Pengo: Kilimo Kwanza ni wimbo tu

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Na Minael Msuya
Mwananchi

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema kuna kila dalili za kukwama kwa Mkakati wa Kilimo Kwanza, kutokana na kushindwa kuelekeza nguvu za kutoa elimu kwa wakulima ili waendeleze sekta hiyo.

Kardinali Pengo alitoa kauli hiyo jana katika hafla ya kuzindua jengo jipya la maabara katika Chuo cha Teknolojia ya Uhandisi cha Mtakatifu Joseph kilichopo Mbezi Luguruni jijini Dar es Salaam.

Jengo hilo limepewa jina la âHis Eminence Polycarp Cardinal Pengo Blockâ.

Kauli ya Kardinali Pengo inakuja wakati serikali imekuwa ikielekeza nguvu nyingi katika kutekeleza mpango huo mkubwa, ikiwa ni pamoja na kusambaza matrekta mikoani.

Akionyesha mtizamo huo tofauti, Pengo alisema, "Kaulimbiu inayotumiwa na viongozi wa nchi (Kilimo Kwanza), haiwezi kubadili au kuleta maendeleo katika kilimo, cha msingi hapa ni kumwezesha mkulima kwanza ili apate elimu ya kuendeleza kilimo.â

Kwa mujibu wa Pengo, ni vigumu kufikia azma ya Kilimo Kwanza bila kuwawezesha wakulima kwa kuwa mabadiliko ya kimaendeleo katika nyanja ya kilimo yanapatikana kwa mkulima mwenye elimu.

âMkakati wa Kilimo Kwanza umekuja wakati mwafaka, lakini cha msingi ni kumuelimisha mkulima kwanza, hii itasaidia kilimo kiweze kuwa na maendeleo kwa kuwa wakulima ndio wanaotakiwa kuwezeshwa kielimu,â alisisitiza Pengo.

Pengo ambaye ni nadra kuzungumzia utendaji wa serikali, alisema kilimo kimekuwa kikizungumzwa kama wimbo, bila kuweka nguvu katika utekelezaji wenye kuwawezesha wakulima ambao ndiyo wahusika wakuu.

Alisema jambo hilo linachangia ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira magumu, hasa maeneo ya vijijini.

âKwa kuwa kilimo kimekuwa kikizungumzwa tu kama wimbo, vijana wengi wamekuwa wakiondoka vijijini na kukimbilia kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam, wakifikiri watapata maisha bora, kumbe wanakuja kukutana na ugumu wa maisha na kupoteza mwelekeo wao kabisa," alieleza.

Alisisitiza kwamba, kutokana na hali hiyo vijana wengi wanaoishi maeneo hayo hukimbilia mijini wakifikiri ndiko kwenye fedha na badala yake hutumbukia katika dimbwi la umaskini na kujiingiza kwenye matendo mabaya.

Kiongozi huyo wa kiroho wa Kanisa Katoliki, alisisitiza kuwa serikali ina wajibu kuhakikisha elimu ya kilimo inaifikia jamii na kumwezesha mkulima kwanza.

Alisema atahakikisha elimu juu ya hilo inatolewa kumwezesha mkulima kwanza kupitia chuo hicho ambacho kitatoa elimu ya kilimo kwa wananchi ili kuongeza uelewa wa kilimo.

Akizungumza na gazeti hili baada ya uzinduzi huo, mwanzilishi wa chuo hicho Thamson Ananth, alisema chuo chake kitaanza kuwapatia wanafunzi elimu ya kilimo kuanzia mwezi Machi hadi Agosti mwaka 2010.

Alisema lengo ni kusaidia utekelezaji na kuikuza kauli na dhamira ya kumuwezesha mkulima kwanza na kuendeleza kilimo.

Aliongeza kwamba, baada ya Agosti mwaka 2010 chuo chake kitakuwa kikitoa elimu hiyo ya kilimo kwa wakulima kupitia chuo chake cha Dar es Salaam na Songea mkoani Ruvuma kwa vitendo.

âTutatoa elimu ya kilimo kwa kipindi cha miezi sita, tunaamini kauli ya kumwezesha mkulima itakuwa na nguvu kwa kuwapatia wakulima mafunzo hayo ya kilimo kwa vitendo kwani nao wataeneza elimu hiyo kwa wananchi," alisema Ananth.

Tangu serikali kutangaza mpango huo wa Kilimo Kwanza, kumekuwa na maoni na mitazamo tofauti kutoka kwa wadau mbalimbali huku wengine wakihofu kushindwa kwa mpango huo kutokana na kutomlenga zaidi mkulima.

Kuanzia uhuru, kumekuwa na kauli mbiu ambayo ilikuwa ikisisitiza kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wa nchi na serikali ya awamu ya kwanza, ilitekeleza kwa vitendo na asilimia 80 ya Watanzania waliishi kwa kutegemea kilimo.

