JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
Edwin Mtei said:Mzee Mwanakijiji,
Nakushuru kwa pendekezo lako linaloonyesha ukomavu wa siasa zako, uzalendo, mapenzi na huruma kwa nchi yetu na watu wake. Ni jambo muhimu sana kwamba kiongozi aliyeko madarakani sasa, yaani Rais Kikwete aongoze katika tamko hilo. Hata kama, kwa sababu yoyote ile, hatafuata ushauri huu, ingefaa Dk. Willibrod Slaa na Profesa Ibrahim Lipumba wakatoa tamko linalozingatia ushauri huu.
Edwin Mtei. (Mwenyekiti Mstaafu na Muasisi wa CHADEMA)
Mzee Mtei,
..kwanza shikamoo.
..naomba nitofautiane kidogo ktk haya mapendekezo yako.
..katika harakati hizi za uchaguzi JK ana hadhi sawa kabisa na ile ya Prof.Lipumba na Dr.Slaa.
..vyama vya upinzani mtakuwa mnajiangusha wenyewe mkianza kumchukulia JK kama yeye ni kiongozi, na wagombea wenu ni waongozwa, ktk suala zima la kushughulikia tatizo lilijitokeza mbele yetu.
..kinachotakiwa kufanyika ni hawa wagombea kukutanishwa chini ya usimamizi wa watu wenye busara na wanaoheshimika na jamii ya wa-Tanzania. katika mkutano huo woote watambuliwe kwamba wana hadhi sawa, yaani ni wagombea wa kiti cha Uraisi wa Jamhuri.