Passport: Maombi ya Hati ya Kusafiri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wapendwa naomba kuuliza,,,ukiwa na mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 2 na unataka kusafiri nae pia unahitaji kumkatia passport?maana mimi nina passport yangu ya miaka 10 na bado miaka 6 ndo ita expire na ninahitaji kusafiri na mtoto nje ya Afrika na bado sijajua nifanyeje,,msaada tafadhali
Miez miwili hapana akiwa na zaid ya miaka 2 ndo utamkatia
 
Hodi wana jamvi, mwaka jana mwezi wa saba, Niliomba paspoti huku mkoani napoishi, madhumuni ya paspoti hiyo ilikuwa nikwa ajili ya kwenda masomoni. Niliambatanisha kila document iliyotakiwa, na nilichukuliwa hadi alama za vidole lakini mwisho wa siku nikaambulia patupu. Nilijaribu kufuatilia sana wakawa wananiambia bado wanafuatilia taarifa zangu hadi deadline ya kwenda kuripoti chuoni ikapita, nikakosa chuo na sponsorship niliyokuwa Nimepewa. Na walinikatisha tamaa waliposema paspoti hadi kuipata itachukua 2 months.
Sasa mwaka huu nimepata tena nafasi hiyo. Nahitaji kuja Dar moja kwa moja nichukulie huko. Please Naomba mwenye kujua utaratibu wa zaidi ya nilioutumia mwanzo anijuze.
Andaa vyeti vya kuzaliwa vyako na wazazi wako, andaa Tsh50,000/-. Kwa kuepusha usumbufu wakati wa mahojiano ya kuthibitisha uraia wako basi jiandae chukua na living certificates za elimu ya sekondari kuanzia kidato cha nne. Usisahau kupiga picha za passportsize za background ya blue.
 
Andaa vyeti vya kuzaliwa vyako na wazazi wako, andaa Tsh50,000/-. Kwa kuepusha usumbufu wakati wa mahojiano ya kuthibitisha uraia wako basi jiandae chukua na living certificates za elimu ya sekondari kuanzia kidato cha nne. Usisahau kupiga picha za passportsize za background ya blue.
Hivi renewal ikoje yangu inaisha mwezi july na sitaki ifike huko nahisi nikitoka itasumbua kurenew
 
binadamu yoyote anaepumua anapaswa kutumia passport yake haijalishi kazaliwa leo asubuhi au la.vya kutumia passport ya mzaz vimepitwa na wakati.
 
Hivi kwanini Passport ikiexpire/ikijaa wakati unarenew unapewa Passport yenye namba mpya kabisa? Kwa nini namba isiwe ilele kama zilivyo documents nyingine kama TIN, Driving Licence etc?
 
niliahirisha baada ya kuambiwa nilete cheti cha babu yangu ,nikawaza babu alizaliwa mwaka 1902,hiki cheti chake nakipataje nikachukua uamuzi wa kuahirisha kwanza ,kwa sasa sijajua endapo urasimu ni ule ule au la.
 
niliahirisha baada ya kuambiwa nilete cheti cha babu yangu ,nikawaza babu alizaliwa mwaka 1902,hiki cheti chake nakipataje nikachukua uamuzi wa kuahirisha kwanza ,kwa sasa sijajua endapo urasimu ni ule ule au la.
Hakuna cheti cha babu.
Ni
1. Barua ya ualiko
2. Barua ya maombi ya pass
3. Cheti cha kuzaliwa wewe na baba/mama yako
4. Passport size 5.
5. Barua ya serikalini ya mtaa.

Basi
 
Mimi ni raia wa Tanzania ambae kwa sasa nipo nchini Ureno, nimepoteza paspoti yangu iliotolewa mwaka 2005(hizi mpya), jambo linalonitatiza ni kuwa hawa balozi wetu hawataki kunisaidia!

Wanasema lazima niende Paris ili nikafanye maombi mapya na kuchukuliwa alama za vidole, lakini mwaka 2005 nilichukuliwa finger print, Je ni lazima kila mtu anapotaka passpoti achukuliwe alama? Huu si mchezo umekuwa kwa maana wenzetu wakichukuliwa basi huwekwa kwenye data base. Kuna msaada gani wa kisheria mnaoweza kunipa wenzangu??

============
============

Yapo mambo ambayo huwaumiza watu vIchwa yumkini yakiwa ni mambo madogo na ya kawaida. Tatizo mara nyingi huwa ni taarifa. Taarifa zikimfikia mtu ndipo huhisi jambo ambalo alikuwa halijui kuwa ni jepesi.
Lakini kabla ya taarifa mtu huendelea kufikiria jambo hilo kwa ugumu.

Katika kipindi kama hiki kuwa na kitu kama pasipoti si jambo la anasa au ufahari tena isipokuwa ni jambo ambalo limeishaingia katika matumizi ya kawaida ya kila siku ya walio wengi. Hii ni kutokana na kukua kwa biashara za kimataifa, mawasiliano, utalii,usafirishaji na kila kitu ambacho husababisha watu kutoka nchi moja hadi nyingine.

Kwasasa kuwa na pasipoti hata kama huna safari ya hivi karibuni ni jambo muhimu sana. Yumkini usisubiri ikutokee safari ya ghafla halafu ndio uanze kukimbizana na pasipoti. Pasipoti inayo manufaa mengi lakini moja ni kuwa pasipoti ni mali kama mali nyingine. Pasipoti inaweza kumdhamini mtu kama mali nyingine inavyoweza kumdhamini mtu.Pasipoti ni amana tena amana ya kuaminika. Ni kutokana na umhimu huu nikaona leo nieleze pasipoti na namna ya kupata pasipoti.

1. PASIPOTI HUOMBWA NA MWOMBAJI LAKINI HUBAKI MALI YA SERIKALI.

Hakuna mtu mwenye umiliki wa kudumu wa pasipoti. Kwa mujibu wa sheria licha ya kuwa pasipoti hutolewa kwa jina na maelezo ya mwombaji,hati hiyo hubaki kuwa ni mali ya serikali. Hii ndio sababu serikali huweza kumnyanganya mtu pasipoti panapo jambo fulani. Ni kwakuwa pasipoti ni mali yake. Wewe mwombaji uliyepewa pasipoti unayo haki ya matumizi na uhifadhi wake lakini mmiliki mkuu ni serikali.

2.ILI KUPATA PASIPOTI UNAHITAJI KUWA NA VITU HIVI.

( a ) Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa kuandikishwa cha mwombaji.Cheti cha kuzaliwa ni hivi vyeti vya kawaida ambavyo hutolewa mahospitalini au mamlaka nyingine baada ya kuzaliwa kwa mtu. Katika kipindi hiki wapo wengine wamekwisapata vyeti vya uraia. Cheti cha uraia chaweza kutumika kama mbadala wa cheti cha kuzaliwa. Pia tumesema hati ya kiapo. Hii hutolewa kwenye ofisi za wanasheria. Mwombaji huwa anaapa pamoja na mambo mengine kuthibitisha kuwa taarifa anazozitoa ni za kweli kwa dhati yake. Pia tukasema vyeti vya uraia wa kuandikishwa. Hivi wanavyo raia wa Tanzania ambao si wa kuzaliwa. Katika kuomba kupata pasipoti nao hutakiwa kuwa navyo.

( b ) Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa kuandikishwa cha
mzazi au wazazi wa mwombaji. Hapo juu tumeona vitu kama hivihivi lakini ilikuwa ni kwa mwombaji wa pasipoti mwenyewe. Hivi hapa sasa ni kwa ajili ya mzazi wa mwombaji. Vile vitu vyote alivyowasilisha mwombaji pale juu ndio vilevile anavyopaswa kuwasilisha mzazi wa mwombaji. Si kwamba mzazi mwenyewe ndio anapeleka vitu hivyo hapana, wewe mwombaji ndio unabeba vitu hivi kwa niaba ya mzazi. Hapa mzazi ni yeyote anaweza kuwa baba au mama.Lengo lake ni kutaka kujua historia fupi ya nasaba ya mzazi wa mwombaji.

( c ) Inahitajika picha ya hivi karibuni ya pasipoti size. Sharti kubwa waliloweka hapa ni kuwa picha hiyo isiwe katika fremu. Fremu hapa si tu ile fremu ya kawaida tuliyoizoea bali pia hata pasipoti kuwa na maringo au mapambo ya kuzungushia pembeni nayo ni fremu kwa maana hii. Pasipoti iwe mnyooko(plain) isiwe na mbwembwe zozote.

( d ) Iwapo mwombaji ana umri wa chini ya miaka kumi na nane (18), wazazi walezi wawasilishe ridhaa ya maandishi. Nyaraka hii ya ridhaa ya maandishi huandaliwa na mwanasheria.Hii ni kusema kuwa utaratibu wa mtu mzima aliyevuka miaka kumi na nane ni tofauti na mtu aliye chini ya miaka hiyo katika kupata pasipoti. Baada ya kukamilisha vitu hivi kama nilivyoeleza basi hatua inayofuata ni kufuata utaratibu huu chini.

3.FOMU ZA MAOMBI HUPATIKANA WAPI.

Ofisi za uhamiaji ndipo zilipo fomu za maombi ya pasipoti. Hii ni popote Dar es salaam au mikoani. Suala la msingi ni kuwa ofisi hiyo iwe ya uhamiaji utapata fomu hizo. Utachukua fomu hiyo utaijaza na baada ya kuijaza itawasilishwa kwa mkurugenzi wa uhamiaji. Aidha suala jingine la msingi ni kuwa fomu hii itawasilishwa sambamba na nyaraka zote zinazotakiwa kama ilivyoelezwa hapo juu.

4.BEI YA PASIPOTI NI KIASI GANI.

Ada rasmi ya kupata pasipoti ni fedha za Kitanzania kiasi cha shilingi 50,000/=( Elfu hamsini tu). Aidha kwakuwa wanasheria ndio hushughulika na kutafuta pasipoti basi bei yao haiingizwi katika ada rasmi ya serikali kama nilivyoieleza hapo juu.

5.UNAWEZA KUOMBWA VIAMBATANISHO VYA ZIADA.

Jambo jingine ni kuwa safari zimeainishwa kwa namna mbalimbali.Ukisoma nyuma ya fomu ya maombi utaliona hili. Kutokana na hilo wakati mwingine waweza kuombwa viambatanisho vya ziada. Hii ni kutokana na utofauti wa safari. Hii ni kusema kuwa yawezekana mwombaji akaombwa viambatanisho viitwavyo viambatanisho &[HASHTAG]#8220[/HASHTAG];maalum&[HASHTAG]#8221[/HASHTAG];. Hivyo basi mtu asishangae kukutana na kitu cha namna hiyo.

MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
Passport inapoisha muda wake, au ukipoteza pasaport alama za vidole ni lazima zichukuliwe kila uendapo kuomba mpya, ku renew au kutaka upewe nyingine baada ya kupoteza, huu ni utaratibu wa serikali haukwepeki hadi hapo watakapo ona kuna haja ya kusitisha kuchukuliwa alama za vidole, hatuna ujanja lazima tifuate utaratibu, tulioko nje hatuwezi kuilazimisha serikali ifanye tunavyotaka ila maoni yanakaribishwa kuiomba serikali ifanye mabadiliko katika sheria na kanuni zake. Akhsanteni.
 
Hakuna cheti cha babu.
Ni
1. Barua ya ualiko
2. Barua ya maombi ya pass
3. Cheti cha kuzaliwa wewe na baba/mama yako
4. Passport size 5.
5. Barua ya serikalini ya mtaa.

Basi
no.3 endapo cheti /vyeti vya wazazi wangu siwezi kuvipata /au walishatangulia mbele za haki .nafanyeje
 
Inategemea na aina ya pasi unahitaji kwa ajili ya safari, maana kuna kama ifuatavyo;
1. Emegency travel document (ETD) ama Shahada ya Safari ya DHARURA imeanishwa nchi unazoruhusiwa kusafiria Yaani KENYA, UGANDA, MALAWI, DRC, RWANDA, BURUNDI, ZAMBIA, &MSUMBIJI
na bei yake ni Tsh. 10,000tu. Fomu zapatikana palepale ofisini unatakiwa kuwa na Picha 3ppt size blue background, cheti cha kuzaliwa cha mwombaji, cha mmoja kati ya wazazi wako, stempu za Tra 2 endapo utatumia viapo, barua kutoka serikali za mtaa.

2. Pasipoti ya Kawaida (ORDINARY PASSPORT) Bei yake ni TSh 50,000tu bila chenga na pasi hii inakuwezesha kusafiri kwenda popote duniani, chamsingi uwe na viambata nilivyovitaja hapo mwanzo na barua ya uthibitisho wa safari yako na ni ndani ya siku 7 (saba) tangu kupokelewa kwa ombi lako unapata pasi yako, na uharaka wa pasipoti yako inategemea udharura wa safari yako na tatizo pia, mfano unaumwa mahututi unatakiwa ukatibiwe nje pasipoti yako inawezekana kuipata siku hiyohiyo.

3. PASI YA AFRIKA MASHARIKI (EAST AFRICAN PASSPORT) Bei yake Tsh 15,000tu na inakuwezesha kusafiri katika nchi wanachama na inakuwezesha kufungua akaunti ya akiba katika nchi wanachama.

Kumbuka ETD haitolewi makao makuu Kurasini na Epukana na Madalali na matapeli nenda moja kwa moja kwa afisa uhamiaji katika sehemu husika hasa ofisi za uhamiaji, pia uwanja wa ndege, bandarini na vituo vya kutokea na kuingilia ni vya uhamiaji, isipokuwa hakuna Pasipoti yeyote inayotolewa katika sehemu tajwa. Itangaze nchi yako kwa kutumia pasipoti ya nchi yako.
Kama wazazi wamefariki hivyo vyeti vyao vya kuzaliwa vina umuhimu gani? Au hapo ina kuwa je?
 
Habar ndugu jamaa na marafiki.
Naitaji kujua taratibu za upatkanaji wa passport ya kusafiria nikimaanisha
*vigezo
*masharti
*Na itatumia siku ngapi.
*Bei gani inagharim
Msaada please...........
 
nimepata nafasi ya training asia leo nahitajika kutuma passport namba kabla ya trh 13 mwezi huu wa sita. aliefanikiwa kupata passport ndani ya siku mbili anipe mwongozo plz
 
Back
Top Bottom