Paul Makonda aja na wawekezaji 40 toka Uturuki

siwafahamu hao wawekezaji ila kuibeza uturuki ni ukosefu tu wa maarifa
1. ni nchi ya kwanza Ulaya (ukitoa urusi) na ya pili Nato nyuma ya Usa kwa jeshi kubwa.
2. Nchi ya 6 ulaya kiuchumi
3. siku zote ipo top 20 kwa nchi zenye technology kubwa Duniani na ufanyaji research duniani. wana tech kama magari ya kupaa, moja kati ya nchi yenye technology kubwa ya lasers, etc
4. wana mabilionaire wengi kushinda bara zima la Africa combined
Turkey haipo umoja wa Ulaya acha story(EU), Turkey kuwa na jeshi kubwa ni kwa sababu Raid wao Edorgan anaamini katika Authoritarianism (nguvu ya jeshi kiutawala), pili Turkey ina idadi kubwa ya watu (kama 100 million). Lakini Uchumi wa Uturuki vijana wengi hawana ajira kama bongo tu. Uturuki anaweza kuwekeza kwenye Tofari, carpentry, na cherehani, lakini kiuwezo wapo chini sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda leo February 18 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davulaglu, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Prof.Elizabeth Kiondo, Mstahiki Meya kutoka Uturuki, Wawekezaji na Wafanyabiashara zaidi ya 40 wa Uturuki waliokuja kuchangamkia fursa za uwekezaji wa viwanda DSM.

RC Makonda amewahakikishia Wawekezaji hao kuwa Serikali ya Mkoa wa DSM itawapatia ushirikiano wa kutosha wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza ili kutimiza malengo ya Rais Magufuli ya Tanzania ya Viwanda.

RC Makonda amewaeleza wawekezaji hao kuwa DSM inajivunia kuwa na amani na utulivu pamoja na fursa ya uwepo wa Bandari, Uwanja wa Ndege na miundombinu yote muhimu ya kuvutia uwekezaji "nitawapeleka Wawekezaji Kigamboni wakajionee maeneo yaliyotengwa kwa uwekezaji"

Balozi Ali Davutaglu amemuhakikishia RC Makonda kuwa Uturuki itazidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo na wamemualika RC Makonda kwenda kutembelea Uturuki.

Watu kama hawa lazima wapingwe na watu wasiopenda Maendeleo,Viva my bro Makonda

Sent using Jamii Forums mobile app
Waturuki hawa ambao ujenzi wa reli toka dar mpaka moro unawatoa jasho! (Sio wazee wa kazi) Labda watamfute H Rungwe awasaidie kununua korosho.
 
Tusipende kukuza na kushangilia mambo yasiyokuwa na msingi.

Hivi unajua ni wageni wangapi wamewahi kuja Tanzania na kutajwa kuwa ni wawekezaji? Na je, waliwekeza?

Mimi mwenyewe kwa niaba ya kampuni, mwakajana nimetembelea nchi 11 kwaajili ya kuangalia fursa za uwekezaji. Na katika nchi hizo, nilikutana na makamishna, mawaziri, wakuu wa Polisi na majeshi, na nchi mojawapo nilikutana pia na Rais.

Lakini baada ya kutembelea nchi 11, tutawekeza katika nchi 1 tu. Mwekezaji kufika nchini haina maana kuwa atawekeza. Unapotaka kuwekeza, tayari una taarifa fulani za msingi, mbaya na nzuri. Unapoitembelea nchi fulani, unataka kujiridhisha juu ya yale unayoyajua.

Hakuna mwekezaji makini anayewekeza nchi yoyote kwa kuangalia kuwa eti kuna kiongozi fulani au kiongozi amemweleza kuwa ni mahali pazuri pa kuwekeza. Makampuni mengi yana vigezo vyake, tunaita Selection Criteria. Nchi ikivipita hivyo, inakuwa katika list ya nchi favorable kwa uwekezaji japo si lazima ukawekeze.

Hawa wawekezaji wametembelea Tanzania. Ndiyo kitu cha msingi. Kama watawekeza, subiri watakapokuja kuwekeza. Wakati wa JK yaliwahi kuja makundi mbalimbali ya wawekezaji, baadhi ya makundi yalikuwa na wawekezaji zaidi ya 200, halafu hakuna hata mmoja aliyerudi kuja kuwekeza Tanzania.

Ukitaka uvutie wawekezaji mambo yafuatayo ni ya msingi kuliko yote:

1) Uwe na stable legal system
2) Uwe na stable, consistent, friendly, conservative fiscal regime
3) uwe na non-compromised Rule of Law

Hivyo ni vigezo vikuu, na vya jumla kwa wawekezaji wote, halafu vinafuata vigezo vya kisekta, na kisha vigezo specific to the company.