Lakini, sekta ya kilimo ilianguka zaidi nchini baada ya mageuzi ya kiuchumi miaka ya 1990 hali ambayo iliua viwanda vya uzalishaji dhana na pembejeo za kilimo.

Tayari kulikuwa na mipango mbalimbali ikiwemo ile ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo, Mapinduzi ya Kijani na sasa Kilimo Kwanza kama mkakati mkuu wa kitaifa.
 
Sahihisha hiyo title yako. Ni Pengo siyo Pendo. Sijui mnakimbiliaga wapi na hizi copy paste zenu.
 
Kwa hili tunapiga hatua, maoni huru kama hivi yanasaidia sana kujenga nchi. Heko kardinali Pengo....Watanzania tumechoka kusikia wasomi wenye uelewa wa mambo wakiunga mkono hoja za kipumbavu ili mradi aliyesema ni kiongozi CCM/Serikali.
 
Kilimo kwanza ni slogan kuelekea uchaguzi mkuu, maana hata hawajatupa maelezo juu ya failure na mafanikio na MKUKUTA na MKURABITA, WANALETA MISAMIATI KUFICHA MAPUNGUFU YAO.
mimi nawashangaa sana, naungana na Pengo kua tuanze na viwanda kisha mapinduzi ya kijani yatawezekana......hebu angalia EMBE, NANASI NA MATUNDA Mengine yanavyooza mitaani , huwezi kuendelea kwenye kilimo kama wakulima hawawezi kuondokana na hasara hizi baada ya jasho jingi...
 
viongozi wa tanzania wakiishiwa hoja wankuja na maneno ya kujitetea yasio na maana
Mkapa= MiTanzania mingine ina wivu wa kijinga
JK= 70% ya watanzania wanafata upepo

sasa hapa nadhani kuna wakinapengo, Butiku na wengineo wanaingia kwenye hiyo ya Mkapa, na wengine tunafuata mkumbo wa kuvaa tshirt na kofia za ARI MPYA, KASI MPYA, NGUVU MPYA, na sasa KILIMO KWANZA nadhani wanaingia kwenye hiyo ya JK

na mwisho kabisa JK anasisitiza UKILA SHARTI ULIWE
 
Wewe Mhehe nini? Mbona badala ya Pengo imekuwa Pendo? Hakuna uhusiano wa karibu wala wa mbali kati ya hayo majina mawali. sasa wewe umetafsiri kwa lugha gani?

Get to the point mpwa si umeisha elewa ni nani anaeongelewa hapo juu sasa badala ya kutoa maoni yako we watujazia QUOTE hapa kwa page.

 
Wakuu,

Cardinal Pengo amenena. Ni kweli ili kuwa na mabadiliko ya kweli kwenye Kilimo inabidi tuanze na wakulima. kauli yake ya WAKULIMA KWANZA ni sahihi kabisa na ina nguvu na radhaa nzuri kuzidi kauli mbiu ya KILIMO KWANZA. Tunawaombea mafanikio zaidi katika mkakati wao kupitia Chuo Kikuu cha Kilimo wanachotegemea kukijenga mkoani Ruvuma kwenye eneo la Hekta 3,000.

Kutokana na azma hii ni muhimu Serikali ikaangalia namna ya kuwasaidia kifedha. Suala ni uamuzi kwani fedha zipo.
 
Alichosema Pengo ni ukweli mtupu; mabadiliko ya kweli hayatatokana na kauli mbiu za watu toka makao makuu bali elimu bora na uwezeshwaji wa wakulima huko vijijini.

Labda ambacho pia Pengo angeongelea pia ni wajibu wa kanisa na wadau wengine wote katika kufanikisha hilo lengo la kumpa elimu Mtanzania na kumwezesha. Kama ambavyo kanisa limeshiriki vya kutosha kwenye masuala ya elimu na afya, wana nafasi pia ya kushiriki ipasavyo kwenye kilimo.

Miradi ya kilimo inayoendeshwa na kanisa au msikiti kwa kushirikiana na waumini wao inaweza kuwa chanzo cha elimu kubwa na mabadiliko ya kweli kwa waumini hao.

Kwa Tanzania wakati mwingine dawa sio kunyosheana vidole kila siku bali kuamua kushiriki kwenye jambo fulani na kuonyesha kwa vitendo kwamba we can do better than those folks in the government.
 
Leo makada wamesemama wanaompinga Jk NI WAHAINI ,KWANINI AWAKAMATWI.
Kweli hii ni kilimo kwanza kabisa.
 
