kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,005
Napendekeza uwepo utaratibu wa kutoa mitihani kila mwaka kabla ya kutoa leseni kwa wafamasia ngazi zote sababu ni kuwa;Wengi hawajisomei na wanaonekana kuwa incompetent sana wanapokuwa kazini.Wengine wanajisahau na kuwa walevi kila siku.Lengo la kufanya hivi ni kuhakikisha ufanisi wa wafamasia wote wenye leseni.
Pili,wekeni utaratibu wa kuwa na orodha ya watu wa kada ya ufamasia wasiofanya kazi ya ufamasia eidha kwa kukosa ajira ama kutokuwa na interest.Sababu ni kuwa kuna wahitimu wa kozi za nacte wanahangaika kutafuta kazi huku ukweli kazi wanazostahili kuzifanya zinafanywa na watu wasio na elimu hata kidogo ya afya.Mifano ipo mingi na hata leo ukitaka kujua pita katika pharmacy nyingi utashangaa.Naamini mnajua labda mnafumbia macho tu.
Imarisheni mijadala ya kifani kupitia mitandao na majarida mbali mbali,ongezeni network na wafamasia wa nje kama wanavyofanya wauguzi,kuna mengi sana ya kubadilishana uzoefu lakini pia tafiti na machapisho mbali mbali.Naona wazee wa zamani walijitahidi sana kufanya hivyo.Leo hata wafamasia wetu hawana mahali pa ku practice utengenezaji wa vitu kama iv fluids,dawa za macho nk.Tumsaidie Rais kuifanya nchi hii ya viwanda
Mwisho kaimuni madaraka kwa mamlaka za halmashauri ikiwa ni pamoja na wenyeviti wa mitaa kuhakikisha watu wasio na sifa hawauzi dawa kwani kuna matatizo makubwa sana katika suala hili japo linafumbiwa macho