Hakuna mwekezaji ambaye atakwenda mahali ambapo sheria, kodi na taratibu zinabadilika kila kunapokuwa na mabadiliko ya uongozi au kila kikao cha Bunge.

Utafanyaje projections zako za miaka 10 au 20 kama kila Rais anayekuja anabadilisha kila kitu, kila kikao cha Bunge sheria zinabadilika.

No way. Tutabakia kuwa nchi ya wachuuzi. Nchi ya kuuza bidhaa zinazotengenezwa toka mataifa mengine. We import commodities, we export employment.
 
Tatizo nini Dangote kaajiri wazungu na wahindi kwenye viwanda vyake, mabasi ya Scandinavian yalikuwa Na meneja mzungu toka ulaya aliyekuwa akiiendesha taabu iko wapi?
Google Calvin Klein ni nani inaonekana humfahamu. Hakuna hoja eti ameajiriwa na waturuki. Ile brand ni ya wamarekani nukta
 
Kwa hiyo unataka kutuambia nini mkuu?
Tusipende kukuza na kushangilia mambo yasiyokuwa na msingi.

Hivi unajua ni wageni wangapi wamewahi kuja Tanzania na kutajwa kuwa ni wawekezaji? Na je, waliwekeza?

Mimi mwenyewe kwa niaba ya kampuni, mwakajana nimetembelea nchi 11 kwaajili ya kuangalia fursa za uwekezaji. Na katika nchi hizo, nilikutana na makamishna, mawaziri, wakuu wa Polisi na majeshi, na nchi mojawapo nilikutana pia na Rais.

Lakini baada ya kutembelea nchi 11, tutawekeza katika nchi 1 tu. Mwekezaji kufika nchini haina maana kuwa atawekeza. Unapotaka kuwekeza, tayari una taarifa fulani za msingi, mbaya na nzuri. Unapoitembelea nchi fulani, unataka kujiridhisha juu ya yale unayoyajua.

Hakuna mwekezaji makini anayewekeza nchi yoyote kwa kuangalia kuwa eti kuna kiongozi fulani au kiongozi amemweleza kuwa ni mahali pazuri pa kuwekeza. Makampuni mengi yana vigezo vyake, tunaita Selection Criteria. Nchi ikivipita hivyo, inakuwa katika list ya nchi favorable kwa uwekezaji japo si lazima ukawekeze.

Hawa wawekezaji wametembelea Tanzania. Ndiyo kitu cha msingi. Kama watawekeza, subiri watakapokuja kuwekeza. Wakati wa JK yaliwahi kuja makundi mbalimbali ya wawekezaji, baadhi ya makundi yalikuwa na wawekezaji zaidi ya 200, halafu hakuna hata mmoja aliyerudi kuja kuwekeza Tanzania.

Ukitaka uvutie wawekezaji mambo yafuatayo ni ya msingi kuliko yote:

1) Uwe na stable legal system
2) Uwe na stable, consistent, friendly, conservative fiscal regime
3) uwe na non-compromised Rule of Law

Hivyo ni vigezo vikuu, na vya jumla kwa wawekezaji wote, halafu vinafuata vigezo vya kisekta, na kisha vigezo specific to the company.

Hakuna mwekezaji ambaye atakwenda mahali ambapo sheria, kodi na taratibu zinabadilika kila kunapokuwa na mabadiliko ya uongozi au kila kikao cha Bunge.

Utafanyaje projections zako za miaka 10 au 20 kama kila Rais anayekuja anabadilisha kila kitu, kila kikao cha Bunge sheria zinabadilika.

No way. Tutabakia kuwa nchi ya wachuuzi. Nchi ya kuuza bidhaa zinazotengenezwa toka mataifa mengine. We import commodities, we export employment.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga tu. Wizara zinazohusika na uwekezaji ziko wapi? Meya wa jiji yuko wapi? Makonda ana uwezo gani wa kugawa maeneo ya uwekezaji?
Cheap politics from empty heads! USA itabaki juu mawinguni.
 
Dogo anayo mema yake mengi tu tatizo huwa anaongea kwanza halafu anafikiria baadae.

Inabidi aachane na hiyo tabia ili ajipunguzie idadi ya wasiomuelewa.
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda leo February 18 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davulaglu, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Prof.Elizabeth Kiondo, Mstahiki Meya kutoka Uturuki, Wawekezaji na Wafanyabiashara zaidi ya 40 wa Uturuki waliokuja kuchangamkia fursa za uwekezaji wa viwanda DSM.

RC Makonda amewahakikishia Wawekezaji hao kuwa Serikali ya Mkoa wa DSM itawapatia ushirikiano wa kutosha wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza ili kutimiza malengo ya Rais Magufuli ya Tanzania ya Viwanda.

