Elections 2010 Pendekezo Jepesi: Wagombea Urais wakutane kabla hatujaenda shimoni!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Mwelekeo wa hali ya uchaguzi unasikitisha kidogo. Matukio ya vurugu za hapa na pale unanifanya nitamani kuwa wagombea wa Urais wa kianzia na Kikwete wakutane ili kulipa taifa picha ya umoja katika tofauti. Watoe kauli ya pamoja ya kuwakata wanachama wao na mashabiki kutotumia nguvu na wale wenye vikundi vya ulinzi wawatulize makada wao. Vinginevyo, tujiandae kulipa gharama kubwa zaidi. Wafanye mapema
 
Yap.Point hili wazo ni baaaab kubwa nafikiri hili laweza kusaidia fujo zisitokee maana hali ilivyo ni tete.
 
Wasije chapana vibao lakini..... Nani atakuwa mpatanishi? Napendekeza maaskofu na mashehe kupitia taasisi zao wateue. TEC, CCT na wale wapentekoste na waislamu wote wakutane na wagombea watatu wa juu then Lewis Makame awe chairman. Litoke neno hapo..... Nisingependa Kinana au Baregu pale..... Asante
 
ccm hawawezi kukubali, kwa asilimia kubwa wana tanataka kutumia advantage ya fujo ili mambo yao yaende, ni point nzuri anyway
 
Wasije chapana vibao lakini..... Nani atakuwa mpatanishi? Napendekeza maaskofu na mashehe kupitia taasisi zao wateue. TEC, CCT na wale wapentekoste na waislamu wote wakutane na wagombea watatu wa juu then Lewis Makame awe chairman. Litoke neno hapo..... Nisingependa Kinana au Baregu pale..... Asante

Hao maaskofu na mashehe wenyewe wamesha vishwa UDINI saivi,sijui tunapo elekea God forbid what i am thinking of
 
Kwa mtazamo wa CCM hakuna vurugu yoyote mpaka sasa, ndio maana wanaishia kupiga kelele eti wapinzani wanatoa kauli za kumwaga damu....
 
Vinywa vya viongozi waliopo madarakani vimekuwa vikitumika kueneza siasa chafu na za uhasama. Wakati wao wanasema kuwa vyama vya upinzani vinataka kumwaga damu kama mtaji wa kuingia ikulu, wao wanakata watu mapanga (sijui kama huu ni kwao ni umwagaji wa maji au ni nini?) na labda unatumiaka kama mtaji wa kukimbia ikulu. Ni vizuri ccm wakajua kuwa wao ndio watakaoipeleka nchi pale pasipotatakiwa endapo wataendelea kufikiri kuwa ndio pekee wenye hata miliki ya kuongoza nchi yetu. Tanzania ni yetu sote na tunafursa ya kujichagulia viongozi tunaowataka na sio wanaotakiwa na watawala, matajiri na watu wachache ambao wamekuwa wakifaidika na mfumo uliopo.

Ni vizuri wagombea hawa wakakutana na kuwa na mkutano wa pamoja utakaowashirikisha pia wadau wa Amani kama alivyofanya juzi IGP Mwema kwa ajili ya mustakabali mwema wa nchi yetu. Huko tuendako kunatisha kwa hali hii!
 
Mwelekeo wa hali ya uchaguzi unasikitisha kidogo. Matukio ya vurugu za hapa na pale unanifanya nitamani kuwa wagombea wa Urais wa kianzia na Kikwete wakutane ili kulipa taifa picha ya umoja katika tofauti. Watoe kauli ya pamoja ya kuwakata wanachama wao na mashabiki kutotumia nguvu na wale wenye vikundi vya ulinzi wawatulize makada wao. Vinginevyo, tujiandae kulipa gharama kubwa zaidi. Wafanye mapema

Mzee Mwanakijiji,

Nakushuru kwa pendekezo lako linaloonyesha ukomavu wa siasa zako, uzalendo, mapenzi na huruma kwa nchi yetu na watu wake. Ni jambo muhimu sana kwamba kiongozi aliyeko madarakani sasa, yaani Rais Kikwete aongoze katika tamko hilo. Hata kama, kwa sababu yoyote ile, hatafuata ushauri huu, ingefaa Dk. Willibrod Slaa na Profesa Ibrahim Lipumba wakatoa tamko linalozingatia ushauri huu.

