Darren2019

JF-Expert Member
Nov 23, 2019
1,112
2,379
Viongozi wenzangu,

Nawasalimu Kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ufuatiliaji unaofanyika shuleni na OR TAMISEMI Umebaini mambo mengi ikiwa ni pamoja na:

1. Baadhi ya walimu ktk Shule za Sekondari wameanza kufundisha maudhui ya masomo mbalimbali wakati Wanafunzi hawajawezeshwa kuwa na umahiri wa stadi za lugha ya kiingereza kama ilivyobainishwa kwenye baseline student book na teachers guide ya Taasisi ya elimu; pamoja na Mkakati wetu wa kuboresha ufundishaji wa English orientation course kipengele cha 3.3.3.1.

2. Imebainika pia Wanafunzi hawawezi kuandika Short stories angalau kwa kurasa mbili. Aidha, imebainika wanafunzi hawajaweza kufanya na kumudu midahalo ya kiingereza kwa ngazi yao.

3. Baadhi ya Shule zilizotembelewa zinaonekana kufuata utaratibu waliozoea kila mwaka wa kuanza kufundisha maudhui ya masomo hata kama wanafunzi hawaelewi kinachofundishwa ( business au usual).

4. Shule nyingi katika mikoa iliyotembelewa hazikuwa na barua za maelekezo ya kuzingatia katika ufundishaji wa kiingereza kidato cha kwanza ( kwa sekondari) na darasa la tatu ( kwa shule za msingi) kama ilivyoelekezwa awali. Hivyo, baadhi ya viongozi wa shule wametumia kigezo hicho kuwa hawakuwa na maelekezo kutoka kwenu ya maandishi; ndiyo maana wameendeleza utaratibu waliozoea.

5. Kufuatia hali halisi hiyo, nawaelekeza kuhakikisha kuwa:

(a) Wanafunzi wa kidato cha kwanza wanamudu umahiri wa lugha ya kiingereza ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuwasiliana, kujadiliana na kuandika kwa lugha ya kiingereza angalau kurasa mbili kabla ya kuanza ufundishaji wa maudhui ya masomo.

(b) ufundishaji wa english Darasa ya Tatu kuimarishwa kama ilivyoelekezwa awali ili kujenga msingi imara wa lugha hii.

(c) Waelekezeni Wakuu wa Shule/walimu wakuu kuzingatia maelekezo haya ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote wanaokiuka kwa kuendeleza utaratibu waliozoea kufanya usioleta tija.

6. Endapo tutabaini uwepo wa kiongozi yeyote ambaye anashindwa kusimamia utekelezaji wa maelekezo haya kwenye Shule zilizo kwenye eneo lake kama inavyoonekana Sasa kwenye baadhi ya shule tutalazimika kumchukulia hatua.

7. Dhamira ya kutembelea shule kwa kila kiongozi wa ngazi za mkoa, Halmashauri na Kata ililenga kuwawezesha ninyi viongozi kujua kinachofanyika kwenye shule zote na kuchukua hatua stahiki ili kuleta tija ya elimu inayotarajiwa kwa kila mwanafunzi mmoja mmoja. Zingatieni kwa dhati dhamira hiyo.

Nawatakia utekelezaji mwema.

NAIBU KM
DR.CHARLES MSONDE
 
Tukishauri lugha ya kufundishia iwe kiingereza kuanzia shule za msingi hawasikii.

Ebu niambieni sasa muhula ndo unakwisha hivyo, kidato cha kwanza wanasoma utangulizi tu, tena mambo ambayo hayapo kwenye muhtasari wa somo, walimu tutamaliza vipi hizo mada?

Kwanini wasitibu tatizo kwenye kiini badala ya kuja na maagizo ya kila wiki?

Kidato cha kwanza tunapokea watoto hata kuandika kiswahili hawawezi, ni lini watamudu kuandika habari kurasa mbili tena kwa lugha ya kiingereza?

Mwaka huu tutafundisha Orientation course mwaka mzima?

Ni lini watanzania tulimudu lugha ya kiingereza? Hatuoni hata viongozi wetu wanapuyanga tu?
 
Kwani msonde yeye alijua kiingereza Akiwa Form ngapi? Walimu wenyewe hawakiwezi then iwe kwa mtoto tena huku pori vijana wanaongea kilugha chao tuu. Kiswahili chenyewe hawakijui.SHIDA SANA
 
Watu hadi wamekuwa maprofesa na bado lugha haipandi, sembuse hao wa kufundishwa miezi mitatu!!
 
Kwani msonde yeye alijua kiingereza Akiwa Form ngapi? Walimu wenyewe hawakiwezi then iwe kwa mtoto tena huku pori vijana wanaongea kilugha chao tuu. Kiswahili chenyewe hawakijui.SHIDA SANA
Mkuu nafundisha Physics kidato cha kwanza hadi cha nne, kidato cha kwanza kina mada 9, hadi sasa sijaanza hata moja, hapo kumbuka pia napambana na mada 9 za kidato cha pili ambao wana mtihani wa taifa mwezi wa 10, kidato cha nne nao nawapambania wavuke salama.

Wakifeli lawama kwangu.
 
Mkuu nafundisha Physics kidato cha kwanza hadi cha nne, kidato cha kwanza kina mada 9, hadi sasa sijaanza hata moja, hapo kumbuka pia napambana na mada 9 za kidato cha pili ambao wana mtihani wa taifa mwezi wa 10, kidato cha nne nao nawapambania wavuke salama.

Wakifeli lawama kwangu.
Mkuu kuna mwalimu alipelekwa chuo kipo bush kidogo so alichofanya asubuhi pindi kama kawa ila kuanzia jioni Kuna extra classes za lugha.

Sijui utaratibu ukoje ila ilitakiwa either pre form 1 iwe compulsory hasa lugha, ama kuweka extra classes za lugha, au English ianze tokea primary otherwise ni ngumu mtu kujifunza English form 1 ilihali miaka 7 amekariri concepts kwa kiswahili.
 
Back
Top Bottom