RC Makonda amewaeleza wawekezaji hao kuwa DSM inajivunia kuwa na amani na utulivu pamoja na fursa ya uwepo wa Bandari, Uwanja wa Ndege na miundombinu yote muhimu ya kuvutia uwekezaji "nitawapeleka Wawekezaji Kigamboni wakajionee maeneo yaliyotengwa kwa uwekezaji"

Balozi Ali Davutaglu amemuhakikishia RC Makonda kuwa Uturuki itazidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo na wamemualika RC Makonda kwenda kutembelea Uturuki.

Watu kama hawa lazima wapingwe na watu wasiopenda Maendeleo,Viva my bro Makonda

Sent using Jamii Forums mobile app
Unamaanisha Bashite ama sijakuelewa vizuri!
 
kwa nini ashee na wewe technology bure bure, halafu iweje, uwe mshindani wake ??

ahamishe viwanda vyake vya Calvin Kline kuja Tanzania, atakuwa mjinga kiasi gani kuua solo la ajira ya kwao kukupa wewe bure bure kitu ambacho wamekipigania udi na uvumba kukipata kutoka makampuni hayo ya nguo??

tumekalia ma mentality ya kutegemea kusaidiwa bure bure tu, wewe Muafrika we nani???? una mchango gani kwa dunia hadi waku favor maendeleo bure bure tu??

mkuu, kwanza kabisa hujanielewa nilichosema, umeniuliza kwanini a share technology bure bure, lakini mimi sijui makubaliano yao na makonda mimi nimeongea tu uwezekano na sina uhakika, hayo ni mawazo yangu na sio terms za mikataba au makubaliano

pia mkuu unaonekana una uelewa mdogo wa viwanda, hujasikia kampuni za ujerumani za magari zinaweka viwanda hapo rwanda ? yaani assembly plant ? unajua kwamba china imepeleka viwanda vya kutengeneza tv za star times africa kusini ?

ni hivi , hao wakileta viwanda hapa bongo watapata faina maana raw materials ipo hapA, kodi ni ndogo kuliko kwao na transportation cost ni ndogo yani utengeneze jeans ulaya ije iuzwe bongo huoni ni costful ? , pia sijamaanisha eti viwanda vitakufa huko kwao, huku bongo itakua ni branch tu,nikukumbushe tu kwamba hata hapa tanzania mzee mengi ali sign makubaliano na kampuni ya korea ya utengenezaji magari kiwekwe kiwanda cha gari hapa bongo ila haimaanishi kinakufa huko korea

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
unajua uturuki wana viwanda vikubwa vya nguo ? imagine waki share technology na sisi au wanunue pamba yetu na watengeneze nguo zao hapa
kelvin clain jeans zinatengenezwa turkey usiwadharau

Sent from my iPhone using JamiiForums

Pamba ipi mtakayowauzia wakati wakulima wanaachana na kulima pamba kutokana na serikali kuvuruga mfumo uliozoeleka wa pembejeo na masoko?
 
mkuu, ni wakulima wote wameacha kulima ?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
mkuu, ni wakulima wote wameacha kulima ?

Sent from my iPhone using JamiiForums

Of course kuna wanaolima, lakini hao walioacha wanasababisha uzalishaji kupungua (na nina uhakika na hili); hakuna ginnery nchi hii inayo-operate at least 40% ya capacity. Pamba inayozalishwa haitoshi hata kukidhi mahitaji ya ndani, ya kuuzia Waturuki (kama anavyoshauri niliemjibu) itatoka wapi?
 
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda leo February 18 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davulaglu, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Prof.Elizabeth Kiondo, Mstahiki Meya kutoka Uturuki, Wawekezaji na Wafanyabiashara zaidi ya 40 wa Uturuki waliokuja kuchangamkia fursa za uwekezaji wa viwanda DSM.

RC Makonda amewahakikishia Wawekezaji hao kuwa Serikali ya Mkoa wa DSM itawapatia ushirikiano wa kutosha wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza ili kutimiza malengo ya Rais Magufuli ya Tanzania ya Viwanda.

RC Makonda amewaeleza wawekezaji hao kuwa DSM inajivunia kuwa na amani na utulivu pamoja na fursa ya uwepo wa Bandari, Uwanja wa Ndege na miundombinu yote muhimu ya kuvutia uwekezaji "nitawapeleka Wawekezaji Kigamboni wakajionee maeneo yaliyotengwa kwa uwekezaji"

Balozi Ali Davutaglu amemuhakikishia RC Makonda kuwa Uturuki itazidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo na wamemualika RC Makonda kwenda kutembelea Uturuki.

Watu kama hawa lazima wapingwe na watu wasiopenda Maendeleo,Viva my bro Makonda

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ni yeye aliyewaleta?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom