Pengo: Polisi wanafuga wahalifu

Polisi wameshindwa kazi, wana maslahi binafsi. Kauawa kamanda Liberatus Barlow wakawapata wauaji. Kauawa padre, wanatuchorea katuni na wanasema ati kukiona mtu anafanana na katuni hiyo tuwajulishe.
 
Walipouliwa wananchi wa kawaida Makanisa, Misikiti na Watu muhimu katika jamii hawakuona kama ni jambo la kukemea, imewasogelea.... nikakumbuka haya <b><span style="font-family: Verdana"><font size="3"><font color="#000000">'Firstthey came for the Jews, I did not speak out because I was not a Jew. They camefor the communist, I did not speak out because I was not a communist. They camefor the trade unionists, I did not speak out because I was not a tradeunionist, when they came for me, no one was left to speak out (Martin Niemoller1984-1984, cited in the Raia Mwema of July 4-10, 2012 no 246 pg 11, by JohnsonMbwambo)'</font></font></span></b>
<br />
<br />
Bredda unakaa pande zipi,kama shimon sikulaumu coz huna access ya habari na kama upo sehemu ambayo update za habari ni 24hrs basi wewe unatakaga ligi tu.,ivi kuna matukio makubwa ambayo hayagusi iman za watu maaskof hawajakemea,wameshatoa machapisho kibao kuhusu mwenendo wa nchi kabla hata haya matukio ya udin hayajaanza..acha ligi tafuta habari,ishughulishe akil yako..
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuelezwa hatua zilizochukuliwa kwa watuhumiwa waliohusika na matukio ya kudhuru viongozi wa kidini visiwani Zanzibar.

Kauli ya Pengo inakuja huku mapadre wawili wa Kanisa Katoliki wakiwa wameshambuliwa kwa risasi pamoja na Katibu wa Mufti wa Zanzibar naye akimwagiwa tindikali usoni na watu wasiofahamika.

Katibu huyo wa mufti alimwagiwa tindikali hiyo Novemba mwaka jana, huku Padre Ambrose Mkenda akijeruhiwa kwa risasi Desemba 26 mwaka huo, na mapema mwaka huu, Padre Evarist Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi.

Pamoja na Jeshi la Polisi nchini kuunda kikosi maalumu kuchunguza matukio hayo, hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu uchunguzi huo jambo ambalo linamtia shaka Kardinali Pengo kutokana na ukimya huo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa salamu za Pasaka, Kardinali Pengo alisema kuwa kuchoma makanisa, kubomoa na kuharibu nyumba za ibada ni hali isiyoridhisha.

“Tumeishi Waislamu na Wakristo kwa muda mrefu bila kukwazana wala kugombana, napatwa na wasiwasi ikiwa hali hii imeanza kujitokeza sasa na watu wanadai ni kundi la wahuni, serikali haiwezi ikaepa majukumu yake,” alisema.

Aliongeza kuwa ama wawe wahuni au watu wengine, serikali haiwezi kutawaliwa na wahuni.

Alisema kuwa wanahitaji kukutana na viongozi wa pande zote mbili ikiwemo serikali ili kupata ufumbuzi wa yaliyotokea.

“Serikali haiwezi kukaa pembeni, pale tutakapokutana tunahitaji mawasiliano na majadiliano. Wanaofanya vitendo hivyo hawana jeshi, sasa ni muhimu kukutana wote na lazima watu wawe tayari kupokea ukweli na kusema ukweli, lakini pia kila upande uwe na mawazo kuwa upande wa pili una nia njema, amani haiji kwa mapambano wala mtutu wa bunduki,” alisema.

Kardinali Pengo alisema kuwa serikali ina jukumu la kulinda amani na kuchukulia hatua mazungumzo yoyote yanayotolewa hasa yakiwa ya vitisho.

Kuhusu madai ya baadhi ya watu kupokea ujumbe wa vitisho kuhusiana na ibada ya Pasaka, alisema: “Sitaacha kwenda kanisani kama kufa nife nikiwa kanisani hiyo ni juu ya serikali.”

Polisi wanasema wale wanaochoma makanisa ni wahuni, OK ni wahuni kwa kuwa polisi inawafahamu.
 
PENGO aache kukurupuka! kukamata waalifu sio kazi yake! ni kazi ya polisi ambao wanautaratibu wao! lakini pia mbona hazungumzii watu wengine waliouwawa yeye anang'ang'ania Padri Mushi ambaye inahusishwa na biashara haramu.
 

ALHAMISI, MACHI 28, 2013 04:52 CHRISTINA GAULUHANGA NA WINIFRIDA RWEGASIRA, DAR ES SALAAM


*Adai wameshindwa kutoa taarifa za mauaji ya Padri Mushi
*Ataka viongozi wa dini, Serikali wakutane haraka


KANISA Katoliki nchini, limesema limesikitishwa na usiri unaofanywa na Jeshi la Polisi kushughulikia matatizo mazito, yakiwamo mauaji ya Padri Evarist Mushi aliyepigwa risasi na watu wasiofahamika kisiwani Zanzibar, Februari mwaka huu.Mbali ya mauaji hayo, kanisa hilo pia limesema linasikitishwa kuona tangu kujeruhiwa Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki Mpendae, hakuna chombo cha dola kilichotoa majibu ya kuridhisha dhidi ya upelelezi unaofanywa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, alisema usiri huo hauwezi kuleta matunda yoyote.

