PhD mbili za Nchimbi Emmanuel ni halali? High level ya uchakachuaji Tanzania

Wadau mi nashuari tusiwe tunawahukumu watu kinadharia bila kufanya utafiti hata mdogo tu.

Nchimbi navyomfahamu ni mtu mwenye uwezo wa kutosha darasani tangu anasoma degree ya kwanza chuo kikuu mzumbe,akiwa waziri wa elimu wa serikali ya wanafunzi katika chuo cha idm wakati ule.


Na kwa kumbukumbu sahihi mh nchimbi kilichomfanya kupata umarufu mkubwa wakati akiwa mwanafuzi wa degree ya kwanza ni uwezo wake wa kuandika maandiko ya mapendekezo mabilimbali serikalini kuhusu kuboresha elimu na hali ya maisha ya wanafunzi wa elimu ya juu(wakati huo mh benjamini mkapa akiwa waaziri wa elimu ya juu).

Kwa maana hiyo nchimbi alionesha tangu mwanzo ni mtu wa kumudu elimu,siasa na hata mambo mengine ya kijamii kwa wakati mmoja.sizani kama anaweza kushindwa kusoma sasa tena phd ambayo ni kwa utafiti tu usioitaji kazi ya kirasiku.

Pia mdau usizani kwamba vyuo vyetu ndio hivyo sana na labda mtu akisoma ulaya ndio utaamini kwamba phd yake ni ya kiwango,hilo sio kweli kabisa naomba fanya utafini nini kimemkuta waziri wa fedha wa ujerumany hivi karibuni.

Kuna tatizo kubwa sana sasa nchini kwetu watu wengi wakiwemo waajiri kuzalau vyeti vya vyuo vya hapa tanzania na kuheshimu mtu akisema kasoma uk na kwingineko wakizani kusoma uk.


Naamini kabisa mh nchimbi amefuzu kwa viwango na sio upendeleo,na faida tu ya wasomaji mh nchimbi alikua na zaidi ya mawaziri 3 amambao nao wailijisajili kusomea phd kweye chuo hicho hicho na kwa mwaka huohuo,ila wenzine wanne hawakuweza kumaliza kwa wakati na hivyo hawakumaliza mwaka huu,kwahiyo sizani kama uwaziri ndio kigezo cha kupata.

Pia tukumbuke mh.karume(raisi mstaafu wa zanzibar) alisoma chuo huria cha tanzania(wakati akiwa rais).wote tunajua alichukua muda mrefu zaidi kumaliza,ingekuwa cheo ndio kigezo naamini ingemaliza haraka sana tu.

Watanzania tuwe na utamaduni wa kuunga mkono yale mazuri wenzetu wanayofanya,na hata tunapokosoa tuwe tunakosoa tukiwa na uhakika na tunayosema.

Tuweke utamaduni wa kujadili vitu vya maana zaidi katika jamii yetu na kuweka muda wa kutosha katika mambo hayo na sio mtu akipata mafanikio tunachukua muda mwingi sana kutafuta uzaifu wa kumchafua.

Nitakupa mfano,miaka michache sana iliopita baada ya kumaliza elimu ya chuo nilijiajiri kwa kufungu kampuni binafsi ya huduma za kitaalamu (consultancy),watu wengi walionizunguka na kunifahamu walichukua muda mwingi kujadili madhaifu yangu,wengine wakisema ni tapeli huyo,alikua hana akili chuo kikuu,hawezi kufika popote,hakuna aliechukua muda kujadili kuhusu nini hasa nachofanya na kampuni hii.

Leo napoongea nawewe kampuni hii ni mmoja ya kampuni zenye mafanikio makubwa sana,na walewale waliopoteza muda wakati ule kusema mabaya juu yangu sasa ndio wanakuja napongezi nyingi na kutaka niwape ushauri nimefanyaje kufanikiwa.

