Pato la Wastani Rwanda $583, Tanzania $434

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,409
9,183
Msaada wanauchumi. Pamoja na rasilimali nyingi nchini, pato la wastani Rwanda ambayo ni landlocked na isiyokuwa na utajiri mkubwa wa madini linazidi pato la wastani la mtanzania kwa $200 kwa mwaka. Nini chanzo cha mafanikio ya kiuchumi ya Kigali?
 
Ukiwa na mke na mtoto mmoja ukapokea mshahara laki 3, wastani wa pato kwa mtu ni 100k, ukiongeza watoto 2 kwa mshahara huo wastani unakua 60k.
Salaam.
 
Sisi yunangoja bure au sana kuuza mitumba au kuwa wamachinga
Tufanye kazi
Wenggi wetu tuna mashamba vijijini tumeyaacha na kuja mjini kutandaza chupi bararabani
 
Wao ni wachache vijisenti vya Bakharessa tu wote wanaonekana matajiri, ni ujumlisho wa mahesabu tu.

ina maana familia ndogo ambayo kila mmoja anapata kipato cha 583 ni maskini kuliko familia kubwa ambayo kila mmoja wake anapata 434? Kajipange upya.
 
Ukiwa na mke na mtoto mmoja ukapokea mshahara laki 3, wastani wa pato kwa mtu ni 100k, ukiongeza watoto 2 kwa mshahara huo wastani unakua 60k.
Salaam.

Kama tatizo/suala ni idadi tu ya watu basi China na India zingekuwa maskini zaidi
 
takwimu ni shida Tanzania. Kipato halisi hakiwezi kujulikana wakati fedha nyingi hazipitii benki ili kukwepa kodi, watu maofisini wanalipwa kwa vocha kukwepa kodi na nssf, fedha zinapelekwa uswiss, nyingine zinaliwa na wachina na consultantsb wazungu. uchumi wa bongo ni mkubwa sana per capita inabidi iwe dollar 2,000 ila haujawekwa vizuri tu
 
Ukiwa na mke na mtoto mmoja ukapokea mshahara laki 3, wastani wa pato kwa mtu ni 100k, ukiongeza watoto 2 kwa mshahara huo wastani unakua 60k.
Salaam.

hujaelewa thread.....nanukuu "Pamoja na rasilimali nyingi nchini, pato la wastani Rwanda ambayo ni landlocked na isiyokuwa na utajiri mkubwa wa madini"

argument yako inge-make sense kama Tz ingekuwa na geografia na raslimali sawa na Rwanda kama mtoa mada alivosema, unajua chochote kuhusu uchumi ?nisije nikawa napigia mbuzi guitar......katika uchumi wingi wa watu ni fursa kubwa kwa maendeleo ya uchumi....(kama hao watu wanazalisha) ila kwa mfano wako wa mke na watoto ambao hawazalishi upo sahihi lazima pato lishuke.....na pengine mfano wako unafit kwa tz
 
Wao ni wachache vijisenti vya Bakharessa tu wote wanaonekana matajiri, ni ujumlisho wa mahesabu tu.

unapotosha watu....au huelewi chochote juu ya uchumi....uchache wa watu si hoja.....marekani au china zina watu wangapi?wingi wa watu ni mtaji kiuchumi ila kiushabiki na umbumbu ndo inaonekana kikwazo cha maendeleo....huo ni wingi wa watu tu sijagusa wingi wa raslimali nyingine...u dont need to read economics to know this if u have senses u will see it....
 
Msaada wanauchumi. Pamoja na rasilimali nyingi nchini, pato la wastani Rwanda ambayo ni landlocked na isiyokuwa na utajiri mkubwa wa madini linazidi pato la wastani la mtanzania kwa $200 kwa mwaka. Nini chanzo cha mafanikio ya kiuchumi ya Kigali?