Alisema hadi sasa, si yeye wala Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Mhashamu Augustino Shayo waliopewa taarifa za maendeleo ya upelelezi wa matukio yote.

"Mimi nadhani vyombo vya usalama ukimya wao hausaidii kumaliza tatizo lililopo sasa, tukio la mauaji ya padri wetu Zanzibar na lile la kujeruhiwa Padri Mkenda, hadi leo mambo yanaendeshwa kwa usiri, si mimi Kardinali Pengo wala mwenzangu Askofu Shayo anayefahamu kinachoendelea&#8230; hali hii haiwezi kusaidia kuimarisha amani nchini, inaonyesha kama vile mambo haya yanataka kufunikwa," alisema Kardinali Pengo.

Akizungumzia hali ya amani nchini, Kardinali Pengo alisema kuna kila sababu Serikali kuona umuhimu wa kukutana na viongozi wa dini za pande zote ili kujadiliana.

Alisema hali ya kutoelewana kama ikiachwa ikiendelea hivi, taifa litakuwa katika hatari kubwa.

"Kama ni suala la udini, mbona tumeishi kama ndugu kwa muda mrefu, hapa huenda kuna kitu kimejificha, sisi kama viongozi tunawajibu wa kukutana na kujadiliana, Serikali ndiyo ina wajibu mkubwa wa kuona hali hii si njema na kuna kila sababu ya kutafuta chanzo na suluhu," alisema Pengo.

Alisema katika majadiliano hayo, ni vyema pande zote zikakubali kufikia muafaka badala ya kufanya malumbano ambayo yatakuwa hayana tija yoyote kwa taifa.

Alipoulizwa kuhusu fununu za watu wasiofahamika kuvamia makanisa katika mkesha wa Sikukuu ya Pasaka, Kardinali Pengo alisema yeye binafsi kazi yake ni kuwaimarisha kiroho wananchi na hawatumii silaha, hivyo jukumu la kuimarisha usalama ni la Serikali.

"Mimi binafsi, sioni sababu za kushindwa kwenda kusali kanisani kutokana na tishio la kuvamiwa makanisani, ninachoahidi hata kama nikisikia kuna watu wanataka kuja kuniua nikienda, nitakwenda na kuingia ili mradi nife nikiomba," alisema Kardinali Pengo.

Hata hivyo, Pengo alitumia fursa hiyo kumtahadharisha kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis I kutokana na mazingira anayoishi.

Alisema dunia ya sasa imebadilika mno na anapaswa kuishi kwa kuchukua tahadhari.

"Papa amezoea kuishi maisha ya kawaida ya kuwa jirani na jamii, lakini kutokana na mazingira yetu nafikiri ni muda muafaka sasa wa kubadili maisha haya na kuchukua tahadhari," alisema Kardinali Pengo.

Alisema lengo kuu la Papa Francis I kuishi hivyo, kunatokana na kupambana na wakandamizaji ambao wanawanyima haki za msingi watu masikini, watu wanaowakandamiza masikini na fukara," alisema Pengo.

Alisema hali ya uvunjifu wa amani inaweza kutokea wakati wowote, kama vila ambavyo iliwahi kumkuta marehemu Papa John Paul II, ambaye alipigwa risasi na kujeruhiwa.

Kuhusu mchakato wa kumpata Papa mpya, alisema ulifanyika kwa amani tofauti na watu wengi wanavyofikiri.

"Ukiwa mle ndani, haufahamu vinavyoendelea nje lakini ninachofahamu mimi hata mwizi akipanga kuiba hujiandaa, hivyo hata yule mtu anayedaiwa alivamia mkutano wetu angejiandaa hata kwa mavazi yanayofanana na sisi tu, huenda amechanganyikiwa," alisema Pengo.

Katika hatua nyingine, Kardinali Pengo amewatakia Watanzania Sikukuu ya Pasaka njema, huku akisisitiza ujumbe wa mwaka huu ni; "Tujenge amani, mshikamano na upendo" na kwamba itafanyika kitaifa mkoani Dodoma.


KUUAWA PADRI EVARIST
Padri Evarist Mushi alifariki dunia, baada ya kupigwa risasi utosini na watu wasiojulikana.

Padri huyo, alikuwa akielekea kanisani kuendesha misa ya saa 3 asubuhi, kwenye Kanisa la Mt. Theresia.

Tukio hilo, lilitokea eneo la Mtoni ambapo alisimamishwa na watu wawili ambapo mmoja wao alimpiga risasi utosini na kufariki papo hapo.

