Dar es Salaam. Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Lumo wilayani Temeke, Isack Ernest alionja mauti baada ya kupigwa na wananchi kiasi cha kufikiriwa kwamba amekufa, akapelekwa chumba cha maiti ambako alizinduka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alisema jana kwamba kijana huyo alipigwa hadi kupoteza fahamu na alipofikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke aliwekwa kwenye chumba cha maiti pamoja na kijana mwingine aliyeuawa katika tukio hilo.
“Mwanafunzi huyo hali akiwa amelazwa pamoja na maiti nyingine zinazosubiri kuwekwa katika majokofu, alitikisika kutokana na baridi ya chumba cha maiti, wahudumu wakamwona na kumtoa, wakamvalisha nguo za maiti nyingine, akarudishwa hospitalini kwa ajili ya huduma,” alifafanua Kamanda Muroto.
Watu wakipelekwa mochwari kuna sindano wanachomwa kabla ya kuwekwa kwenye fridge ili wasiharibike!Sindano ipi?
Jina lake nani vile, ana bahati kweli kucheleweshwa wale ndugu zetu tungesha sahauAna bahati kwa sababu wamemchelewesha tu
Tunakuwa tumebeba panga bro,tushavuta cha Arusha na kubugia toti kibao za Valuu.Wanaume wa dar bhana!! Yani tumadogo twa miaka 16 tunazinguwa kitaa du!!! Si twa kuzaba vibao tu
hii kauli nilikuwa nasubiriaWanaume wa Dar buana hata kupiga hamjui!
Imekufikia mkuuhii kauli nilikuwa nasubiria
Kesi za namna hii ni nyingi sana Africahili linaprove kwamba ile case ya singida kuna some possibility ilikuwa kweli basi ndugu zetu wengi hufia makaburin
basi inasikitishaKesi za namna hii ni nyingi sana Africa