**~** penzi la clara **~**

Asante mkuu,
lakini mimi nilikuwa nazungumzia kuanzia mstari wa kwanza unapoanzia
ilianza hivi,

Nilihisi kuna mtu amesimama karibu na kochi nililokuwa nimejilaza. Ni ile hisia ambapo bila kuangalia nyuma unahisi kuna mtu anakunyemelea au kuna mtu anakuangalia na unapogeuka unakuta ni kweli. Nilikuwa nimejilaza chali kwenye kochi kubwa la rangi nyeusi huku Radhiya akiwa bado amekaa juu yangu. Shanga zake zikiwa zinaning’inia na kugusa kiuno changu. Kiunoni mwake alikuwa amejifunga kanga tu, tulikuwa tumeloa jasho, miili imechoka huku usingizi ukitupitia taratibu. Ilikuwa ni mara ya pili ndani ya saa moja tulifanya mapenzi ya nguvu.

Hisia hiyo ya mtu kuwa karibu ilinishtua mimi na kabla sijafanya lolote Radhiya naye alishtuka pia. Tulipofumbua macho yetu tulipigwa na butwaa la mwaka. Mke wangu Husna, alikuwa amesimama pembeni ya kochi tulilokuwa tumejilaza. Mkononi alikuwa ameshika kisu kikubwa chenye ncha kali kilichokuwa kinameremeta. Alikuwa amekunja uso wake, huku machozi yakimtoka na midomo ikimtetemeka. Kabla sijapata nafasi ya kusema Radhiya alijiondoa kwa nguvu na kuruka pembeni huku akishikilia kanga iliyokuwa ikimning’inia. Hakufanya ajizi alinyakuwa mkoba wake uliokuwa mezani na funguo za gari lake na kukimbilia mlangoni huku akijaribu kujisitiri na kanga yake. Alitoweka

Hapa inaonyesha msaliti wa ndoa ndio alianza kusimulia kisa na mwanamama akamalizia mkasa.
 
kwakweli malizia mkuu ni tamu nampenda clara sana yani umenigusa na clara malizia pls
 
Hizi hadith huwa tunatumia kwenye mahubiri... sometimes...

GS unatangaza nia lini tukuunge mkono au hili pambo?

Mgombea Ubunge Mtarajiwa(CHADEMA)-Niunge Mkono

Mkuu Askofu..Hilo sio pambo ni kweli kabisa..Nia nimeshatangaza kuweka tu hiyo signature hapo maana yake ni kutangaza nia..Najua umemaanisha uliposema kuniunga mkono..NitakuPM for more information na mawasiliano zaidi ili kujua ni jinsi gani tunaweza kusaidiana..Thank You for Your Consern..Really appreciated!
 
Thank you MMKJJ. I enjoyed the first chapter of your story. Why not get published?
 
....Hii hadithi mbona kimyaaaaa? Nachungulia kila siku sioni mwendelezo!! MMKJ kulikoni au majukumu yamezidi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom