PhD ya Magufuli na wanasiasa wengine zichunguzwe upya!

Narudi kwenye hoja
Kuna PhD za aina 2 kuu. 1.PhD by Monography, hii unafanya utafiti wako na kuandika thesis ya kitabu kikubwa hivi . Aina hii ya PhD haina ulazima wa wewe kupublish ila unaweza kufanya hiyo kwa mapenzi yako na pia pia supervisors wako. Nadhani hi aina ya PhD ndo aliyoofanya Mhe. JPM hapo UDSM. Hongera Mhe Rais

2. PhD by publications. Hii aina ya PhD ni lazima uwe na machapisho . Mangapi, inategemea na chuo. Zingine zinataka hata 2 published + 2 submitted au 3 .... Hii ni aina ya PhD inayokulazimu utoe machapisho.

Kwa maoni yangu, hata kama umefanya PhD by monograph ni vizuri ku kupublish hata paper 1-2 , hata baada ya kumaliza course ili uweze kushare findings zako na dunia ingine. Kwani ugunduzi wako unaweza kuwa na maana kubwa kwa watu wengine hata kuzidi wewe na wakautumia vizuri. Si vyems kabisa kuweke findings zako LIBRARY TU.

Nguvu ha hoja ya mtoa Mada, ni kwamba, Utafiti wa wasomi wetu wanao upata utumike kutatua matatizo ya wananchi na siyo kubaki LIBRARY au kwenye JOURNALS. So Mhe JPM asaidie kuonyesha mfano, hasa ukizingatia anamamlaka na knowledge, huo utafiti wake ujiuyonyeshe katika kuwasaidia au kutatua shida za wananchi. Kufanya hivyo kuan weza kusaidia policy zetu za utafiti zilenge moja kwa moja kutatua matatatizo ya nchi na isiwe mtu akifanya utafiti anaenda kuweka kwenye kabati wakati kodi za wananchi zilitumika na hivyo wananchi lazima wapate matunda. Hili litakuwa somo zuri kwetu kama Mhe JPM ataanza na hizo korosho.
 
Habari wana JF,

Ni siku ya jana nilibandika andiko la kutafuta chapisho la PhD holder Rais Magufuli. Sikuwa na maana mbaya kama baadhi walivyodhani na kudai sina haja na chapisho bali kuzungumzia elimu yake. La hasha hiyo haikuwa maana yangu.

Nilikuwa na malengo ambayo mimi naweza kupambanua kama ifuatavyo:

Kwanza kabisa nilitaka kujua kama kweli hawa wasomi wetu wanazitendea haki elimu zao, au ndiyo tunasoma kwa ajili ya "title tu". Pili nilitaka kuonesha ni aina gani ya elimu tuliyonayo hapa nchini hasa sayansi kama nitakavyoeleza kwenye aya zinazofuata hapo chini. Kwa mtazamo wangu mimi naona bado tunasoma historia ya sayansi. Kama research za PhD. zinakuwa ni research ambazo zinaongelea jambo lilishasemwa na wanasayansi wengine, je hii si historia ya sayansi? Kwa nini tuendelee kung'ang'ana na upangaji madaraja na viwango vya elimu na si kuhangaika kubadili mfumo wa elimu ili uwe ni ule utakaompa mwanafunzi ujuzi na maarifa katika tasnia husika?

Thesis ya Mh. ina title ya "The potential of anacardic acid self assembled monolayer from Cashew Nut Shell Liquid as corrosion protection coatings".
Kwa wanakemia hasa wale wa organic chemistry wanajua hizi ni alkenylphenols ambazo zinapatika kwenye maganda ya korosho. Hiyo anacardic acid ndiyo inapatika kwa wingi katika hayo maganda. Hata aliyemsimamia research hiyo Dk. Magufuli ambaye ni Dk. Joseph Buchweishaija aliwahi kufanya kazi ya kuitenganisha yeye na wenzie walifanikiwa ku-isolate kwa asilimia 82% wakitumia sample ya 3g ndani ya dakika 150.

