Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

Nimekua kimya nikijaribu kufuatilia hoja zenu waungwana,mnaodai ukatibu mkuu wa slaa ni mkubwa kuliko ubunge,hoja yenu dhaifu sana,umaarufu wa slaa hautokani na ukatibu mkuu wake bali ulitokana na ubunge sasa kwa nini asirudi bungeni akamalizie kazi aliyoianzisha?au mnataka asubiri nafasi ya ubunge wa kuteuliwa na rais mwaka 2013 mwishoni kufuatia muafaka wa haya mazungumzo ya upenuni kati ya jk na mbowe?kama hamjui ndio tunakoelekea!Na nyie mnaodai eti slaa ni rais mnamdanganya pamoja na kujidanganya nyie!na pia mnaosema eti sijui ataibiwa kura na kufirisika kisiasa pia ni uongo!hivi kura huwa zinaibiwaje?ndugu zanguni amkeni msikubali kudanganywa na wanasiasa,tatizo wanasiasa wetu wa africa huwa hawasemi ukweli kwa kuogopa kuwajibika kutokana na kushindwa chaguzi ndio huwa wanakuja na kisingizio cha kuibiwa kura wakishindwa,hivi hamjiulizi kama wizi wa kura upo kwanini cuf inairesa ccm pemba?au kwanini Ndesambura anaitesa kila wakati ccm moshi mjini?au kwanini Mzee Said Arfi makamu mwenyekiti wa cdm amekua kwa muda mrefu hata wakati slaa hajulikani amekua akiitesa ccm huko mpanda kwake?au zitto kwa nini anitesa ccm?Huwezi kuiba kura,huwa mnakua mmeshindwa tu,msidanganyike na watu kujaa kwenye mikutano yenu ya kampeni au hapa jf watu wengi kuonekana wanaipenda chadema,wengi sio wapiga kura!
Jamaa Mzushi sana wewe. Dr Slaa amekuwa Mbunge tangu mwaka 1995 na Arfi ameingia Bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2005 halafu unasema Arfi alikuwa anaitesa CCM wakati Dr Slaa bado hajulikani? Labda wewe ndio ulikuwa humkui lakini Patrick Tsere wa Karatu anamfahamu vizuri sana. Wazo la Slaa kugombea Areumeru halikubali, sio muafaka, ni kichochezi na linaashiria agenda binafsi kama sio uoga wa nguvu zake anazoelekeza kuijenga CDM. Hebu rudi kaendeleze hoja yako ya Mrithi wa marehemu Regia Mtema hapa umechemsha sana
 
Big NO. magamba wataona anuchu wa madaraka na pesa hasa za bungeni , hadhi ya chama itashuka. abaki kuwa mgombea urais tuu. Cha msingi wajipange sawasawa, wachukue jimbo hilo.
 
Mkuu yule kijana Joshua nilimuona kwenye mchakato majimboni enzi zile za kampeni, kwakweli alionyesha ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa na upeo mkubwa wa uelewa wa mambo,
Nilisikitika sana aliposhindwa uchaguzi, kunahitajika kuwaacha vijana waonyeshe uwezo wao

elishilia kaaya ambaye ni mkurugenzi mwendeshaji wa aicc na mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm taifa nec anachukuwa ubunge huo wa arumeru mashariki mapema asubuhi hakuna ndani ya cdm wa kushindana naye
 
Siungi mkono hoja. Akigombea CCM wanaweza kutumia hata sh trilioni moja ili wamwangushe ambapo sasa atakufa kisiasa. Pili ataonekana ana tamaa. Tatu jimbo lake Karatu sio Arumeru.

Watu wasiojua, hapa mjini kabila lolote anaweza kupata ubunge isipokuwa ilala na temeke pagumu. Ila vijijini kama si mtu wa pale si rahisi kupata. Mimi ni mmeru na nawajua wameru tulivyo wakorofi ukimleta Mmbulu anaweza kukosa.

Kwa swala la ubunge kuna ukabila sana, hata kama angekuwa mmeru lakini si wa jimbo hilo asingepata. Nenda msukukumu ukagombee Kyela, mchagga ukagombee Bukoba vijijini, Mpare ukagombee Hai, huwezi kupata. Nampigia chapuo kijana yule agombee Dr akampigie debe tu
Umechambua vzr kaka, Slaa kichwa cha urais kile, kugombea ubunge ah, no. Kwani bila wizi yeye si ndo angekuwa prezidaa wetu sasa? Wamweke huyo kijana agombee tena, hulo ni kwao, ana uchungu nako mkubwa, Dr Slaa ampigie debe, kura zilindwe, na nina uhakika CDM itashinda tu!
 
Nimekua kimya nikijaribu kufuatilia hoja zenu waungwana,mnaodai ukatibu mkuu wa slaa ni mkubwa kuliko ubunge,hoja yenu dhaifu sana,umaarufu wa slaa hautokani na ukatibu mkuu wake bali ulitokana na ubunge sasa kwa nini asirudi bungeni akamalizie kazi aliyoianzisha?au mnataka asubiri nafasi ya ubunge wa kuteuliwa na rais mwaka 2013 mwishoni kufuatia muafaka wa haya mazungumzo ya upenuni kati ya jk na mbowe?kama hamjui ndio tunakoelekea!

