Paul Makonda ameagiza Waziri wa TAMISEMI kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Pangani Haraka Sana

Huu Ujinga wa kua Kiongozi alafu unasubiri Kiongozi fulan ndo afanye maamuzi, ndo umekua kikwazo kikubwa sana hapa Nchini.


Tena sio tu Makonda.... Inamaana hiyo halmashauri Haina Mwenyekiti? Mkuu wa Wilaya ? Mkuu wa mkoa??.


Ujinga mtupu
Nami ndiyo swali langu sababu pale kuna RC/RAS/DC/DAS hawa wote kazi yao nini?
 
Nami ndiyo swali langu sababu pale kuna RC/RAS/DC/DAS hawa wote kazi yao nini?
Ndio Sababu lazima tukubaliane kwamba, hii Nchii inahitaji watu aina ya Makonda.

Unajua tuna maviongozi meeéngi sana ambayo ni Mzigo, mavivu, yalopata Uongozi Kwa kubebwa .

Mimtu kama hii, inahitaji mtu Mmoja tu Kichaa wa kwenda nao hatua Kwa hatua .
 
Ndio Sababu lazima tukubaliane kwamba, hii Nchii inahitaji watu aina ya Makonda.

Unajua tuna maviongozi meeéngi sana ambayo ni Mzigo, mavivu, yalopata Uongozi Kwa kubebwa .

Mimtu kama hii, inahitaji mtu Mmoja tu Kichaa wa kwenda nao hatua Kwa hatua .
Kwa hiyo hao wengine waendelee kupokea mishahara mikubwa bila kazi?
 
Yeye mwenyewe ni mtu wa kupewa maigizo je ni nani alimtuma atoe maagizo kwa waziri? Yeye ni tarishi tu hana mamlaka ya kumuagiza/kumuamrisha kiongozi yeyote,aache kiherehere.
Chama ndicho kimetoa maagizo na Mheshimiwa Makonda ndiye msemaji wa chama cha Mapinduzi
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Paul Makonda ametoa maagizo ya chama kwa waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa kumsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Pangani Haraka sana.

Hii ni baada ya kukutana na kero nyingi sana katika halmashauri hiyo zilizotolewa na wananchi pamoja na Wafanyabiashara mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa huduma kwa halmashauri lakini hawalipwi pesa zao ,na wanapodai haki zao za kulipwa madai yao wamekuwa wakipewa majibu yasiyoridhisha huku mkurugenzi akijifanya Mungu mtu.

Mheshimiwa Makonda pia ametoa maagizo kwa Mh waziri kuhakikisha kuwa anaunda timu na kuipeleka Pangani kwenda kufanya uchunguzi wa masuala mbalimbali ambayo yamekuwa ni kero na kulalamikiwa na wananchi . Pia amezungumzia suala la kukwama kwa miradi ya serikali na masuala mengine mengi sana yanayochochea chuki ya wananchi kwa serikali yao.

Katika hatua nyingine Ametoa pia kauli nzito sana iliyotetemesha na kuibua shangwe kwa wananchi baada ya kuagiza wakurugenzi wote nchini kushugulikia kero za wananchi ,na kwamba mahali ambapo itaonekana mkurugenzi ameshindwa kutatua kero basi chama hakitasita kutoa maagizo kwa serikali ya kusimamishwa kazi kwa mhusika. Lakini pia amewaagiza wenyeviti wote wa CCM nchini wilaya na mikoa kutoa taarifa juu ya wakuu wa mikoa,wilaya ,wakurugenzi na watendaji wengine wa serikali wanaoshindwa kufanya kazi na kutimiza majukumu yao vizuri ili wachukuliwe hatua.

Ndugu zangu Watanzania kupitia jukwaa hili niliwatahadhalisha sana na kuwasihi sana viongozi wote wa serikali mikoani na wilayani kuwa waanze kufanya kazi na kwenda kwa wananchi kuwasikiliza kero zao.niliwaambia ya kuwa ziara za Mheshimiwa Makonda zitakuwa za moto sana tena sana na zitasomba wengi sana hasa wale wazembe na wanaofanya kazi kwa mazoea na kujifanya miungu watu hawatasalimika wala kuachwa salama katika ziara za Mheshimiwa Makonda. Kwa sababu kila mtu anafahamu ya kuwa Mheshimiwa Makonda hanaga huruma wala subira wala uvumilivu kwa wazembe kazini.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Waziri wa TAMISEMI hajawahi kufika Halmashauri ya Pangani Tanga ateuliwe.​

Mkurugenzi anakakaa Pangani kama Papa.
 
Back
Top Bottom