Petition: Wito wa kusitisha tozo/kodi ya laini ya simu kila mwezi kufuatia mabadiliko ya sheria

Hivi serikali ina sera ya utozaji kodi?Sioni kama vigezo na masharti vimezingatiwa hapo.Naona kukurupuka tu tena kwa hali ya juu.So sad indeed
 
"Ili kupata maoni ya katiba mpya yatakayopelekea CCM na viongozi wake kupona hebu tafuta njia ya kuweza kuwaweka busy wananchi wa Tanzania kwa kujadili huku maoni ya CCM yakipita kwenye katiba". Watanzania zindukeni katiba ndo mkombozi wa yote haya!
 
,Ahsante Bandit tumsaidie huyo sangarara tafadhali.
Mkuu si unajua nchi hii watu ni mabingwa wa kukariri?....Nchi ina kila kitu hii...dhahabu,tanzanite,mito maziwa,ukanda wa pwani zaidi ya km1400 bado serikali inakamua watu vikodi vya ajabu ajabu huku matajiri wakipewa tax holiday!
 
serikali ya ccm ni ya ajabu sana,lile kampuni la gesi limekiri kukwepa kodi kwenda kuchukua inashindwa,kwanini isinunue mtambo ule wa kama nchi nyingine ili kampuni zilipe kodi sahihi,kwenye madini hakuna kitu,bahari kuu hakuna kitu,mwl serikali ya wala rushwa haikusanyi kodi hata ikikusanya itakusanya kwa watu wadogo
 
Kodi ni lazima, serikali haiwezi kuendeshwa bila sisi wananchi kulipia kodi, ili serikali hii ieweze kutekeleza majukumu yake na hasa kutimiza ahadi za mheshimiwa rais wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 ni lazima wananchi tulipe kodi labda kama ulidhani alimaanisha kuleta neema zote zile kwa pesa kutoka mfukoni mwake.

by the way wewe unataka ubaki na hiyo elfu moja ya nini? watu milioni moja tukitoa hiyo buku buku kwa mwezi mmoja tu inapatikana bilioni moja, do you know what this Government can do with one billion?

TULIPE KODI KWA MAENDELEO YA TAIFA.

YES!
Buy more gas guzzling Japanese and BMW monsters,Increase unproductive foreign travels with unnecessarily large delegations,buy more anti riot vehicles and gear,pay for clandestine operations to frame CHADEMA national leadership,Placate the army so they can continue to suppress and oppress the poor walalahoi in Mtwara and Lindi,stash some of it to pay for the biggest election fraud come 2015,Misappropriate half of it,OR BETTER YET.......SPENT IT ALL AND THEN SOME ON OBAMA VISIT!

Just a thought..............
 
Acha ubinafsi,tunaongelea uwezo wa watanzania walio wengi,kama elfu moja kwa mwezi kwako ni ndogo,kwa wengine ni kubwa,Hakika nina mashaka na wewe,usowafikiria wengine?Hakuna asiyetaka kulipa kodi hapa,mbona kodi nyingi wananchi tunalipa?ni maendeleo yapi yaliyofikiwa mpaka sasa? kinachosikitisha ni pale kodi inakusanywa kutoka kwa wanyonge tu,lakini makampuni ya kigeni yanafumbiwa macho.Usituharibie mood kaa kimya wewe uliye tajiri acha sisi masikini tuzungumze juu ya hili.
Mimi ni masikini kama wewe, usifikiri niko safi hata kidogo, hapa nina shida kibao, lakini hizi bado sio sababu za kukataa kulipa kodi. kukataa kulipa kodi ni kupanda kuidhoofisha serikali na kusababisha mafisadi waiweke mifukoni mwao, kama kweli tunakiri hii ni serikali yetu, basi tulipe kodi kuiimarisha zaidi.
 
