Albedo
JF-Expert Member
- Feb 24, 2008
- 5,559
- 1,452
Ni mikakati gani basi ambayo hawa wapiganaji wanaweza kuitumia kuelekea na hatimaye kujiletea ushindi?
Nina Maswali kwa Wapiganaji na wale watetezi wa Wapiganaji na Mbinu Zao
1: Kwa Kuwa wao wanadai wanapambana dhidi ya Mafisadi, je ni mikakati gani wanayoweka kuhakikisha hao wanaowadhani ni Mafisadi hawarudi Mjengoni?
2: Hii inanipa shaka kwa sababu
Wapiganaji wanadai wanapambana na Mafisadi, lakini the battle ground ni katika Majimbo yao at least basi wangehamishia uwanja wa Mapambano katika kuhakikisha hao Masifadi hawarudi Mjengoni au wanadhani wapiga kura wa Kyela wana uwezo wa Kubadilisha matokeo ya Bariadi Mashariki?
3: Nimesikia katibu mwenezi Chiligai amesema wanawaunga Mkono, Chiligati huyu huyu aliwaambia Wapiganaji wanaligeuza Bunge Ze Commedy, sasa wao wanasimama wapi?
4: Je hawaoni kwamba wanapowaambia watu wapokee rushwa ni kinyume na Maadili ya Viungozi, je wamesahau kwamba Rushwa kwangu ni mwiko sitapokea wala kutoa Rushwa? naongezea " Wala sitahamasisha Rushwa"?
Mimi ningewaona Vidume kama wangeenda katika Majimbo ya hao wanaowaita Mafisadi na kuwaelimisha wananchi wasiwarudishe Mjengoni, vinginevyo ninawaona Waoga kama KUKU