Sasa huu ndio utamaduni wa wengi wetu mtu akifanya kitu badala tujifunze kwake na kumpa moyo tunatafuta sababu za kujifariji kwa kumuonesha sio kitu wala chochote.tubadilike.
 
Hata ukiwa na PHD ngapi what matters ni can you deliver? Kuna watu wana phd kibao tu but what have they done with them. Unakuta mtu una Phd ya IT then unafanya supporting work,total wastage of taxpayers money kama ulisomeshwa na serikali. Go out of your way and solve pressings problem in the society. For me I will respect mtu anafanya positive contributin kwa society bila any degree than a professor who keeps on whining about the sorry state of his/her country!
 
Nahisi nchimbi anaandaliwa kuja kupewa uongozi flani na watu flani wabaya
 
Nahisi nchimbi anaandaliwa kuja kupewa uongozi flani na watu flani wabaya

Hayo ni mawazo ya kichawi. Umekuwa shekh Yahaya wewe? Mwenzio akifanikiwa unasema kaiba, akikosa unasema ulijua atashindwa. Aah watz bana, hadi mfe njaa ndo mtajifunza kuuona na kuutetea ukweli. Acha majungu
 
wakuu wa kazi, juzi mzumbe walikaririwa na vyombo vya habari wakimtunuka nchimbi phd. Ieleweke kuwa kwa muda mrefu huyu jamaa amekuwa akiitwa doctor kumbe hana phd. Kama hali imefikia hivi hatuoni kuwa Tanzania tumefika kubaya? Mtu anajiita dr wakati he doesnt have such qualification. Na hata kama mzumbe wamempa hii phd tuambiwe amesoma saa ngapi?

hiyo thesis imefanywa na nani kwa sababu ndi ngumu sana kubalance between masomo na siasa, especially being a minister. I am doubting universities zetu hizi, zinachangia kuzalisha wasomi feki. The top most three in fake phd are UDOM, UDSM and MZUMBE. Hii ni embarassment kwa jamii ya wasomi kutoa degree zisizofanyiwa kazi.

Hatuwezi kufika huko tunakotaka kama hali yetu ndiyo hii. maana tumefikia upumbavu wa hali ya juu kwa kujidanganya kuwa tuna wasomi kumbe sifa haziendani na kisomo cha mtu. Huu ni ufisadi wa aina ya pekee. Wanasiasa wanaweza kupata phd ki rahais hivi!

Question:
Can one get two PhD’s each in a different subject?

Answers on Google:
“If you have the energy and money, yes you can. You can pursue as many PhDs as you want in as many areas as you want. However, acquiring one PhD is a major achievement in itself. List your priorities and take one step at a time. Best wishes!!”

“For those students who fall in love with academia before they necessarily fall in love with a particular field, this might be an option for eventually getting to the outcome they desire. I'm not saying it's wise or appropriate. But it is something to consider for those who know for certain that they want to do research, service, and teaching at a university setting. It is probably true that there are many history professors out there who would rather be English professors than a whole other third career, and would have gone the distance to ensure they got to the academy, no matter what particularly department that would be in.”

“There's no question that you don't need to have two PhD's to do interdisciplinary research - psychology professors have contributed to the work of marketing professors for years, for example. But if you had an area that really did require boatloads of knowledge and multiple methodologies, you'd be hard-pressed to find a better preparation to do relevant, life-changing, compelling research. There must be some double-doctorates out there who could honestly say they call upon both PhD's to do their work, are happy they went around twice (with coursework and exams, at least).”
 
Hata ukiwa na PHD ngapi what matters ni can you deliver? Kuna watu wana phd kibao tu but what have they done with them. Unakuta mtu una Phd ya IT then unafanya supporting work,total wastage of taxpayers money kama ulisomeshwa na serikali. Go out of your way and solve pressings problem in the society. For me I will respect mtu anafanya positive contributin kwa society bila any degree than a professor who keeps on whining about the sorry state of his/her country!

