[Parallel Histories Of Histories Israel-Palestine:Side by Side

cassavaleaves

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
1,377
1,716
Wana forum:

Nimekuwa nikufuatilizia debates zinazoendelea ndani ya forum yetu, kwa kile kichoendelea Mashariki ya Kati, hasa kipindi hiki cha vita kati ya Israel na Hamas.

Kilichonisikitisha sana ni hoja za ushabiki ndio nyingi, wengi wetu tunakuja kutetea pasipo kuonyesha kwa nini uko upande huyo , na kwa sababu ipi. Mgogoro huu ni complex, wengi wamejaribu sana kutoa mawazo yao.Mgogoro umebeba kila aina ya mitazamo, dini, utaifa na mitazamo mbali mbali.

Baada tu ya kuangaza mgogoro huu, nimejaribu sana kutafuta vitabu mbalimbali ili niweze kupata narratives za kila upande, hata upe upande nao egemea nisiwe mbumbumbu na kuafuata kama kasuku.

Jana niliagiza Kitabu ambacho Wanazuoni wa Kiyahudi na Wapelistina walikaa pamoja na kujaribu kuandika historia ya mahali kila mtu akionyesha upande wake unavyoungalia mgogoro huo. Kitabu hiki kinaitwa Side By Side: Parallel Histories of Israel-Palestine

Natoa ushauri kama unataka kujifunza tu kuhusu huu mgogoro, na kujua kila upande unavyo itafsri historia na kujenga hoja zake, jipatie hiki kitabu

1708332579181.png


Nadhani ukiweza kupata Kitabu hiki kitasaidia mno kukuelimisha na kukufungua macho kuona Mitazamo ya Israel na Palestina inavyotofautiana na pia katika maeneo mengine kushabihiana.
 
Jina la kitabu...Side By Side : Parallel Histories Of Israel -Palestine! Edited by Sam Adwan, Dan Bar-On, Eyal Naveh, and Peace Research Institute In the Middle East (Prime)
 
asa sisi wavivu itakuwaje!!

Dem boy: Kuna usemi unasema "No Research, no right to speak" ....Mkuu sasa itabidi utegemee Tiktok tu! ......Sana sana huwa inazidi ku reinforce mtazamo wako tu....! Na tatizo lake pia, ni kuwa hata kile unachoakiamini huwa unashindwa kukitetea...

Nimeona wengi katika mijadala hata zile basic facts tu za Mgogoro ni watupu kabisa.

Na sababu ya mimi kukinunua kitabu hiki ni kutaka kujua tu, maana nimeona kuna narratives nyingi ambazo wengi tumepewa misikitini, makanisani hata mashuleni ambazo tayari ziko biased!

Nilifundishwa huko nyuma kusikiliza na kujaribu kuyaelewa mawazo ambayo hata hukubaliana nayo, au kujaribu kujua kwa nini mtu fulani ana mtazamo huo, hii ni katika nyanja zote za maisha na mahusiano.

Hivyo nakuomba ondoa uvivu kidogo inaweza kusaidia katika mijadala inayozidi kujitokeza.
 
Back
Top Bottom