Nani anakataa kulipa kodi? Watu wanapigania kupata huduma ya simu kwa wasio na uwezo, Kama hiyo kodi imewekwa kwenye huduma muhimu ili kunyima watu HAKI ya kupata huduma hapo kuna usahihi gani wa Kuwa na kodi ya hivyo
 
watu wanaweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja wacha kuogopa

"Ili kupata maoni ya katiba mpya yatakayopelekea CCM na viongozi wake kupona hebu tafuta njia ya kuweza kuwaweka busy wananchi wa Tanzania kwa kujadili huku maoni ya CCM yakipita kwenye katiba". Watanzania zindukeni katiba ndo mkombozi wa yote haya!
 
Watanzania tujenge tabia ya kulipa kodi.

Mkienda huko nje ya nchi kwa wenzenu walio serious na maendeleo mnajikuta mnafanya kazi usiku na mchana kazi tatu tatu ili muweze kumudu gharama ikiwemo hii ya kulipa kodi
. Mimi nataka kodi iwe chachu ya kufanya watanzania wafanye kazi usiku na mchana bila kulala.

Haiwezekani kodi wanazolipa wananchi wa huko Japan, Marekani, Canada, Sweden n.k ndio zije hapa tuweke kwenye bajeti yetu tutakuwa omba omba hadi lini?

Naomba serikali iongoze hii kodi kutoka Sh 1000 angalau iwe 1500.

heheheheh naona umeaanza kuropoka, hizo nchi za nje unazoengelea ni zipi? karibu nchi zote za ulaya zinawalipa watu wasio na kazi , wazee, watoto na walemavu pia kufanya kazi, hizo nchi alipoli hela kwa masikini tax system zao zinalinga masikini na wasio na kipato, uzuri ni kwamba hakuna hizo kodi za namba za simu maana tayari kuna VAT kwenye matumizi ya simu
 
Kodi ni lazima, serikali haiwezi kuendeshwa bila sisi wananchi kulipia kodi, ili serikali hii ieweze kutekeleza majukumu yake na hasa kutimiza ahadi za mheshimiwa rais wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 ni lazima wananchi tulipe kodi labda kama ulidhani alimaanisha kuleta neema zote zile kwa pesa kutoka mfukoni mwake.

by the way wewe unataka ubaki na hiyo elfu moja ya nini? watu milioni moja tukitoa hiyo buku buku kwa mwezi mmoja tu inapatikana bilioni moja, do you know what this Government can do with one billion?

TULIPE KODI KWA MAENDELEO YA TAIFA.

me najua gvt yetu hii watagawana wengine wataficha uswisi, wengine kuhonga, watajenga mahekalu masak mbez bich etc etc
 
PETITIONS.JPG
 
Wakuu,

Naona tunatumia muda mwingi kusign hizi petition ambazo hazina athari zinazotakiwa. Nilipokuwa masomoni Marekani, nilifundishwa mbinu moja nzuri ya uanaharakati, lakini nawamegeeni hizi mbili, muweze kuzitumia kufanikisha lengo kuu.