Mkuu siku watu wakiacha kulea makaratasi wakaanza production tutafika mbali..
 
Hivi watu mmekosa kazi kila siku ni kuropoka tu, UDOM hawajatoa phd hata moja we umeanza kuita feki, UDSM haya twambie ufeki wao uko wapi? Na wewe umepata wapi uwezo wa kutambua phd feki na genuin?
Vijana mbona mmejiingiza kwenye majungu ambayo hayatawasaidia? Nchimbi wewe huwezi kushindana nae phd kashapewa unapoteza muda wako na ela yako kuandika pumba humu.
Vijana chapeni kazi acha majungu
Wenzako wanaongelea elimu wewe unaongelea siasa sijui kama mtaelewana.
 
inategemea phd ya kwanza kaipataje kwani kuna nchi ukishapublish paper kama 3 na una level ya mastesr wanakutunuku phd
labda alipublish hatuwezi jua, kwa hii alopata juzi inategemea alifanya phd ya kitu gani, kwa thesis sio lazima kuwa chuo unafanya popote ulipo unakuwa na mawasiliano na supervisor,kwani Magufulu aliingia darasani phd pale mlimani?
 
Nachukua nafasi hii kumpongeza DR. EMANUEL NCHIMBI kwa kufanikiwa kupata shahada ya Udaktari wa Falsafa.
Nampongeza kwa sababu kuu mbili:
1. Kukubali kuwa shahada yake ya kwanza ilikuwa kanyaboya, na kuwa tayari kusahihisha.
2. Kuonyesha kwa vitendo kuwa kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa uhunzi. Ameweza kujiandikisha tena nyumbani kwenye vyuo vilivyopitishwa na baraza la vyuo vikuu Tanzania na kujibidisha hadi kumaliza shahada yake.

Japo mie sio mpenzi wa siasa zao, lakini pale mtu anapofikia mafanikio fulani, mpeni sifa zake, na kwa hizi Dr Nchimbi anastahili. Nafahamu kuwa hata aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki "Kamara" nae yupo masomoni, na mida simingi pia atatunukiwa. Hawa Wazee vijana wanapaswa kupongezwa kwa kukubali kutupa kasa walizokuwa wamemeza.
 
Mtoa hoja ana mtazamo wa jumla sana inaonekana tatizo ninnchimbi kuwa mwanasiasa,mbona magufuli aliweza kumaliza Phd na tukashangilia na kumsifia?kama Nchimbi ameweza kubalance majukumu na kukamilisha Thesis yake anastahili kupongezwa na sio kubezwa tatizo wa Tz wengi kutwa kucha porojo tu na umbea watu wanapiga shule wakihitimu mnasena shahada feke present basi yako real tuione kama mfano,we talk much than what we act wake TZ
Kaka tatizo sio phd yake, ila ni kwanini alikuwa akijiita dr wakati alikuwa haja qualify? Au yeye ni dr, dr nchimbi?
 
Kumbuka kwamba ili mtu apate phd ni sharti atetee (to defend) thesis yake. Ni wazi kwamba endapo atakuwa ameandikiwa hiyo thesis hataweza kuidefend, hata kama akipewa coaching namna gani. Wala mimi sioni suala la ufisadi hapa. Inawezekana kabisa kuwa ile phd ya kwanza ilikuwa feki, lakini hii ya Mzumbe ni halali. Jamani hebu tuwe na confidence na vyuo vyetu.
 
Hivi watu mmekosa kazi kila siku ni kuropoka tu, UDOM hawajatoa phd hata moja we umeanza kuita feki, UDSM haya twambie ufeki wao uko wapi? Na wewe umepata wapi uwezo wa kutambua phd feki na genuin?
Vijana mbona mmejiingiza kwenye majungu ambayo hayatawasaidia? Nchimbi wewe huwezi kushindana nae phd kashapewa unapoteza muda wako na ela yako kuandika pumba humu.
Vijana chapeni kazi acha majungu
Jk alipewa unesi na udom?
 
