Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,023
- 144,381
Utaratibu wa kutumia kura ya maoni ili kufanya uamuzi wa jambo lenye maslahi kwa taifa sasa hauna budi kutumika kuamua kama tuna haja ya kuendelea kuwa na serikali hii ya awamu ya nne.Kwa jinsi mambo yanavyokwenda hapa nchini na muda uliobaki ni hatari sana kuendekea kuvumilia watu walioshindwa kuwajibika.Ni bora tukachukua tahadhari mapema kuliko kuchelewa au kutokuchukua tahadhari kabisa.
Iwapo katika kura hiyo ya maoni asilimia zaidi ya 80% wakiunga mkono pendekezo la kuitaka serikali ikae pembeni basi serikali iwajibike.Sisi ndio waajiri na sisi ndio tunapaswa kufukuza.
Bunge ndio limepewa mamlaka kikatib kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali lakini nani ana imani na bunge letu kwa jambo kama hili?Tuendelee kuangamia tukisubiri bunge kibogoyo na lisilojua wajibu wake?
Na ikiwezekana utaratibu huu uwe wa kikatiba , kila raisi awe anapigiwa kura ya maoni katikati ya kipindi chake cha utawala au hata pale inapobidi ili kuleta uwajibikaji na si kufanya nafasi ya uraisi kama ni cheo cha kifalme.Mtu kashindwa basi aondoke sio nchi inayumba naye anayumba nayo huko amengangania usukani.Huu ni uendawazimu!