  1. Hit your enemy where it hurts the most: his pockets! Tafsiri yake ni kwamba "Mpige adui yako mahali ambapo ataumia zaidi: kwenye mifuko yake." Tafsiri fupi ni kwamba, kama ana mapato, tafuta njia ya kumnyima mapato, kumtia hasara kubwa, ikiwezekana, mfilisi kabisa. Kwa hili tufanyeje? Badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari na kusign petition, tunachopaswa kufanya ni kuendesha mgomo baridi wa hata saa 24, kwa kuzima simu zetu za mkononi. Matumizi ya simu hizi, kisheria, na kibiashara, ni kwamba, mteja anaponunua line ya simu (SIM card) na kupewa namba ya simu ya mtandao wowote ule, anakuwa na hiari ya kutumia au kutotumia simu yake hiyo, na wala hapangiwi kiasi cha fedha anachopaswa kutumia. Kutumia aku kutotumia ni hiari yake; halazimishwi. Hebu fikirieni, iwapo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, tena wale ambao wana kipato cha chini ambao ndio wenye matumizi makubwa zaidi, kwani mapato ya hizi kampuni za simu hupatikana zaidi kwenye SMS, na watumiaji hawa ni wengi zaidi kuliko matajiri, waamue kusitisha kutumia simu zao kwa saa 24 hadi 48, hasara watakayoipata wamiliki wa kampuni za simu itakuwa kubwa namna gani? Kampuni hizi zimeingia ubia haramu na Serikali yetu wa kuwanyonya Watanzania ambao wengi wao tayari ni maskini, ambao wengi wao kipato chao hakitoshi hata mlo mmoja wa siku. Ni ajabu walidunduliza MIAKA NGAPI hadi kupata uwezo wa kununua hizo simu zao za mkononi, kisha kununua line, na leo Serikali inakuja na kodi ya kinyemela kuwatoza Shs. 1,000 kwa mwezi? Dharau iliyoje? Basi na sisi (najua nitaitwa mchochezi lakini hizi ni harakati) tuwagomee huduma yao hii, kwa hizo saa 24 hadi 48. Najua wataleta vitisho kwamba kila atakayezima simu yake atafungiwa line yake hiyo, lakini hizo zitakuwa ni nguvu ya soda, kwani hakuna kampuni ya simu hata moja ya kuifungia line yoyote ile iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria, EPOCA, kwani sasa line hiyo ni chanzo cha mapato kwa Serikali. Kampuni hizo haziwezi kukiuka mkataba wake na Serikali; tuzitie adabu, tuzitie hasara. Adabu isipotosha, mgomo huo (boycott) unarudiwa, mpaka Serikali na wabia wake haramu washike adabu, na waiondoe kodi hiyo haramu. Kwani wamiliki halali wa nchi hii ni nani kama sio sisi Watanzania, tena wanyonge, masikini, tulio wengi? Kwani viongozi wetu wanaolilia kututawala huja kuomba kura kwa nani wakati wa uchaguzi, kama sio kwetu sisi, ambao ndio tunaowapa dhamana hiyo ya kutwaa madaraka? Sasa cha kuogopa ni nini? Tukijipanga vizuri, tutafanikiwa. Hakuna kuogopa, zama hizo zimepitwa na wakati. Hata hivyo, kususia kutumia huduma hii ya simu SIO KOSA LA JINAI! NI HIARI! Tujipange! Inawezekana!
  2. Put his dirty laundry out in the open! Tafsiri ya mbinu hii ya pili ni "Anika nguo zake chafu hadharani!" Tafsiri fupi ni "anika siri zake za uhalifu/ufisadi hadharani". Kwa lugha ya Kiingereza, "dirty laundry" ina maana ya "uhalifu/ufisadi". Tukubali ukweli. Hakuna asiye na siri. Kampuni hizi za mawasiliano ya mkononi zimekuwa zikiwaibia (pasi na kuwa na ushahidi wa jinsi wanavyoibiwa) wateja wake kuwa miaka lukuki. Waajiriwa kwenye kampuni hizo, ambao ni Watanzania wenzetu, wamekuwa (kutokana na njaa zao) wakirubuniwa kushiriki kwenye wizi huu, pasi na kujua kwamba huu ni unyonyaji mkubwa kwa Watanzania, wengi wao ambao ni maskini. Watanzania wengi wamekuwa wakilalamika jinsi pesa zao zinavyokatwa kinyemela pasi na kuwa na maelezo kwa sababu gani mambo haya yanafanyika. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watendaji katika vyombo husika vya kusimamia sheria husika nao wameingizwa mtegoni, kwa kupewa ruzuku lukuki (bahasha za khaki), ambapo, kwa mfano, wanaposafiri nje ya nchi, hupangiwa masurufu makubwa ambayo kampuni hizi huhesabu kuwa "gharama ya uendeshaji kampuni ya ziada", au "overhead"/ Hapa tunahitaji kuwabembeleza Watanzania wenzetu wanaofanya kazi kwenye kampuni hizi kuwa wazalendo zaidi, na kutufunulia uchafu wote unaofanywa na kampuni hizi, kama ilivyofanyika kwa kampuni ambayo imekuwa ikiliibia taifa kwenye mapato ya matumizi ya umeme kwenye minara yake ya kurushia mawimbi, zaidi ya 1,700, na kusababisha hasara ya zaidi ya Bilioni 119 KWA MWEZI! Sasa harakati na ziendelee. Tuanike nguo zao chafu hadharani, kila mtu azione: Tuifanye thamani ya kampuni zao iwe ndogo kabisa, kiasi kwamba wezi hawa washitakiwe kwa mujibu wa sheria, ikishindikana, wauze kampuni zao kwa wafanyabiashara wengine ambao wataogopa kutuibia, kwani watatambua kwamba, kwanza, wamenunua kampuni hizo kwa bei ya "kutupa", lakini pili, watatuheshimu Watanzania na kuogopa kurudia makosa ya wenzao.