Ni kweli moja wapo ya kazi ambayo hiyo acid inaweza kufanya ni kuzuia kutu kwa kuzuia oxidation. Si lengo langu kufundisha kemia kwenye uzi huu, point yangu ni hii;
Mtwara kuna korosho, bahati nzuri aliyefanya research hii ndiye Rais wa nchi hivi sasa. Imeshindikana je kuitafsiri research hii katika vitendo na badala yake imehifadhiwa kwenye makablasha hapo UDSM? Mimi nilishangaa sana jana watu walivyokuwa wananiambia nikaitafute kwenye library ya UDSM. Hivi kweli hilo ndiyo lengo la kufanya research? Tutaendelea kufanya tafiti za kutunukiwa degree tu na kuachana nazo mpaka lini?

Kwa mtazamo wangu mimi naona mfumo mzima wa elimu yetu unakasoro bila kujali ni level ipi. Unahitaji kushughulikiwa ili kuondoa fikra za nadharia zilizotawala vichwa vyetu. Ufike wakati tutafsiri nadharia kwa vitendo, hapo tutasonga mbele na si kupangua alama za ufaulu na sifa za kwenda Vyuo vikuu.

Tunapong'an'ania kuwa elimu bora ni kupata "A" tu kwenye karatasi ni kujidanganya kuwa tuna maarifa kumbe ni maarifa ya nadharia tuliyoyaacha kwenye karatasi. Ni nani asiyejua kuwa hizi "A" zinapatikana kwa kukesha tukisolve lundo la mitihani iliyopita? Hata huko vyuo vikuu watu wanahangaika kupata mitihani iliyopita wakibahatisha basi ni "As" na GPA za 4.5 hewa? Katika chuo kikuu kimoja hapa nchini vijana wanasoma Bsc. Physics mwaka wa kwanza hadi wa pili practical kubwa wanayofanya kila semister ni ya Cathode Ray Oscilloscope kustudy frequency za source za umeme kama DC generator, halafu hawa ndiyo watakuwa technologists kweli?

Natoa Rai kwa serikali hii kama kweli ina nia ya dhati katika kuboresha elimu isihangaike tu na madaraja na viwango vya ufaulu, bali twende kwenye elimu ya kutenda zaidi si ufaulu wa karatasi tu. Tunahitaji falsafa mpya ya elimu. Inawezekana je mtu anasoma mechanical engineering miaka minne lakini aingie workshop mwaka mmoja tu? Ni hayo tu, sikuwa na maana ya kukosoa elimu ya bwana mkubwa bali falsafa ya elimu tuliyong'ang'ania ya ufaulu wa makaratasi.

Mkuu ulichesema ni kweli tupu. Mfumo wa elimu yetu unakasoro kubwa. Tuna vipanga wengi kwenye makaratasi tu. Mtu ana GPA nzuri sana lakini maarifa aliyonayo hayaendani na hiyo GPA yake. Hapa suala zima la kuhire wafanyakazi tunazingatia sana vyeti badala ya kuzingatia demonstration anayo present mhusika siku ya usahili. Tunashindwa kujua hizo A mara nyingi watu wanazipata kwa kudesa ili wafaulu mitihani. Nchi nyingi zilizoendelea mtu anapoomba kazi anawasilisha CV tu wala hawahitaji matokeo yake. Ukweli utajulikana kama kweli alichokiweka kwenye CV yake kinaendana na alichonacho kichwani. Elimu ya nadharia haitoweza kutufikisha popote kabisa kama hakutafanyika total transformation ya mfumo wa elimu yetu.
 
Tupaze sauti tutasikika na tutaeleweka.
 
Mtoa mada , asante , hoja yako ni nzuri ingawa naona watu kama akina YEHODAYA wanaanza kuleta siasa hapa. Namuomba hii mada asije akachafua.

Narudi kwenye hoja
Kuna PhD za aina 2 kuu. 1.PhD by Monography, hii unafanya utafiti wako na kuandika thesis ya kitabu kikubwa hivi . Aina hii ya PhD haina ulazima wa wewe kupublish ila unaweza kufanya hiyo kwa mapenzi yako na pia pia supervisors wako. Nadhani hi aina ya PhD ndo aliyoofanya Mhe. JPM hapo UDSM. Hongera Mhe Rais

2. PhD by publications. Hii aina ya PhD ni lazima uwe na machapisho . Mangapi, inategemea na chuo. Zingine zinataka hata 2 published + 2 submitted au 3 .... Hii ni aina ya PhD inayokulazimu utoe machapisho.

