Ama kweli, dini inapobadili imani na misimamo yake, inatia Shaka mno uhalali wa dini yenyewe.
Ukipewa andiko la Biblia,tafadhali naomba unitag. Ni mambo waliyojiwekea RC wenyewe,lakini Biblia haina kitu hicho.Bro, kwani wakiruhusiwa kuoa, nini kitaharibika, hii sheria kwamba wasioe ilitokea wapi kwenye Bibilia?
Imeandikwa wapi ni amri????Yani amri ya Mungu ina amriwa kufutwa au kutofuatwa.
Yeye ana mamlaka ya kufuta amri kama vile kaileta yeye.
Mkuu hujaelewa lengo la kuruhusu waoe sio kwamba mapadri ndio wanataka bali vijana wengi wanaukacha upadri kisa hataoa, sasa huko brazil kuna uhaba wa mapadri sana yaani watu wanaojiunga na upadri ni wachache kuliko mapadri wanaodednitashangaa sana na hili haliwezi kutokea, anayeshindwa mashariti anayo ruhusa ya kuacha upadre na kuoa, kwa nini wanataka vyote? isitoshe hata wakiruhusiwa kuoa si kwamba ndo hawatatenda dhambi, kuna watu wana ndoa na bado wanatoka nje ya ndoa zao.
Ndoa kwa mashoga haijawahi hata kujadiliwa maana haijadiliki na hakuna askofu hata wa kuuliza hilo maana ni sawa na kujadili Yesu ni Mungu? Kilijadiliwa namna ya kuwahudumia mashoga ili shoga anayetafuta uso wa Mungu asitengwe kwa sheria kali ....habari za Kanisa Katoliki zinapotoshwa sana ....bora ukosome habari kama hizi kwenye sources za Kanisa then ujue ukweli ....Mapadri kuoa inajadilika na kuendana na nyakati hizi inawezekana kulegezwa na kutoa fursa hiyo ....Hataweza...
Hili litafeli kama lilivyofeli lile:-
La kuruhusu Ndoa za Mashoga lilivyofeli.
Haiwezekani...
Taarifa hii haina ukweli wowote Bali ni kati ya fake news nyingi, simply haiwezekani!View attachment 623282
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amependekeza kubadili mfumo wa utumishi wa mapadre akisema itakuwa vyema iwapo makasisi hao wakaruhusiwa kuanza kuoa.
Hata hivyo, imefahamika kuwa pengine pendekezo hilo likawaruhusu mapadre wa Brazil pekee kutokana na mjadala unaoendelea nchini humo. Hivi karibuni Askofu wa Brazil, Kadinali Claudio Hummes alimwomba Papa Francis kufikiria kuondoa sheria inayowakataza makasisi kufunga ndoa.
Ingawa pendekezo hilo la Papa Francis huenda likapunguza tatizo la uhaba wa wanaume wanaojiunga kwenye utumishi huo, lakini linatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa waumini wenye msimamo mkali na hata pia kusababisha mgawanyiko ndani ya kanisa.
Ombi hilo linatarajiwa kujadiliwa katika kikao cha baraza la kanisa kinachotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Brazil.
Kanisa Katoliki linahubiri mafundisho ambayo yanapiga marufuku makasisi wake kufunga ndoa ingawa kumekuwa na baadhi wanaovunja mwiko huo na kuisha maisha ya ndoa. Hata hivyo, wale wanaochukua uamuzi huo hujitenga na kanisa.
Kasisi moja aliyetambulika kwa jina la Paddy O’Kane amenukuliwa na baadhi ya magazeti akielezea uwezekano wa Papa Francis kuchukua uamuzi wa kuwafungulia mapadre kifungo cha kutokua wakati wowote mwezi huu.
“Hivi karibuni nilimsikia Papa anataka kutekeleza ombi alilolipata toka Brazil kama jaribio lake la kwanza,” alisema.
Papa Francis na mtangulizi wake, Benedict XVI wamekuwa wakieleza kuwa suala la makasisi kutoruhusiwa kuoa siyo jambo lisiloweza kubadilika na kwamba jambo hilo linajadilika.
Chanzo: Mwananchi
Hata wachungaji na mashehe wanaooa wana kesi hizoWe’re on the same page Mkuu. Kumbuka pia zile kesi za kulawiti USA na Europe.
Daah nayaona mamlaka ya dini yaliyo mikononi mwa mtu,"Lolote mtakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lolote mtakalofungulia duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni."
Kwani peoples wifes waliooa hawafanyi?Ni wazo zuri, wawe wanaruhusiwa kuoa au kutokuoa. These choices should be available them. It will reduce or stop many serious problems like secrets affairs with other people wives, Pedophilia activities, sodomy and rapes etc.