Kubadilika vigezo vya kozi za Diploma ya pharmacy ni hatua nzuri lakini..!

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,364
4,065
Nimepata taarifa isiyo rasmi kuwa vigezo vya kijiunga na diploma ya pharmacy vimebadilika kutoka D za kemia na biolojia hadi D 5 zikiwemo fizikia,hisabati na English.
Nawapongeza kwa mabadiko hayo lakini hayawezi kuwa na tija yoyote.

Ukifanya utafiti mdogo utagundua kuwa sababu kubwa ya kufanya hivi ni kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kufeli mitihani yao.Walioongeza vigezo walidhani,(maana hawana takwimu za kuamua hivyo) kuwa kufeli kwa wanafunzi ni kwa vile hawakufaulu fizikia na hesabu!

Hata hivyo kwa hisia hizo hizo ( za ndaani kabisa),uamuzi huu umefanywa kutokana na chuki ya wafamasia wengi,dhidi ya wamiliki wa vyuo vya pharmacy, kudahili wanafunzi wengi kupita kiasi,hata kupelekea washindwe kutoa mafunzo kwa ufanisi,na kuvitumia vyuo vya pharmacy kama vyanzo vya mapato yenye faida kubwa,huku wakifaidika na mfumo wa rushwa unaovipa vyuo fursa ya kucheza na elimu.

Macho yangu yanaona jinsi vyuo vitavyofilisika na kuwafuta kazi wafamasia ambao wengi kimbilio lilikuwa katika vyuo hivi.

Pamoja na haya yote,bado katika tasnia hii ya famasi,bado inahudumiwa na watu wengi wasio na elimu ya taaluma ya famasi.Katika maduka mengi ya dawa,utakuta vijana wahuni tu wakiuza dawa na mfamasia katundika cheti tu.Wakati wa ukaguzi wanajiita wahasibu,wengine mameneja n.k ingawa ni ajabu fundi bomba kuwa meneja wa duka la dawa.

Ni ndoto za uongo kudhani kuna tofauti sana kati ya F na D ya hisabati,tofauti ambayo inatarajiwa kuboresha matokeo.
Uchache wa wanafunzi tu ndio utaleta tofauti na vigezo hivyo
 
Una hoja nzuri lakini hujaipanga vizuri, ulipaswa kuleta taarifa badala ya kuonekana unalalamika
Asante kuna watakaotoa taarifa wataandika vizuri,mimi sina taarifa rasmi kwani nimeingia tovuti ya NACTVET sijaona kitu
 
Kwa maelezo yako tayari umeshaonesha tija ya mabadiliko hayo, na bado ukasema huoni tija!
 
Back
Top Bottom