Kwa maoni yangu, hata kama umefanya PhD by monograph ni vizuri ku kupublish hata paper 1-2 , hata baada ya kumaliza course ili uweze kushare findings zako na dunia ingine. Kwani ugunduzi wako unaweza kuwa na maana kubwa kwa watu wengine hata kuzidi wewe na wakautumia vizuri. Si vyems kabisa kuweke findings zako LIBRARY TU.

Nguvu ha hoja ya mtoa Mada, ni kwamba, Utafiti wa wasomi wetu wanao upata utumike kutatua matatizo ya wananchi na siyo kubaki LIBRARY au kwenye JOURNALS. So Mhe JPM asaidie kuonyesha mfano, hasa ukizingatia anamamlaka na knowledge, huo utafiti wake ujiuyonyeshe katika kuwasaidia au kutatua shida za wananchi. Kufanya hivyo kuan weza kusaidia policy zetu za utafiti zilenge moja kwa moja kutatua matatatizo ya nchi na isiwe mtu akifanya utafiti anaenda kuweka kwenye kabati wakati kodi za wananchi zilitumika na hivyo wananchi lazima wapate matunda. Hili litakuwa somo zuri kwetu kama Mhe JPM ataanza na hizo korosho.

Umeeleweka mkuu ! Especially hapo kwenye aina za PhD .,.

Tukirudi kwenye kuziweka kwenye vitendo, inakuwa ngumu kidogo.. Na hili linaanzia mbali sana , katika shule zetu za sekondari, nakumbuka tulikuwa tunajibu mtihani wa kemia practical bila kufanya hizo practical zenyewe ( kama mnakumbuka titration ) na walimu walikuwa wanatufundisha kabisa kufanya zile calculations , kwa ufupi that was cheating ...

Wanasema mwana umleavyo ndivyo akuavyo, mabadiliko inabidi yaanze chini kabisa...
 
Kwa vile sipo kwenye usaili siwezi jibu. We kama unajua mwaga nondo nikusome.

Naomba nikurahisishie swali, kwanini university graduate student mwenye First Class GPA na tena ni best student akiingia kwenye soko la ajira ana perform to the minimum level tofauti na ufaulu alopata chuoni?
Kuthibitisha hilo utakubaliana na mimi waajiri wengi hulalamika na kuona wameingia hasara kwa kuajiri unskilled worker/mzigo ambapo hupelekea aibu kwa Chuo na zaidi mwanafunzi husika.
 
Umeeleweka mkuu ! Especially hapo kwenye aina za PhD .,.

Tukirudi kwenye kuziweka kwenye vitendo, inakuwa ngumu kidogo.. Na hili linaanzia mbali sana , katika shule zetu za sekondari, nakumbuka tulikuwa tunajibu mtihani wa kemia practical bila kufanya hizo practical zenyewe ( kama mnakumbuka titration ) na walimu walikuwa wanatufundisha kabisa kufanya zile calculations , kwa ufupi that was cheating ...

Wanasema mwana umleavyo ndivyo akuavyo, mabadiliko inabidi yaanze chini kabisa...
Nadhani ni muda muafaka kuanzia huko chini unakokusema, elimu iwe ya ujuzi na maarifa. Mtu ahukumiwe kwa maarifa aliyoyapata shuleni na si alikariri vipi maswali.
 
hua ninapata faraja sana nikiona bado kuna watanzania wenye kufanana na huyu mtoa mada, i know that i am not a phd holder and i don't know much about getting a phd but maybe one day i will, but surely we as countrymen really need to have constructive thoughts like this man, this is how you help your country to move from one poor state to a better state, this is what we really need to plant in our minds if we need a better system for better changes.

Ni bahati mbaya sana watu wenye kuweza kuleta michango chanya kwa taifa wamekua adimu kama kakakuona, si ndani ya chama tawala au vyama vya upinzani ( so called UKAWA ) wote wamekua ni watu wenye kuendekeza siasa zisizokua na tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla na yawezekana hii ndoto ya kua angalau nchi yenye uchumi wa kati tukaendelea kuiota kwa kipindi kirefu mbele unless watu wenye mawazo chanya kama mtoa mada waongezeke nchini.

what is the use of being a professor or phd holder if your knowledge is not helping us as a country? we won't manage to compete with the developed countries if we continue to provide this kind of education to our children, it surely won't get us anywhere. I am saying this because am among the victims of this poor education system in our beloved country, may the Lord God help to heal this country.

