Paul Makonda awajibu wanaosema anafanya majukumu yasiyo yake, asema fanya yako nami nafanya yangu

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,343
9,770
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Paul Christian Makonda Katibu wa itikadi , uenezi na mafunzo wa CCM Taifa siku ya jana akihutubia ma elfu kwa Malaki ya wananchi mkoani katavi amewajibu kwa ujasiri na kwa kujiamini kama Simba awapo mbugani wale wanaosema anaingilia na kufanya majukumu yasiyo muhusu.huku akishangiliwa na wananchi waliofurika kama mchanga wa bahari amesema amekuwa akichungulia kwenye mtandao wa wasapu na kuona wengine wakisema hayo.

Amejibu kwa kusema kuwa fanya yako nami nifanye yanguuuu,amesema CCM Ndio iliyoomba kura kwa wananchi na hivyo inawajibu na jukumu la kuwasikiliza na siyo kuwaacha wakiteseka ,kuhangaishwa na kuzungushwa na watumishi wa umma katika kupata haki zao.ambapo unakuta mwingine anaambiwa mara njoo kesho mara kesho kutwa mara faili limepotea au halionekani.amesema chama cha Mapinduzi kikipata kero chenyewe ni kumalizana hapo hapo.jambo lililopelekea mafuriko ya watu waliohudhuria kulipuka kwa shangwe, nderemo,vifijo na furaha kumshangilia Mheshimiwa Paul Makonda ambaye anaitwa kwa sasa mtetezi ,sauti na kimbilio la wanyonge.

Amesema kuwa CCM haiwezi kuwavumilia watumishi na viongozi wazembe,wavivu na Wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao na kupelekea wananchi kuichukia serikali na chama .amesema kuwa chama hakipo tayari kuona Mheshimiwa Dr Samia Suluhu Hasssan akienda kuomba kura kwa kupiga magoti kwa kuwa tu kuna watu wameshindwa kufanya kazi zao vizuri kuhudumia wananchi.

Nami nasema Mheshimiwa Makonda chapa kazi ,songa mbele kama jeshi lililo vitani.wewe ni mshindi katika mioyo ya watanzania. Watu wanataka kusikilizwa.watu wamebeba maumivu na mizigo katika mioyo yao ambayo wamezunguka nayo bila kupata msaada kutokana na kuzungushwa sana .sasa wewe umekuja kama mkombozi wao na tumaini jipya katikati ya giza.wasikilize watu na wape majibu,wapokee watu na wape tumaini,faraja na furaha katika mioyo yao.

Mama alikuteua kwa kuwa anatambua uwezo na umahili wako wa kiuongozi.songa mbele kwa kishindo na ujasiri kwa kuwa chama kipo nyuma yako na kina matarajio makubwa sana kutoka kwako.kazi unayoifanya kwa sasa inakiheshimisha sana chama chetu.yoyote anayekupiga vita basi ajuwe ni adui wa chama kizima.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
IMG-20240202-WA0004.jpg
IMG-20240114-WA0016.jpg
 
Ulikuwa #chawawaAkson na sasa
Umekuwa #chawawaPaulo
Sijawahi kubadili msimamo wangu hata siku moja. Mheshimiwa Dr Tulia Acksoni Mwansasu Dada wa Taifa ,msomi wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini na Rais na mwanamke wa kwanza kutoka Tanzania na barani Afrika kuongoza IPU kama Rais naendelea kuwa upande wake ,kumuunga mkono na kumuombea kila la heri.

Mheshimiwa Makonda ni kijana ambaye kila mtanzania mwenye akili Timamu anavutiwa na kuguswa na uchapa kazi wake .hakuna mwenye akili Timamu na anayejitambua anayeweza kushindwa kumuunga mkono Mh Makonda.mimi nimeanza kumuunga mkono Mheshimiwa Makonda tangia akiwa mjumbe wa bunge maalum la katiba baadaye akawa DC na RC.
 
CCM ilipewa kura na wananchi kutokana na kukidhi matarajio ya watanzania.uchaguzi ujao inakwenda pia kuzoa na kubeba kila kitu.
Hata ukiweka jiwe badala ya mtu ndio awe mgombea wa ccm bado hao waliyoipa ridhaa ccm watalichagua hilo jiwe ili kuiridhia ccm,hao ndio wanachi unaowazungumzia.
 
Back
Top Bottom