 
Police ni Tawi la Chama Tawala Nchini... Wanapandishwa VYEO kwa KUVIVIMBIA vyama vya UPINZANI...
 
Haiwezekani unapochunguza jambo basi au kuwatafuta watu kama wauaji kuweka hadharani taarifa za uchunguzi wako kama hujakamilisha kwa sababu unaowatafuta ama kuwachunguza na wao pia ndipo wanapanga mikakti yao ili wasitambulike ama kujulikana. Tuwe na subira ili tupate taarifa zilizo kamilika.
 
Nilisoma mahala kuwa kuna mchungaji wa assemblies church alitekwa na hajajulikana alipo.
Serikali yetu sikivu. Inasikiliza lakini kutenda haiwezi katu. INASIKILIZA just like everybody else. Ngoja sasa Pinda arudi na tamko, hakawii kulia machozi na kusisistiza naye ni mkatoliki na amesikitishwa mno mno!
Crass!

My dear siku hizi halii tena, kaja na style mpya ya ..... Liwalo na liwe...
 
Haiwezekani unapochunguza jambo basi au kuwatafuta watu kama wauaji kuweka hadharani taarifa za uchunguzi wako kama hujakamilisha kwa sababu unaowatafuta ama kuwachunguza na wao pia ndipo wanapanga mikakti yao ili wasitambulike ama kujulikana. Tuwe na subira ili tupate taarifa zilizo kamilika.

Nahisi we unaendeshwa na ushabiki kwa chama chako na sio ukweli.
Ni lini jeshi la polisi lilishawahi kufanya uchunguzi wa kimya kimya? Kuropoka ndio style ya utendaji wa jeshi letu, HILO HALINA UBISHI.

Lakini jambo lingine ni kwamba, kwenye matukio yetu ya kihalifu hasa ya utekaji nyara na mauaji ya raia, huwa tume zinaundwa kufanya uchunguzi, lakini mara zote maendeleo na hata matokeo ya chunguzi hizo huwa haziwekwi wazi......KWA NINI?
Tabia hii ndo inayotufanya tuamini kuwa kwenye hayo matukio ni ama jeshi hilo, TISS au IKULU zinahusika.

Kimsingi sisi raia tunapaswa kufahamu mwenendo wa chunguzi zote zinazofanywa, NI HAKI YETU!
 
pengo avue kanzu avae gwanda. muda haujawa mrefu sn. aache polisi waendelee na uchunguzi
 
Police haven't failed. It's too early to accuse them of that.


Radhia!!!!!!!!!!!!!!! Bwalo was short dead in mwanza and it took police two weeks to arrest those involved.
kwa nini sasa hapa tunachorewa kipicha?????????????????
 
Mkuu, nakubaliana nawe ki-aina. Lakini angekuwa kauawa mkeo/mmeo au mtoto wako ungekuwa na ujasiri wa kuongea kama ulivyoongea? Kwamba kwa sababu wahalifu nao ni professionals basi tusubiri hata miaka ipite kabla hawajakamatwa?
sasa kama hawana lead ya kuwapelekea kwa hao wahalifu wanafanyaje?.Hata marekani imewachukua miaka 11 kumnasa bin laden.Na bado kuna matukio ya uhalifu hata FBI huwa wanafika kwenye deadend na kesi ina remain unsolved.It is nothing new.
 
If you remember in 1998 MWEMBECHAI KILLING WALISEMA WAUENI WAHUNI HAO na waliotekeleza mauaji hao walipandishwa na vyeo na kushangiliwa na hata na PENGO kwa wakati huo rais alikaa kimya na wale wale wameendelea kufanya mauaji hayo tena kwa makusudi kabisa kamakwamba hatuna haki ya kuishi katika nchi hii ambayo viongozi wake wanafikiria kwa kutumia mak.....vp kule Arusha Iringa Mbeya na sehemu nyingine ambapo wamefanya mauaji bila sababu. Ni ukweli usiofichika kwamba amani hakuna labda MAGOGONI,ST JOSEPH MTORO. Kibanda kasema tu tayari wamemgwipande. Matokeo ya haya yote ni dhuruma kwa watu ipo sababu wameuza madawa ya kulevya akawazima na wao wakamuulia mbali
 
PENGO aache kukurupuka! kukamata waalifu sio kazi yake! ni kazi ya polisi ambao wanautaratibu wao! lakini pia mbona hazungumzii watu wengine waliouwawa yeye anang'ang'ania Padri Mushi ambaye inahusishwa na biashara haramu.
hapo ndo ushangae yaani katika waliokufa yeye kaona mushi tu,kumbe huyu kadinari ako na matatizo eeah...
 
Pengo aliwahi kusema wale waliopigwa risasi na polisi kwenye maandamano Pemba Mwembechai walikuwa wahuni.

Leo Mushi kapigwa risasi anawalalamikia tena polisi.

Pengo vua ukadinali ingia kwenye siasa.
 
Back
Top Bottom