China poised to overhaul US as biggest publisher of scientific papers
source: China poised to overhaul US as biggest publisher of scientific papers

Royal Society report shows China pushing UK into third place in scientific publishing and predicts it will soon surpass the US

China could overtake the United States as the world's dominant publisher of scientific research by 2013, according to an analysis of global trends in science by the Royal Society. The report highlighted the increasing challenge to the traditional superpowers of science from the world's emerging economies and also identified emerging talent in countries not traditionally associated with a strong science base, including Iran, Tunisia and Turkey.

The Royal Society said that China was now second only to the US in terms of its share of the world's scientific research papers written in English. The UK has been pushed into third place, with Germany, Japan, France and Canada following behind.

"The scientific world is changing and new players are fast appearing. Beyond the emergence of China, we see the rise of South-East Asian, Middle Eastern, North African and other nations," said Chris Llewellyn Smith, director of energy research at Oxford University and chair of the Royal Society's study.

"The increase in scientific research and collaboration, which can help us to find solutions to the global challenges we now face, is very welcome. However, no historically dominant nation can afford to rest on its laurels if it wants to retain the competitive economic advantage that being a scientific leader brings."

In the report, published on Monday, the Royal Society said that science around the world was in good health, with increases in funding and personnel in recent years. Between 2002 and 2007, global spending on R&D rose from $790bn to $1,145bn and the number of researchers increased from 5.7 million to 7.1 million.

Hapa nataka kuonesha tu kwamba ku-publish ni jambo la muhimu sana kwa msomi yeyote
 
hua ninapata faraja sana nikiona bado kuna watanzania wenye kufanana na huyu mtoa mada, i know that i am not a phd holder and i don't know much about getting a phd but maybe one day i will, but surely we as countrymen really need to have constructive thoughts like this man, this is how you help your country to move from one poor state to a better state, this is what we really need to plant in our minds if we need a better system for better changes.

Ni bahati mbaya sana watu wenye kuweza kuleta michango chanya kwa taifa wamekua adimu kama kakakuona, si ndani ya chama tawala au vyama vya upinzani ( so called UKAWA ) wote wamekua ni watu wenye kuendekeza siasa zisizokua na tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla na yawezekana hii ndoto ya kua angalau nchi yenye uchumi wa kati tukaendelea kuiota kwa kipindi kirefu mbele unless watu wenye mawazo chanya kama mtoa mada waongezeke nchini.

what is the use of being a professor or phd holder if your knowledge is not helping us as a country? we won't manage to compete with the developed countries if we continue to provide this kind of education to our children, it surely won't get us anywhere. I am saying this because am among the victims of this poor education system in our beloved country, may the Lord God help to heal this country.
Unaweza kufarijika zaidi ukiwa na taifa ambalo uongozi uliopewa dhamana ya kuongoza linatambua umuhimu wa kuyapa nafasi mawazo ya wengine ilimradi yanaweza kusaidia kuchochea ukuaji wa maendeleo katika nchi. Siasa ni muhimu sana hapa; kwamba ni watu wa gani tunawapa kura zetu ili watuongoze? Je, chama tunachokipa madaraka kipaumbele chake ni nini? Siasa zisizo na tija zinatokana na watu wanaoamua kuchagua kutoelewa wanataka nini, na wanaoelewa wanataka nini wanajiweka pembeni kusubiri kulaumu wanasiasa kuwa wanafanya siasa zisizo na tija wakati wao wenyewe wanaweka madarakani watu wasiopenda kuona au kusikia "critical thinking"! Na mbaya zaidi hao wanaoelewa wanataka nini wanakuwa wepesi kupofushwa kwa mabo yenye faida ya muda mfupi, tena kwao wenyewe, na wala sio kwa jamii pana zaidi!
 
Kupiga kura huwa ni ushahidi tu lakini kinachotokea baada ya kupiga kura huwa hakijulikani.
 
Habari wana JF,

Ni siku ya jana nilibandika andiko la kutafuta chapisho la PhD holder Rais Magufuli. Sikuwa na maana mbaya kama baadhi walivyodhani na kudai sina haja na chapisho bali kuzungumzia elimu yake. La hasha hiyo haikuwa maana yangu.

Nilikuwa na malengo ambayo mimi naweza kupambanua kama ifuatavyo:

Kwanza kabisa nilitaka kujua kama kweli hawa wasomi wetu wanazitendea haki elimu zao, au ndiyo tunasoma kwa ajili ya "title tu". Pili nilitaka kuonesha ni aina gani ya elimu tuliyonayo hapa nchini hasa sayansi kama nitakavyoeleza kwenye aya zinazofuata hapo chini. Kwa mtazamo wangu mimi naona bado tunasoma historia ya sayansi. Kama research za PhD. zinakuwa ni research ambazo zinaongelea jambo lilishasemwa na wanasayansi wengine, je hii si historia ya sayansi? Kwa nini tuendelee kung'ang'ana na upangaji madaraja na viwango vya elimu na si kuhangaika kubadili mfumo wa elimu ili uwe ni ule utakaompa mwanafunzi ujuzi na maarifa katika tasnia husika?

Thesis ya Mh. ina title ya "The potential of anacardic acid self assembled monolayer from Cashew Nut Shell Liquid as corrosion protection coatings".
Kwa wanakemia hasa wale wa organic chemistry wanajua hizi ni alkenylphenols ambazo zinapatika kwenye maganda ya korosho. Hiyo anacardic acid ndiyo inapatika kwa wingi katika hayo maganda. Hata aliyemsimamia research hiyo Dk. Magufuli ambaye ni Dk. Joseph Buchweishaija aliwahi kufanya kazi ya kuitenganisha yeye na wenzie walifanikiwa ku-isolate kwa asilimia 82% wakitumia sample ya 3g ndani ya dakika 150.

Ni kweli moja wapo ya kazi ambayo hiyo acid inaweza kufanya ni kuzuia kutu kwa kuzuia oxidation. Si lengo langu kufundisha kemia kwenye uzi huu, point yangu ni hii;
Mtwara kuna korosho, bahati nzuri aliyefanya research hii ndiye Rais wa nchi hivi sasa. Imeshindikana je kuitafsiri research hii katika vitendo na badala yake imehifadhiwa kwenye makablasha hapo UDSM? Mimi nilishangaa sana jana watu walivyokuwa wananiambia nikaitafute kwenye library ya UDSM. Hivi kweli hilo ndiyo lengo la kufanya research? Tutaendelea kufanya tafiti za kutunukiwa degree tu na kuachana nazo mpaka lini?

Kwa mtazamo wangu mimi naona mfumo mzima wa elimu yetu unakasoro bila kujali ni level ipi. Unahitaji kushughulikiwa ili kuondoa fikra za nadharia zilizotawala vichwa vyetu. Ufike wakati tutafsiri nadharia kwa vitendo, hapo tutasonga mbele na si kupangua alama za ufaulu na sifa za kwenda Vyuo vikuu.

Tunapong'an'ania kuwa elimu bora ni kupata "A" tu kwenye karatasi ni kujidanganya kuwa tuna maarifa kumbe ni maarifa ya nadharia tuliyoyaacha kwenye karatasi. Ni nani asiyejua kuwa hizi "A" zinapatikana kwa kukesha tukisolve lundo la mitihani iliyopita? Hata huko vyuo vikuu watu wanahangaika kupata mitihani iliyopita wakibahatisha basi ni "As" na GPA za 4.5 hewa? Katika chuo kikuu kimoja hapa nchini vijana wanasoma Bsc. Physics mwaka wa kwanza hadi wa pili practical kubwa wanayofanya kila semister ni ya Cathode Ray Oscilloscope kustudy frequency za source za umeme kama DC generator, halafu hawa ndiyo watakuwa technologists kweli?

Natoa Rai kwa serikali hii kama kweli ina nia ya dhati katika kuboresha elimu isihangaike tu na madaraja na viwango vya ufaulu, bali twende kwenye elimu ya kutenda zaidi si ufaulu wa karatasi tu. Tunahitaji falsafa mpya ya elimu. Inawezekana je mtu anasoma mechanical engineering miaka minne lakini aingie workshop mwaka mmoja tu? Ni hayo tu, sikuwa na maana ya kukosoa elimu ya bwana mkubwa bali falsafa ya elimu tuliyong'ang'ania ya ufaulu wa makaratasi.
Elimu yetu ni ya kupatia ajira tu!
Hata Magufuli hajawahi kuimagine ktk big scale kuwa hicho alichokifanyia kazi kitawork au la!
Alifanya PhD wakati akiwa waziri, amekuwa raisi wala korosho hajawahi kuitaja, yeye amefall in love with barabara tu!
Of course sio yeye peke yake mwenye tatizo hili! Wengi wetu hatfanyii kazi taaluma tulizonazo, zinatusaidia kupata mshahara tu!
 