Edwin Mtei. (Mwenyekiti Mstaafu na Muasisi wa CHADEMA)
 
Jk kama rais wa sasa anajukumu la kusimama na kukemea hili pasi hawa wagombea kukutana. si suala la compromise kwa sasa. Otherwise wenyeviti wote wa vyama ama wasemaji wao wasimame kukemea. By the way NEC sijui kazi yao nini? si wawafute kwenye uchaguzi.
 
Mzee Mwanakijiji,

Nakushuru kwa pendekezo lako linaloonyesha ukomavu wa siasa zako, uzalendo, mapenzi na huruma kwa nchi yetu na watu wake. Ni jambo muhimu sana kwamba kiongozi aliyeko madarakani sasa, yaani Rais Kikwete aongoze katika tamko hilo. Hata kama, kwa sababu yoyote ile, hatafuata ushauri huu, ingefaa Dk. Willibrod Slaa na Profesa Ibrahim Lipumba wakatoa tamko linalozingatia ushauri huu.

Edwin Mtei. (Mwenyekiti Mstaafu na Muasisi wa CHADEMA)

Mzee wetu,

Ahsante kwa hilo nadhani wewe unayo nafasi nzuri kwa Dr Slaa kumuomba awe wa kwanza hata kama wengine hawatafanya kwani tutakuwa tumeonyesha njia.
 
Kwa mtazamo wa CCM hakuna vurugu yoyote mpaka sasa, ndio maana wanaishia kupiga kelele eti wapinzani wanatoa kauli za kumwaga damu....
Ndugu yangu kama huna taarifa basi nikwambie tu kuwa CCM kule Hai mkoani Kilimanjaro wameteka mtu na kupasua vioo vya magari ya CHADEMA. Unataka kusema hawa ni wafuasi wa nani?
 
Mwelekeo wa hali ya uchaguzi unasikitisha kidogo. Matukio ya vurugu za hapa na pale unanifanya nitamani kuwa wagombea wa Urais wa kianzia na Kikwete wakutane ili kulipa taifa picha ya umoja katika tofauti. Watoe kauli ya pamoja ya kuwakata wanachama wao na mashabiki kutotumia nguvu na wale wenye vikundi vya ulinzi wawatulize makada wao. Vinginevyo, tujiandae kulipa gharama kubwa zaidi. Wafanye mapema

Kitu wanachi wanatakiwa kufahamu ni kuwa tarehe 1/11/2010, itabidi warudi kwenye familia zao kama kawaida na wakati huo hakutakuwa na mikusanyiko kama iliyopo sasa hapa ndipo kila mtu atavuna alichopanda kwani hawa wagombea hawatakuwa nao tena.
 
Kikwete hatakubali. Dawa ni maandamano...

Washauri wa jmk (shabibu/green guards kinana, makamba, mnajimu na mnadhimu mkuu) si wazuri hawataruhusu ushauri huo wao hawana uchungu na watz lengo lao kubwa ni ushindi kwa gharama yeyote isitoshe Utz wao umelenga mafao zaidi, jmk anayasikia watz kukatwa mapanga mbona hajakemea wala shimbo hakumsema? Vyema jmk apumzike uprezidaa kazi ngumu na imemuelemea kiwango cha kutisha
 
Wazo muhimu sana Mzee Mwanakijiji. Taifa letu linatakiwa kuwa Taifa moja hata mara baada ya uchaguzi. Naona kama tumesahu hilo. Tumeanza kugawana kwa udini, ukabilana uchama. Na hii inaonyesha uongozi legelege. Tutaishia kulia kama waisraeli, waliokuwa wanakumbuka sayuni kama tutaiharibu hii amani.
 
Itakuwa kiini macho, ukumbuke at this point problem is not so much about jk rather wanamtandao ambao sasa hana control nao
 
Itakuwa kiini macho, ukumbuke at this point problem is not so much about jk rather wanamtandao ambao sasa hana control nao
 
Wasipokutana sasa wasije kujikuta wanaomba wapatanishi wa kuwakutanisha baada ya uchaguzi kama ilivyokuwa Kenya kati ya Mwai na Rais. Kikwete kwa miaka yake mitano hajawahi kukaa na kuzungumza kwa pamoja uongozi wa vyama vya upinzani kuhusu masuala ya kitaifa lakini historia ina tabia mbaya sana; yaani kutukumbusha!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom