Papa afikiria kuruhusu mapadri waoe

Ama kweli, dini inapobadili imani na misimamo yake, inatia Shaka mno uhalali wa dini yenyewe.

Inaonyesha ni mambo ya watu wachache walijifungia na kutunga,muda wowote eti dini inaweza kubadili msimamo wa kiimani. Hii ndo kwanza nasikia kwa wenzetu hawa. KKKT afadhali baada ya kuujua ukweli,wakatupilia mbali nadharia za kusadikika.

Dini bora hujali maandiko yanasema nini na siyo sheria za watu kujipangia mambo ambayo hata Yesu hakulisemea. Anyaway tuhitimishe kuwaachia waumini wao,ila za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Sisi tunatoaa sadaka kuwalea mapadri wetu sasa wakioa si ndo watafany ni urithi wa familia zao
 
Yani amri ya Mungu ina amriwa kufutwa au kutofuatwa.
Yeye ana mamlaka ya kufuta amri kama vile kaileta yeye.
 
Mi nlifikiri tunatakiwa kufuata amri za Yesu na sio wanadamu??
Waliokataza mwanzo walitumia sababu zipi ambazo yeye ameona hazina tena maana??
 
Itakua kasevu maana kidume kilicho kamilika kisigonge!! Nyege hazina Ubaunsa
 
nitashangaa sana na hili haliwezi kutokea, anayeshindwa mashariti anayo ruhusa ya kuacha upadre na kuoa, kwa nini wanataka vyote? isitoshe hata wakiruhusiwa kuoa si kwamba ndo hawatatenda dhambi, kuna watu wana ndoa na bado wanatoka nje ya ndoa zao.
Mkuu hujaelewa lengo la kuruhusu waoe sio kwamba mapadri ndio wanataka bali vijana wengi wanaukacha upadri kisa hataoa, sasa huko brazil kuna uhaba wa mapadri sana yaani watu wanaojiunga na upadri ni wachache kuliko mapadri wanaoded
 
WA wawaache tu waoe, ila na masister nao waolewe. Ila lazima niongeze mke WA 2
 
Hakuna jambo ambalo halina faida! Pamoja na kwamba si agizo la kibiblia kuoa au kutooa bali ni utashi wa mtu mwenyewe katika kuitawala tamaa ya mwili! Aliyeweka utaratibu huu alilenga hasa kutengeneza kanisa kama taasisi yaani kumwondolea mtumishi mambo yanayoweza kumpelekea kuwa na tamaa hasa za mali, kwa mfano huwezi mwambia mtu mwenye familia kwamba sadaka hii ni ya Kanisa wakati ana watoto na mke wanaodai matumizi.

Pili ili hawa watu waishi pamoja kama ndugu lazima wasiwe na familia au umiliki wa Mali bali ukiruhusu kimoja lazime na kingine ukiruhusu( Mali na familia), ili limesaidia katika kulinda kanisa kwa mihongo mingi sana tangu kuanzishwa kwake.

Unaweza fanya utafiti kidogo kuhusu utitiri wa Makanisa ya kileo, sababu kubwa ya mmeguko huu ni kutafuta mali lakini si kulifundisha neno maana hata huko huyo nabii au mchungaji alikotoka wanafundisha neno hilo hilo na haya yanachangiwa na watumishi kuwa na wategemezi ambapo akikaa chini ya Kiongozi flani hawezi ishi katika ukwasi anaotaraji.

Hivyo basi ili Papa abadili utaratibu wa utumishi wa mapadre inabidi abadili pia mfumo wa uendeshaji wa kanisa yaani Kanisa lisiwe taasisi bali liendeshwe kama makanisa yakilokole au Lutheran ambapo Padre atakuwa na utaratibu na Mamlaka kamili ya kuendesha Kanisa katika eneo lake kama utashi wake utakavyokuwa. Athari ya hili ni kumeguka kwa Kanisa katika kiwango kisichotegemewa utaanza kusikia kanisa la Padre flani flani.
 
YAni mtu mmoja anaamua kubadiri vitu kama Mungu wao vile.
Mambo yanabadirika kwenda na wakati hayana misingi thabiti ni sawa na siasa za nchi, yani vitu haviendi kwa reference ya mwongizo wa kitabu cha biblia.
 
Hataweza...

Hili litafeli kama lilivyofeli lile:-
La kuruhusu Ndoa za Mashoga lilivyofeli.
 
Hataweza...

Hili litafeli kama lilivyofeli lile:-
La kuruhusu Ndoa za Mashoga lilivyofeli.
Ndoa kwa mashoga haijawahi hata kujadiliwa maana haijadiliki na hakuna askofu hata wa kuuliza hilo maana ni sawa na kujadili Yesu ni Mungu? Kilijadiliwa namna ya kuwahudumia mashoga ili shoga anayetafuta uso wa Mungu asitengwe kwa sheria kali ....habari za Kanisa Katoliki zinapotoshwa sana ....bora ukosome habari kama hizi kwenye sources za Kanisa then ujue ukweli ....Mapadri kuoa inajadilika na kuendana na nyakati hizi inawezekana kulegezwa na kutoa fursa hiyo ....
 
Kwani vipapa havioi? Na kama hawaoi matamanio yao wanayapeleka wapi na wanakula wanashiba?
 
View attachment 623282

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amependekeza kubadili mfumo wa utumishi wa mapadre akisema itakuwa vyema iwapo makasisi hao wakaruhusiwa kuanza kuoa.

Hata hivyo, imefahamika kuwa pengine pendekezo hilo likawaruhusu mapadre wa Brazil pekee kutokana na mjadala unaoendelea nchini humo. Hivi karibuni Askofu wa Brazil, Kadinali Claudio Hummes alimwomba Papa Francis kufikiria kuondoa sheria inayowakataza makasisi kufunga ndoa.

Ingawa pendekezo hilo la Papa Francis huenda likapunguza tatizo la uhaba wa wanaume wanaojiunga kwenye utumishi huo, lakini linatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa waumini wenye msimamo mkali na hata pia kusababisha mgawanyiko ndani ya kanisa.

Ombi hilo linatarajiwa kujadiliwa katika kikao cha baraza la kanisa kinachotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Brazil.

Kanisa Katoliki linahubiri mafundisho ambayo yanapiga marufuku makasisi wake kufunga ndoa ingawa kumekuwa na baadhi wanaovunja mwiko huo na kuisha maisha ya ndoa. Hata hivyo, wale wanaochukua uamuzi huo hujitenga na kanisa.

Kasisi moja aliyetambulika kwa jina la Paddy O’Kane amenukuliwa na baadhi ya magazeti akielezea uwezekano wa Papa Francis kuchukua uamuzi wa kuwafungulia mapadre kifungo cha kutokua wakati wowote mwezi huu.

“Hivi karibuni nilimsikia Papa anataka kutekeleza ombi alilolipata toka Brazil kama jaribio lake la kwanza,” alisema.

Papa Francis na mtangulizi wake, Benedict XVI wamekuwa wakieleza kuwa suala la makasisi kutoruhusiwa kuoa siyo jambo lisiloweza kubadilika na kwamba jambo hilo linajadilika.

Chanzo: Mwananchi
Taarifa hii haina ukweli wowote Bali ni kati ya fake news nyingi, simply haiwezekani!
 
Ni wazo zuri, wawe wanaruhusiwa kuoa au kutokuoa. These choices should be available them. It will reduce or stop many serious problems like secrets affairs with other people wives, Pedophilia activities, sodomy and rapes etc.
Kwani peoples wifes waliooa hawafanyi?
 
Back
Top Bottom