Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,894
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Na Minael Msuya
Mwananchi
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema kuna kila dalili za kukwama kwa Mkakati wa Kilimo Kwanza, kutokana na kushindwa kuelekeza nguvu za kutoa elimu kwa wakulima ili waendeleze sekta hiyo.
Kardinali Pengo alitoa kauli hiyo jana katika hafla ya kuzindua jengo jipya la maabara katika Chuo cha Teknolojia ya Uhandisi cha Mtakatifu Joseph kilichopo Mbezi Luguruni jijini Dar es Salaam.
Jengo hilo limepewa jina la âHis Eminence Polycarp Cardinal Pengo Blockâ.
Kauli ya Kardinali Pengo inakuja wakati serikali imekuwa ikielekeza nguvu nyingi katika kutekeleza mpango huo mkubwa, ikiwa ni pamoja na kusambaza matrekta mikoani.
Akionyesha mtizamo huo tofauti, Pengo alisema, "Kaulimbiu inayotumiwa na viongozi wa nchi (Kilimo Kwanza), haiwezi kubadili au kuleta maendeleo katika kilimo, cha msingi hapa ni kumwezesha mkulima kwanza ili apate elimu ya kuendeleza kilimo.â
Kwa mujibu wa Pengo, ni vigumu kufikia azma ya Kilimo Kwanza bila kuwawezesha wakulima kwa kuwa mabadiliko ya kimaendeleo katika nyanja ya kilimo yanapatikana kwa mkulima mwenye elimu.
âMkakati wa Kilimo Kwanza umekuja wakati mwafaka, lakini cha msingi ni kumuelimisha mkulima kwanza, hii itasaidia kilimo kiweze kuwa na maendeleo kwa kuwa wakulima ndio wanaotakiwa kuwezeshwa kielimu,â alisisitiza Pengo.
Pengo ambaye ni nadra kuzungumzia utendaji wa serikali, alisema kilimo kimekuwa kikizungumzwa kama wimbo, bila kuweka nguvu katika utekelezaji wenye kuwawezesha wakulima ambao ndiyo wahusika wakuu.
Alisema jambo hilo linachangia ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira magumu, hasa maeneo ya vijijini.
âKwa kuwa kilimo kimekuwa kikizungumzwa tu kama wimbo, vijana wengi wamekuwa wakiondoka vijijini na kukimbilia kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam, wakifikiri watapata maisha bora, kumbe wanakuja kukutana na ugumu wa maisha na kupoteza mwelekeo wao kabisa," alieleza.
Alisisitiza kwamba, kutokana na hali hiyo vijana wengi wanaoishi maeneo hayo hukimbilia mijini wakifikiri ndiko kwenye fedha na badala yake hutumbukia katika dimbwi la umaskini na kujiingiza kwenye matendo mabaya.
Kiongozi huyo wa kiroho wa Kanisa Katoliki, alisisitiza kuwa serikali ina wajibu kuhakikisha elimu ya kilimo inaifikia jamii na kumwezesha mkulima kwanza.
Alisema atahakikisha elimu juu ya hilo inatolewa kumwezesha mkulima kwanza kupitia chuo hicho ambacho kitatoa elimu ya kilimo kwa wananchi ili kuongeza uelewa wa kilimo.
Akizungumza na gazeti hili baada ya uzinduzi huo, mwanzilishi wa chuo hicho Thamson Ananth, alisema chuo chake kitaanza kuwapatia wanafunzi elimu ya kilimo kuanzia mwezi Machi hadi Agosti mwaka 2010.
Alisema lengo ni kusaidia utekelezaji na kuikuza kauli na dhamira ya kumuwezesha mkulima kwanza na kuendeleza kilimo.
Aliongeza kwamba, baada ya Agosti mwaka 2010 chuo chake kitakuwa kikitoa elimu hiyo ya kilimo kwa wakulima kupitia chuo chake cha Dar es Salaam na Songea mkoani Ruvuma kwa vitendo.
âTutatoa elimu ya kilimo kwa kipindi cha miezi sita, tunaamini kauli ya kumwezesha mkulima itakuwa na nguvu kwa kuwapatia wakulima mafunzo hayo ya kilimo kwa vitendo kwani nao wataeneza elimu hiyo kwa wananchi," alisema Ananth.
Tangu serikali kutangaza mpango huo wa Kilimo Kwanza, kumekuwa na maoni na mitazamo tofauti kutoka kwa wadau mbalimbali huku wengine wakihofu kushindwa kwa mpango huo kutokana na kutomlenga zaidi mkulima.
Kuanzia uhuru, kumekuwa na kauli mbiu ambayo ilikuwa ikisisitiza kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wa nchi na serikali ya awamu ya kwanza, ilitekeleza kwa vitendo na asilimia 80 ya Watanzania waliishi kwa kutegemea kilimo.
Lakini, sekta ya kilimo ilianguka zaidi nchini baada ya mageuzi ya kiuchumi miaka ya 1990 hali ambayo iliua viwanda vya uzalishaji dhana na pembejeo za kilimo.
Tayari kulikuwa na mipango mbalimbali ikiwemo ile ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo, Mapinduzi ya Kijani na sasa Kilimo Kwanza kama mkakati mkuu wa kitaifa.