MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 766
- 1,568
Pamoja na kupania na kukamia mno katika michuano ambayo timu zingine makini iliyachukulia kama sehemu ya kupima baadhi ya sajili zake huku zikipeleka vikosi B na kujàribu baadhi ya wachezaji wa u20 kwa ajili ya kutunza nguvu ya vikosi vya kwanza kwa mashindano makubwa na kuepuka majeraha kwa wachezaji tegemeo kwa ajili ya mashindano makubwa
Hali ambayo imeķuwa tofauti kwa Simba sc ambayo yenyewe ikapeleka kikosi cha kwanza ambacho kilishuhudiwa kucheza katika mashindano ya CAF dhidi ya Wydad, Asec na Jwaneng n.k
hii inaonyesha kwamba timu hii yenye makazi yake msimbazi pamoja na kupeleka kikosi cha kwanza bado haina uwezo wa kutunishiana misuli hata na vilabu vidogo kama mlandege ambao wamewaadabisha vikali mithili ya mbuzi aliyemwagiwa maji ya moto katika michuano hiyo.Je, kama kikosi cha kwanza hali ni hii, Je ingepeleka kikosi B pamoja vijana wa u20 hali ingekuwaje, Je, isingekuwa mwanzo wa 5G zingine?
Inasikitisha sana.