Pendekezo: RPC Kamuhanda (Ruvuma) ajiuzulu kwa kulea majambazi; kauli yake ni ya utata aombe radhi!

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Hivi sasa mkoani Ruvuma hususani manispaa ya Songea kumetokea wimbi kubwa la majambazi wanaoua wananchi.Mpaka hivi sasa ninapoandika thread hii watu 9 wameshapoteza maisha yao.Chanzo kikubwa cha mauaji haya hivi sasa ni kuwa huko msumbiji kuna mganga anayewapa utajiri wachimba madini.Hivyo anayehitaji utajiri huo analazimika kupeleka viungo vya binadamu hususani vyeti zake.Na mwanadamu anayesemekana ana bahati zaidi ni mwanamke.Hivyo watu ambao wameshachinjwa katika manaispaa hii wanakutwa wameshanyofolewa uchi na ulimi.

Hivi sasa mji wa songea upo katika hofu.Wananchi wamelalamikia hali hii na kumpelekea kamanda Michael Kamuhanda,lakini majibu yake yamekuwa kwamba watu wanakufa au kuchinjwa sababu kubwa ni mapaenzi na hadi sasa wameuawa watu 2 tu jambo ambalo ni uwongo.Juzi jioni sheikh amechinjwa akiwa anatokea msikitini.Je huyu naYE NI WIVU WA KIMAPENZI?Leo ninavyoamka lazima tena tupate habari mpya ya kuchinjwa watu.
Wananchi wa kata ya Lizaboni juzi waliandama baada ya kauli ya RPC kuwa hakuna mauaji.Wakafika kwa Said Mwambung mkuu wa mkoa huu.Majibu yake yakawa naye anasikia mauaji hayo lakini hajapewa taarifa kamili.Hapa RPC Kamuhanda tunamshuku ana maslahi binafsi na mauaji haya.
Sambamba na hilo Radio Jogoo iliyopo hapa Songea nayo tutaandamana ifungiwe kusema uongo kuwa hakuna jambo kama hilo mkoani hapa.Kamuhanda ametukera zaidi kwa kushindwa kutoa ulinzi wa polisi.Hakuna msako wowote uliofanyika kuwasaka watu hawa.Na inasemekana watu wanaofanya vitu hivi wanatokea msumbiji amabako dili hilo lilikoanzia.Watanzania wenzetu tuungeni mkono tumwondooe kamanda huyu.
 
Mimi nilitegemea kuwa tayari mpo barabarani mpaka ang'ooke...nawashangaa mnasubiri nini.
 
Inaonekana una bifu na kamanda wako.

1. Unasema leo lazima mpate taarifa ya mtu mwingine kufa. Kwa hiyo wewe unauhakika lazima mtu atakufa. kama unajua hilo, umeonesha ushirikiano gani kwa jeshi kudhibiti mauaji hayo?
2. Kwa nini jeshi lisikutie mbaroni kwa kushiriki uuaji, kwani unajua lini mtu atakufa na lini mtu hatakufa?
3. Umeshirikiana vipi na UHAMIAJI kudhibiti kuingia na kutoka kwa watu ambao sio watanzania?

kabla hujatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio, to boriti kwenye jicho lako
 
Hivi ni ukosefu wa elimu au ujInga uliokithiri? Wangeanza na nyeti zao af waone km familia zao ztatajirika ama......
 
Katika maandamano watu wawili wamepigwa risasi hadi kufa na polisi. So sad!
 
Inaonekana una bifu na kamanda wako.

1. Unasema leo lazima mpate taarifa ya mtu mwingine kufa. Kwa hiyo wewe unauhakika lazima mtu atakufa. kama unajua hilo, umeonesha ushirikiano gani kwa jeshi kudhibiti mauaji hayo?
2. Kwa nini jeshi lisikutie mbaroni kwa kushiriki uuaji, kwani unajua lini mtu atakufa na lini mtu hatakufa?
3. Umeshirikiana vipi na UHAMIAJI kudhibiti kuingia na kutoka kwa watu ambao sio watanzania?

kabla hujatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio, to boriti kwenye jicho lako

Hapo kwenye red nadhani imeshapata yaliyojiri.soma thread zote zinazohusu songea leo utaona kilichotokea.Nilichoandika ndicho kimetokea.Serikali yako ina pwaya
 
Hali ya mambo iliyotokea leo imethibitisha kuwa raia wakiamua wanaweza.Taarifa niliandika asubuhi lakini saa nne mambo yakaiva.Hali ya kamanda huyu kama hatarekebisha kauli yake mji utaendelea kushuhudia machafuko.
 
Kuna bwana mmoja amenipa taarifa hyo kutoka songea ilikuwa ni saa 11 jioni na akasema kuwa mpk muda huo zaidi ya raia 7 na askari mmoja wameuwawa kutokana na vurugu hizo
 
Inaonekana una bifu na kamanda wako.

1. Unasema leo lazima mpate taarifa ya mtu mwingine kufa. Kwa hiyo wewe unauhakika lazima mtu atakufa. kama unajua hilo, umeonesha ushirikiano gani kwa jeshi kudhibiti mauaji hayo?
2. Kwa nini jeshi lisikutie mbaroni kwa kushiriki uuaji, kwani unajua lini mtu atakufa na lini mtu hatakufa?
3. Umeshirikiana vipi na UHAMIAJI kudhibiti kuingia na kutoka kwa watu ambao sio watanzania?

kabla hujatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio, to boriti kwenye jicho lako

dah we unaonekana sio mtanzania,hivi kaa chini ujiulize nini maana ya kuchagua viongozi,usilete maneno ya biblia pengine hata maana hujui,sasa kama we ni kiongozi wa ulinzi na usalama,halafu usalama haupo unategemea nini?toka waache wanaojua wajibu wao wafanye kazi,eti we ni mwanausalama afu ndo unaongoza kuua,kuna usalama hapo kweli?kama huyo kamanda ni ndugu yako mwambie ajiuzuru ukamanda umemshinda akafuge kuku
 
Quotation za kilatini hakikisheni zipo sawa ili msiharibu maana ya maneno.

Unataka nianze kukufundisha conjugations za kilatini?au linakusumbua neno "quod" kwamba halijatafsiriwa?quod kwa kiingereza ni because,sasa hujaliona kwenye tafsiri linakusumbua.Pia neno "sensu" ni la kilatini lakini ni plural form,hivyo ulitaka liwe "senses".Unataka tafsiri aina gani?Nieleze nikupe tuition.Huenda hukupitia darasa la kilatini.
 
Kuna bwana mmoja amenipa taarifa hyo kutoka songea ilikuwa ni saa 11 jioni na akasema kuwa mpk muda huo zaidi ya raia 7 na askari mmoja wameuwawa kutokana na vurugu hizo

Taarifa hiyo ni ya kweli.
 
Kunauwezekano mkubwa wachimba madini wakawa wanasingiziwa kumbe ni wanasiasa/watawala washirikina wanatoa kafara ili waendelee kuwepo madarakani.

Tena unaweza kuta wauaji wanatoka mfLikuyu,
 
Tuiondoe ccm na serikali yake.kampeini nyumba kwa nyumba inaanza ianze.na kuwapa mafunzo makali mawakala wetu.[mbuni za kisasa kabisa kutoka nje ya nje].
 
Back
Top Bottom