Hii ndio ile marehemu soda ya Mabibo?
Ilikuwa maarufu mwanzoni mwa miaka ya sabini?
Lakini mwalimu Wake si aliisha ifanyia utafiti thesis hii?
 
Exactly. Sio kila PhD inatoa machapisho, angalau tu ya kitaifa achia mbali ya kimataifa ambapo kuchapisha kwenye reputable journal mf science nako nasikia kuna politics kibao.
Haya ndio matatizo ya kukosa falsafa ya elimu ya juu. PHD holder maana yake ni bigwa katika uwanja mahsusi na kwa maana hiyo haina maana kama haisaidii kutatua tatizo mahsusi kwa jamii husika.

Haishangazi kukuta kijana wa miaka 30 hajawahi kuajiliwa na hata chuo kikuu chochote ana PhD. Kwa mtu kama huyu unategemea utapata machapisho mangapi? Watanzania tunashangaza sana.
 
Main objective inabaki kuwa ule ujuzi ulopata utumike in real life na uwe msaada kwako na kwa wengine(Society) katika kurahisisha na kufanikisha maisha.
Tofauti na hivyo that education becomes useless.
Mtoa mada yeye kaelezea vizuri kwa kuita huko ni kusoma kwa "title tuu" yani kuitwa Prof, Dr, blah, blaa
Ni kweli. Kuna watu wana hizo PhDs lakini hawana uwezo unaofanania mtu mwenye kiwango hicho cha elimu. Yuko mmoja alikuwa DIT, hawezi kufundisha, hawezi kusimamia project za wanafunzi na alikuwa mwalimu, sasa unajiuliza hii PhD yake inasaidia nini na ina maana gani?

Huyu sasa ni mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha. Katafuta ukuu wa chuo kwa njia ya lobbying kapata. Nenda kaangalie anachokifanya pale. Mitaala ina hatua zake mpaka ikamilike, yeye anatengeneza mitaala bila kukusanya maoni ya wadau. Wiki moja ilitosha kuhuisha mitaala ya idara zote zilizopo chuoni. Ladha ya kufanya mambo kitaalamu/kisomi haipo, na jambo lolote lisilo na maslahi ya moja kwa moja kwa mkuu halifanyiki.

Vitu vinavyofanyika na kutangazwa sana ni fabrications tu kama wanavyofanya wanafunzi wa kiwango cha VETA. Lakini elimu ya chuo hiki iko beyond VETA, ni degree level. Tunategemea mwanafunzi wa elimu ya Sayansi/Teknolojia wa level hii awe na maarifa mapana ya ubunifu, lakini mazingira hayajajengwa hivyo. Chuo hiki kilikuwa mahali tulivu kwa ajili ya kutoa taaluma bora lakini ghafla pamegeuka kuwa sehemu ya kero, maudhi, manyanyaso, upendeleo na aina mbalimbali zisizofaa. Katika mazingira ya aina hii taaluma haiwezi kumea na kuchanua inavyotakiwa.
 
Asante mkuu kwa challenge hii ya kisomi, hopefully wahusika wamesikia
 
Mngekuwa mnajua hizo phd zinapatikanaje hapo UDSM msinge mlaumu Dr Magufuli. Nyingi ni za kupewa au na kufanyiwa na watu sasa mwisho wasiku mhusika anaenda kuchukua phd bila hata kufanya tafiti directly hawezi kufanya publication yoyote kwa sababu anakuwa hana anachoelewa kwa undani juu ya phd anayo chukua
 
Hili ndilo tatizo la tafiti na hususan tasnifu zetu. Nyingi zilifanyika ili kutafutia hadhi na sio kutatua matatizo ya kijamii. Ingekuwa vema tukaanza na msomi kiongozi wa nchi aiweke mtandaoni PhD Thesis (Tasnifu) yake ili watu waone ni jinsi gani itaweza kutumika kutatua matatizo ya kijamii. Hili litakuwa fundisho kwa wengine wote wanaandika Tasnifu zao waziweke mtandaoni ili kila anaetaka kudadisi na kuitumia aipate kwa urahisi.
 
Back
Top Bottom