Nong`ona wenywewe wanyarwanda wasikusikie.Hizo hela ni hela za kwenye makaratasi.Hazina uhusiano na maisha halisi ya watu .Tanzania tulikuwa na pato kwa mtu dogo sana wakati wa Nyerere lakini watu walikuwa wanasoma bure,wanatibiwa bure,ajira bwerere kila kona.Saa hii pato la mtanzania kwa hesabu hizo za kipuuzi liko juu maisha ya watu yako chini.Hizo hesabu tuliosomea ujamaa tunaziita hesabu kichaa za mabeberu achana nazo tafsi yake ni pana na siyo rahisi kama ulivyo-conclude.
 
mie uchumi wangu, Prof.Osoro, Prof.Amani, Dr.Mwamba na Dr.Mashindano walisema hata nifanyeje siwezi pata zaidi ya C, ngoja wachumi #1 waje waseme ili tufahamu sababu ni nini?
 
hiyo ni kawaida inatokana na ukubwa wa nchi na wingi wa watu,qatar wananchi wake ndio wenye kipato kikubwa zaidi duniani,qatar na nchi za ulaya au america ipi zaidi,huo ni mfano2
 
Wacha ubishi pato la wastani huongezeka kadri uzalishaji unavyoongezeka na hupungua kadri idadi ya watu inavyoongezeka if other things constant ndio maana China ni nchi ya pili kwa utajiri ya kwanza Marekani,China imekuwa ya pili baada ya kuipiku Japan miaka ya karibuni lakini china haipo ata kwenye top 5 ya dunia ya nchi zenye pato la wastani kubwa,hivyo basi yawezekana Rwanda imejitahidi kiuzalishaji lakini usipinge uwezekano wa uthibiti kama si idadi ndogo ya watu iwabebe kwenye par capital income,pia fahamu Rwanda wanamatatizo fulani ya ukosefu wa amani, uhuru, starehe zilizobanwa na huwezi kujiachia kama Bongo, kwetu hadi Rais anatukanwa lakini ametulia nenda Rwanda uone,hivyo basi hiyo figure haiakikishi maisha bora inategemea na mambo mengi kama haya niliyoyataja.
Kama tatizo/suala ni idadi tu ya watu basi China na India zingekuwa maskini zaidi
 
1961 wastani wa pato la Mtanganyika lilikua juu ya china, tuliongeza ukubwa wa familia kufurahia uhuru mpaka miaka ya 90 tulipoanza kuiona nyota ya kijani. Tafuta wastani wa kaya sensa ya 88 kama si watu 7 wakati china 3.
Kama tatizo/suala ni idadi tu ya watu basi China na India zingekuwa maskini zaidi
 
Ukiwa na mke na mtoto mmoja ukapokea mshahara laki 3, wastani wa pato kwa mtu ni 100k, ukiongeza watoto 2 kwa mshahara huo wastani unakua 60k.
Salaam.

vipi kama tukikuongezea mshahara(rasilimali) then ukaongezewa na watoto(population)!
 
Nafikiri ni Zeze la umeme. Hamna nchi ya Afrika isiyo na madini, murunda, pindula-dhahabu, kigemi-almasi, biumba-bati, usisahau Goma yao pia. Hesabu ya kawaida, wastani wa pato inaathiriwa na namba ya chini 'idadi ya watu' ndio maana wastani wa pato uholanzi ni mkubwa kuliko labda kuliko marekani nchi tajiri duniani.
hujaelewa thread.....nanukuu "Pamoja na rasilimali nyingi nchini, pato la wastani Rwanda ambayo ni landlocked na isiyokuwa na utajiri mkubwa wa madini"

argument yako inge-make sense kama Tz ingekuwa na geografia na raslimali sawa na Rwanda kama mtoa mada alivosema, unajua chochote kuhusu uchumi ?nisije nikawa napigia mbuzi guitar......katika uchumi wingi wa watu ni fursa kubwa kwa maendeleo ya uchumi....(kama hao watu wanazalisha) ila kwa mfano wako wa mke na watoto ambao hawazalishi upo sahihi lazima pato lishuke.....na pengine mfano wako unafit kwa tz
 
Ongezeko la mshahara 'uchumi' kwa wastani % uwe juu ya ongezeko la wastani % watoto 'population' = uchumi wa kaya umekua.
vipi kama tukikuongezea mshahara(rasilimali) then ukaongezewa na watoto(population)!
 
Back
Top Bottom