Na nyie mnaodai eti slaa ni rais mnamdanganya pamoja na kujidanganya nyie!na pia mnaosema eti sijui ataibiwa kura na kufirisika kisiasa pia ni uongo!hivi kura huwa zinaibiwaje?ndugu zanguni amkeni msikubali kudanganywa na wanasiasa,tatizo wanasiasa wetu wa africa huwa hawasemi ukweli kwa kuogopa kuwajibika kutokana na kushindwa chaguzi ndio huwa wanakuja na kisingizio cha kuibiwa kura wakishindwa,hivi hamjiulizi kama wizi wa kura upo kwanini cuf inairesa ccm pemba?au kwanini Ndesambura anaitesa kila wakati ccm moshi mjini?au kwanini Mzee Said Arfi makamu mwenyekiti wa cdm amekua kwa muda mrefu hata wakati slaa hajulikani amekua akiitesa ccm huko mpanda kwake?au zitto kwa nini anitesa ccm?Huwezi kuiba kura,huwa mnakua mmeshindwa tu,msidanganyike na watu kujaa kwenye mikutano yenu ya kampeni au hapa jf watu wengi kuonekana wanaipenda chadema,wengi sio wapiga kura!

Mhe wizi wa kura uwa upo,mimi binafsi nilishawai kushiriki kabla sijaokoka,mimi naamini unaleta utani,hao unaowataja kuwa mbona wanashinda uwa wanashinda kwa kiwango kikubwa ambacho hata kamati za ushindi/wizi haziwezi kubadili kitu,si rahisi kubadili kura za tofauti ya 5000!lakini kama ni ndani ya 1000 uwa wanaweza kubadili,kumbuka wizi unaotumika ni wa aina nyingi sana,si wakuchomeka kura tu,upo wa aina nyingi mfano kuharibu kura za upinzani kurubuni mawakala wa upinzani na kuandika idadi ya uongo kuendana na kura zilizopigwa nyingine ni kununua shahada kabla ya uchaguzi,kama utapinga yote hayo utakuwa umeamua kubisha tu.
 
"Mmiliki halali" wa Jimbo hili ni Lowasa. Atakalosema ndilo litakalokuwa. Hata akiamua mkwewe amrithi baba yake ndivyo itakavyokuwa.
 
Tunamhitaji Dr W Slaa Arusha Mjini bana ha ha ha ha ha ha ha ha ha.
 
jibu wapi nilipoandika au kuonyesha nina nasaba na hicho chama chenu cha kususa na kuandamana?mbona unaikwepa hii,sema tu ulikurupuka usione haya!

Pole Magamba mbinu yako imejulikana peupe.Rudi kwa Nepi mwambie wale watu wamenishtukia
 
Binafsi napendekeza CHADEMA imsimamishe Dr.SLAA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huko Arumeru. Hii itaipa chadema kwanza nafasi kubwa ya kukinyakua kiti hicho kwa kuwa Slaa kwa sasa ni heavy weight politician na pia watanzania wenye uchungu na nchi hii tumekuwa tukiukosa mchango wa Dr pale bungeni.

Wengi tunaukumbuka ujasiri wake akiwa anga zile, kiukweli Mboe anapwaya kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani pale bungeni,waziri mkuu Pinda na serikali yake wanahitaji kuchangamshwa na mtu machachari wa aina ya Slaa,Lema au Tundu!....

Mboe amekua na huruma huruma hivi,sasa slaa kama atafanikiwa kushinda ubunge(nina uhakika atashinda)basi mh.mboe awe muungwana kwa kumpisha bwana Slaa kiti cha kiongozi wa upinzani!hii imekaaje wadau,yote ni katika kuimarisha makali ya bunge.
Lema ana uwezo mdogo sana wa kujenga hoja zenye logic za kisomi na kutoa structured arguments kutetea kile anachodai, hivyo si sahihi kabisa kumuweka kundi moja na Dr.SLAA, LISSU au Zitto. Lema ana siasa za ufuasi zaidi kwa maana ya kuwa na upeo mdogo!
 
Hiyo ya kushindwa mimi siiamini sana,ok pengine labda tunatofautina,mimi ni mpiganaji huwa siamini katka kushindwa bali kushinda tu.Na hii haitakua mara ya kwanza kwa heavy weight wa aina ya slaa ambae ni national figure kwenda jimbo lingine na kushinda,alifanya hivyo mrema,licha ya serikali nzima kuhamia temeke kumhami sisco mtiro lakini kwa kuwa kura ni siri mrema alishinda,achaneni na maneno ya kitoto ya wizi wa kura,wananchi wakiamua ushinde utashinda tu.Rejea uchaguzi wa tarime kumrithi chacha.

Kwa nini naamini slaa atakua bora zaidi ya mbowe bungeni?jibu lake ni tofauti wa ELIMU na ufahamu wa wawili hawa,katika hivyo viwili mboe na dr ni sawa sawa na kulinganisha kifo na usingizi,mboe ni kama usingizi tu kwa kifo(slaa),na elimu ni jambo muhimu sana nadhani wote hapa tunakubaliana ya kwamba mwenye elimu zaidi ana maarifa zaidi.Sitaki kusema sana hapa namstahi mwenyekiti.Nadhani naeleweka,watu wazima nyie.

Kijana joshua kama yuko kwa ajili ya chama ataitwa na wazee kina makani watamuelewesaha ataelewa tu kama alielewa zitto na ukaidi wake wote tunaojua akamuachia mbowe uenyekiti itakua joshua!ndio mana kuna wazee,wazee ni grisi kazi yao ni kulainisha chuma kinapopata moto.kumsimamisha mtu kama joshua kwa nyingi lenye interest za mafisadi kama arumeru is a disaster!

Kabla ya kuleta upupu hapa kashauri kwanza ccm wenzako namna ya kujivua gamba
 
Kwa hadhi ya dkt.SLAA kusimama na MAGAMBA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge ni kumdhalilisha kisiasa. Pia MAGAMBA wako tayari kuhamishia jeshi,vifaru mizinga, usalama wa taifa maguruneti, silaha zote za kivita vigagura na wachawi wao kwenye jimbo husika kuhakikisha dkt SLAA anashindwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom