Paracetamol kudhibiti nyoka

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542

Paracetamol: Kwa nini dawa inayotumika kupunguza maumivu inaweza kutumika kuua nyoka?​


Dawa ya Paracitamol

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Serikali ya Marekani inatumia paracetamol, ambayo tunaitumia kupunguza homa kuua spishi ya 'Brown Tree Snake' katika kisiwa cha Guam.
Nchi hiyo imetumia miligramu 80 ya paracetamol kuua nyoka hao kisiwani Guam.
Nyoka hao ambayo huishi kwenye miti hula panya walionaswa kwenye magamba ya miti. Paracetamol ikitumiwa kwa panya kama mtego huua nyoka ndani ya saa chache.
Idara ya Kilimo ya Marekani inatumia vifaa maalum kufuatilia baadhi ya panya ili kubaini ikiwa nyoka wamekufa kutokana na kula paracetamol.

Mapambano ya dhidi ya 'nyoka'​

Marekani iko vitani na Nyoka wa Mti wa Brown, ambaye ana urefu wa mita tatu hivi. Inagharimu dola milioni nane kwa mwaka.
nashangaza kwanini serikali ambayo inastahili kulinda wanayama pori inaua nyoka huyu. Marekani inasema imechukua hatua hiyo kutokana na uharibifu unaofanywa na nyoka huyo.
nyoka aina ya (Brown Tree Snake)

CHANZO CHA PICHA,JAMES STANFORD
Kisiwa cha Marekani cha Guam kipo magharibi mwa bahari ya Pasifiki karibu kilomita 11,000 kutoka eneo la bara la nchi hiyo.
Kisiwa hicho kiko karibi kilomota 2,500 kutika Ufilipino na na kilomita 4,500 kutoka Australia.
Idadi ya nyoka wa mti wa brown katika kisiwa cha Guam imeongezeka mara dufu. Nyoka hao ni tishio kwa aina ya spishiya ndege wa kipekee ambao ni nadra kupatikana.
Marekani inasema spishi tisa ya ndege kati ya 11 wameangamia kutokana na hilo. Kando na hilo maisha ya twiga na popo yako hatarini.
Matatizo ya mara kwa mara ya kupotea kwa nguvu za umeme hutokea wakati nyoka hawa wanaponaswa kwenye nguzo za umeme. Vifaa vya usambazaji wa umeme vimeharibiwa.
Mamlaka ya kawi katika kisiwa cha Guam inakadiria kuwa kukarabati vifa vya umeme umeme mara kwa mara kunasababisha kupotea kwa zaidi ya dola milioni 4 kwa mwaka.
Kutokan na sababu hiz Marekani inajaribu kudhibiti idadi ya nyoka wa kahawia. Kisiwa cha Guam, ambacho ni kidogo kieneo ukilinganisha na mji wa Hyderabad, kinakadiriwa kuwa na zaidi ya nyoka wa kahawi 300,000.
Hata hivyo kampuni kama PETA imelaumiwa kwa kuua idadi kubwa ya nyoka kwa kutumia dawa aina paracetamol.
Kisiwa cha Guam
Kisiwa cha Guam

CHANZO CHA PICHA,FB/VISIT GUAM
Maelezo ya picha,
Nyoka huingia kisiwa cha Guam kupitia meli
Spishi hii ya kipekee ya nyoka ilifika kisiwa cha Guam karibu miaka 70 iliyopita.
Kisiwa cha Guam kilikuwa kambi ya jeshi la Marekani wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Pia iliwahi kuwa chini ya utawala wa Japan wakati mmoja.
Nyoka huyo alifika Guam kupitia meli ya mizigo zinazopitia kisiwa hicho wakati inapokuwa safarini.
Nyoka wa kahwia hupatikana kwa wingi katika nchi kama Australia, Indonesia, na Papua New Guinea. Guam sio makazi yao asilia kumaanisha hakuna maadui wa spishi hiyo ya nyoka katika kisiwa hicho.
Hali ambayo imechangia kuongezeka kwa idadi ya nyioka hao. Ni vigumu kuwaona kwa sababu wanaishi juu ya miti.
Nyoka hao walipokuwa wengi walianza kuvamia spishi za wanyama wanaopatikana naktika kisiwa cha Guam.Kwa hivyo bioanuwai kisiwani humo inaharibiwa sana.

Lengo ni kudhibiti nyoka hao​

Nyoka ya kahawia anayeishi kwenye miti alionekana kwa mara ya kwanza kwenye kisiwa cha Guam mwaka wa 1950. Kisha kufikia miaka ya 1990 wakageuka kuwa shida kubwaa. Hatua zimechukuliwa kudhibiti aina hiyo ya nyoka tangu wakati huo.
Kuwaua kwa kutumia dawa aina ya paracetamol ni moja ya hatua hizo. Lengo la Marekani ni kudhibiti nyoka hao katika kisiwa cha Guam.
Inasema kuwa sio nia yao kumuua nyoka kabisa, lakini kudhibiti idadi yao.
Nchi hiyo inatumai madhara yatakuwa makali ikiwa nyoka huyo atasafiri kutoka kisiwa cha Guam hadi Hawaii au bara la Amerika.
Kwa sababu hawana maadui wa asili huko Marekani, inahofiwa kwamba nyoka wa kahawia wanaweza kuwa wauaji kwa viumbe vingine.
Ndiyo maana Marekani inawafuatilia nyuka hao kwa karibu nyoka ili wasiingie ulimwengu wa nje kupiatia meli na ndege.
Nyoka hao wameangamizwa kabisa katika uwanja wa ndege wa Guam na karibu na bandari. Mamlaka pia inapeleka mbwa wa kunusa waliopewa mafunzo maalum kuwatambua nyoka hao katika viwanja vya ndege.
 
Back
Top Bottom