Mbinu hizi mbili zinatosha. Acheni kuhangaika na hizo petition. Hazisaidii chochote. Mkitaka ushauri wa jinsi ya kuratibu harakati hizi, nitawapa, lakini msiniPM. Sitapokea PM ya mtu yeyote kuhusu hili, kwani najua miongoni mwetu humu wamo mandumilakuwili wengi tu. Siko tayari kumwamini mtu yeyote nisiyemjua kuhusu hili. Nitaweka mambo hadharani.

Kila la heri.

A luta continua!
 
heheheheh naona umeaanza kuropoka, hizo nchi za nje unazoengelea ni zipi? karibu nchi zote za ulaya zinawalipa watu wasio na kazi , wazee, watoto na walemavu pia kufanya kazi, hizo nchi alipoli hela kwa masikini tax system zao zinalinga masikini na wasio na kipato, uzuri ni kwamba hakuna hizo kodi za namba za simu maana tayari kuna VAT kwenye matumizi ya simu

Unafikiri hizo pesa wanazolipwa watu wasio na kazi zinatoka wapi?

Watu wanaofanya kazi wanakamuliwa vya kutosha ili wasio na ajira wapate chochote kitu.

Watanzania tuachane na ndoto maendeleo hayaji bila wananchi kujifunga mikanda.

Mimi nadhani sisi ambao tunatumia sh 15,000 kwa mwezi au zaidi kwenye simu ilibidi tulipe zaidi.

Kodi kubwa ndio chachu ya wananchi kujipatia kipato tuache utegemezi tulipe kodi kwa maendeleo ya Taifa.
 
Nimesikia Mnyika anatafuta signatures za wananchi sasa nimeshangaa sana.

Wananchi wanaotumia simu wapo zaidi ya milioni 10 nina hakika huyu bwana mdogo hawezi kupata hata signature milioni moja.
 
Unafikiri hizo pesa wanazolipwa watu wasio na kazi zinatoka wapi?

Watu wanaofanya kazi wanakamuliwa vya kutosha ili wasio na ajira wapate chochote kitu.

Watanzania tuachane na ndoto maendeleo hayaji bila wananchi kujifunga mikanda.

Mimi nadhani sisi ambao tunatumia sh 15,000 kwa mwezi au zaidi kwenye simu ilibidi tulipe zaidi.

Kodi kubwa ndio chachu ya wananchi kujipatia kipato tuache utegemezi tulipe kodi kwa maendeleo ya Taifa.

Kwa hiyo unataka kusema wanalipwa kisha nao wanalipa laini za simu za mkononi ! Hiyo kodi haipo , nchi zilizoendelea hazitozi kodi zaidi ya VAT kwenye huduma Kama mawasiliano , kwenye hizi simu mpaka sasa watu wote tunalipa VAT, sasa wamwleta ya Internet 14% na hii ya sh 1000 kwa mwezi, hizo kodi zote kwenye huduma moja za nini? Wangejaza kodi nyingi hivi kwenye migodi ya Madini na makampuni ya uwindaji tusingekuwa mbali, pia na wao wahache kuiba hela ya kodi
 
Pamoja na hayo petition ni way forward na inatumika dunia nzima , wewe katie saini hayo mengi subiria matokeo

Back
Top Bottom