Na isitoshe, PhD examiners care less on how much or how less your research will change the world - key things that they look for are:

1. The research must be original meaning it has to involve fresh/new enquiries/empirical data collected from the field;

2. The research should develop after a critical examination of the current state of knowledge in the subject area; in the process, the researcher should demonstrate that there are some research gaps that he/she has identified; for instance, Nchimbi's research was based on Credit Challenges to Micro and Small Entrepreneurs; as long as he pursued his research by reviewing the literature that was available prior to his research and examined it critically and demonstrated that to the examiners, expose the identified gaps in the current research i.e. detected issues what other studies prior to his, haven't looked at, and consequently tackle them accordingly, his research should be a good pass; and this is where the issue of original contribution to research comes in; you should be able to demonstrate how your research contributes to the current state of knowledge;

3. Also, during defense, examiners seek to determine whether the scholar has gained an understanding that Research is something that an individual undertake in order to find out things in a ‘systematic way', thereby increase his/her knowledge; also that - research involves describing, explaining, understanding, criticizing and analyzing data; importantly, your research should be based on logical relationships and not just personal beliefs;

Pia what is more important than the title of your research, your research design or strategy is the validity of the study itself. That is to say, whether the research method (s) devised really assesses what it is intended to assess; Also of equal importance are ethical issues in the data collection phase e.g. privacy of research subject/participants, respect….and that they were not forced to provide the researcher with data but instead collaborated based on a mutual understanding and agreement;
We have many exemplary Professors at Mzumbe, UDSM, SAUT and other places (Tanzanians) who can enable a serious scholar perform based on the above; Hongera Dr. Nchimbi;

Lastly, Mwalimu Nyereer hakutuacha bila kulizingumzia hili:
"Kujielimisha siyo maana yake kwenda shuleni; Kama ingekuwa ndivyo, TANU ingekuwa imefanya kosa kubwa sana kutamka kila mwanachama ajitahidi kujielimisha na kutumia elimu yake kwa ajili ya wote; Kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo; kwenda shule hutusaidia;"

Pia Mwalimu anazidi kusema:

"Tunayo haki ya kutazamia matunda kutoka kwa wale waliohitimu katika chuo kikuu, na wengine waliopata elimu ya juu ya aina yoyote; hatuna matumaini matupu, tunatazamia kuvuna; tunadai huduma kwa wananchi, na huduma ambayo ukubwa wake utalingana na kiasi cha elimu mtu aliyopata;"

"Ni dhahiri kwamba mtu anaweza kuitumia elimu aliyoipata shuleni au katika chuo kwa faida yake mwenyewe binafsi, na faida nyingine kwa wananchi zikapatikana kwa bahati tu; Na kwa kweli wakati mwingine inaonekana kwamba utaratibu wa nchi zetu ndivyo ulivyo, kwa sababu vishawishi vya mishahara ya juu vimewekwa kwa zile kazi ambazo hazina faida kubwa kwa wananchi kwa ujumla; Lakini hata katika zile kazi za kuwahudumia sana wananchi, mara nyingi watu wenye elimu au utaalamu wanaweza kutumia vibaya dhamana yao, wakipenda;"

Dr. Nchimbi anaongoza Wizara muhimu ya Maendeleo ya Vijana, Kwahiyo hii ndio nafasi yake ya kuonyesha mfano katika kujenga taifa based on ujumbe wa Mwalimu.
 
Nampongeza nchimbi kujipatia phd ya ukweli sasa. Wenzake 8 wanasota out kuzitafuta. Kumbe kweli tunaongozwa na waongo
 
Elimu ni nzuri na wote lazima tuitafute. Kujaza vyeti na kutumia mgambo kupiga na kupora machinga ni ujinga ulioenda shule. ng'ombe1000 nyumba ya nyasi. Godoro ngozi.
 
Back
Top Bottom