This is what we call "walking the talk". Serikali ni maneno matupu jana nilimuona Waziri Wasira katika Jambo Tanzania-TBC1 anamungunya maneno kuhusu kilimo kwanza ni siasa tupu! Welldone Cardinal Pengo
 
Mtanzania, ulichosema ni kitu cha msingi sana. Binafsi sina wasiwasi na kanisa katoliki watafika mbali sana na hicho Chuo chao Kikuu cha Kilimo wanacho tegemea kukijenga mkoani Ruvuma kuanzia mwakani, 2010. Historia ya utendaji wao na mashirika yake ni ushahidi mzuri linapokuja suala na kuanzisha taasisi mbalimbali na kuziendesha kwa ufanisi pamoja na miradi husika.

Kwa upande huohuo, naamini dini zetu zikiamua kushirikiana na kuunganisha nguvu kwa ajili ya kumkomboa mkulima tutafika mbali sana ndani ya miaka 10 ijayo. Hapa napata wazo la dini zetu la kuwa na Mfuko wa Pamoja kwa ajili ya wakulima wetu hasa upande wa elimu na uwezeshwaji kama alivyoshauri Cardinal Pengo. Njia endelevu na nzuri ya kupata fedha kwa ajili ya Mfuko huo ni kuwa na UTARATIBU WA KUTOA SADAKA MAALUM KILA WIKI KATIKA NYUMBA ZETU ZA IBADA. Iwapo wazo hili litakubalika na kutekelezwa, sitashangaa kila mwezi Sadaka Hii maalum kuzidi shilingi bilioni 20 toka kwa zaidi ya waumini milioni 30 waliopo nchini mwetu.
 
Kilimo kwanza ni mradi wa vigogo wa nchi hii kupata nafasi ya kuuza matrekta yao kupitia halmashauri za wilaya huku wakiwaacha wananchi maskini wakiendelea kulima kwa jembe la mkono na kuwa maskini, heko Cardinal Pengo kwa kuwaambia ukweli.
 
Nilikuwa safarini mikoani hivi karibuni, kusema kweli kilimo kwanza is a serious joke. Mikoa ya Morogoro, Iringa na Mbeya njiani ukipita mkulima bado yuko vilevile jembe la mkono, shamba lake halijaongezeka ukubwa, mbolea anabeba kichwani yeye mtoto wake na wajukuu kupeleka shambani. Literally hakuna kilichobadilika hebu tuelezeni vizuri kilimo kwanza maana yake ni nini mkulima mtanzania au kuna mkulima mwingine anayefikiriwa.

Mnahangaika na power tillers, kama mkulima anashindwa jembe la kukokotwa na ng'ombe atawezaje power tiller ambayo itakuwa chini ya halmashauri ya wilaya yenye viwavi vyenye njaa ya pesa. Mkulima atasalimika mikononi mwa maafisa wajanja wa halmashauri?

Kwa mujibu wa Pengo, ni vigumu kufikia azma ya Kilimo Kwanza bila kuwawezesha wakulima kwa kuwa mabadiliko ya kimaendeleo katika nyanja ya kilimo yanapatikana kwa mkulima mwenye elimu.

Wazo la kilimo kwanza sio la mkulima Mhadhama Kadinali Pengo yuko sahihi kabisa, kwa vile mkulima hakuhusishwa wazo hili haliwezi kufanikiwa kwa mkulima mtanzania, linaweza kufikiwa kwa walengwa ambao sio wakulima Watanzania
 
Kilimo kwanza pesa zake zinatokea Ireland na JK na wenzae wamechukulia kama kauli mbiu ya CCM . Hawakuwa na wazo hili ila kwa kuwa mapesa yanatoka kwa wazungu wamechamkiwa sana na mwisho hakuna lolote . Hakuna cha kilimo kwanza wala nini ni ubabaishaji mkubwa . Fika kijijini kwetu huku wala hawana habari na Kilimo kwanza ila iko majukwaani huko mjini na huko hawalimi .
 
Watanzania bwana. Hivi mnafikiri wazungu walipewa elimu kwanza ndio wakaanza kuwa wakulima wazuri?

Ukienda huko Songea watu wanajua kucheza ngoma vizuri bila kupewa mafunzo yoyote yale. Wengine wanacheza vizuri unafikiri walizaliwa wakiwa wameshikilia ngoma.

Tuachane na mambo ya ubishi ubishi. Kuna kazi haziitaji elimu hata kidogo na mojawapo ni ya ukulima. Fomula zote za kulima vizuri zipo na watu walichazitumia kwa zaidi ya miaka 2000 kwanini mnapoteza muda kutaka kusomesha watu?

Hata suala la kilimo mnataka kuingiza siasa.
 
Hivi yale mamilioni ya JK yameishia wapi???
Yametafunwa na wajanja, wala hayakufikia walengwa hata kwa asilimia 2! Nadhani pamoja na sababu nyingine(Michango ya kujenga shule-ambazo nazo zilitafunwa pia), hii isue ndo iliochangia kwa Kandoro kuamishwa Dar
 
Back
Top Bottom